Monday, October 12, 2015

MAMA SAMIA ATIKISA KWA KAMPENI KATIKA MAJIMBO YA SHINYANGA, ATINGA GEITA KWA KISHINDO

 Wananchi wakiwa wamezuia msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika eneo la Tinde jimbo la Msalala mkoani Shinyanga, wakati ukiwa njiani kwenda Kahama mkoani humo Oktoba 11, 2015.
 Mama akiwa amekwenda na watoto wake, kumshuhudia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi
ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan msafara wa Mgombea huyo ulipoziwa na wananchi katika eneo la Tinde jimbo la Msalala mkoani Shinyanga, wakati ukiwa njiani kwenda Kahama mkoani humo.
 Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakishushwa kwenye Pick Up walipowasili kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika jimbo la Kahama mkoani Shinyanga .
 Wasanii wa Bongo Movie wakiwasalimia wananchi baada ya kuwasili kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, uliofanyika jana katika jimbo la Kahama mkoani Shinyanga
 Kiongozi wa kundi la kamapeni za CCM la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mangele maarufu kwa jina la Steve Nyerere, akihamaisha wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Kahama mkoani Shinyanga.
 Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Kahama mkoani Shinyanga.
Wasanii wa kundi la kampeni la Ninesttuka, wakishambulia jukwaa kuhamasisha wananchi wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Kamaha mkoani Shinyanga.
 Mgombea Ubunge jimbo la Kahama mkoani Shinyanga, Jumanne Kishimba, akiomba kura kwa wananchi, katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo hilo mkoani Shinyanga.
 Kada wa CCM ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda,  akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Kahama mkoani Shinyanga.
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Kitaifa Chrisopher Ole Sendeka akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Kahama mkoani Shinyanga.
 Baadhi ya viongozi wa CCM wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wakiwa kwenye mkutano wa kampeni wa Mama samia uliofanyika katika jimbo la kahama.
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Kamaha mkoani Shinyanga
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Kitaifa, Angela Kizigha, akisalimiana na  Mjumbe wa NEC, Gasper Kileo katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Kahama mkoani Shinyanga.
 Mgombea Ubunge jimbo la Msalala, Ezekiel Maige akisalimia wananchi wakati msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hasaan ulipozuiwa na wananchi katika eneo la Nundu mkoani Shinyanga.
 Mgombea Ubunge jimbo la Msalala, Ezekiel Maige (kushoto) akikimbia kuwahi gari lake, bada ya kusalimia wananchi
wakati msafara wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia
Suluhu Hasaan ulipozuiwa na wananchi katika eneo la Nundu mkoani
Shinyanga.
 Wananchi wakiwa katika shamrashamra wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Nyang’wale mkoani Geita.
 Wananchi wakiwa na bango kumfikishia ujumbe, Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM,Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Nyang’wale mkoani Geita
 Mgombea ubunge jimbo la Nyang’wale Hussein Amar akiomba kura wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika  katika jimbo hilo mkoani Geita
 Mkuu wa mkoa wa Geita Fatma Mwasa (kulia) akijadiliana jambo na wajumbe wa kamati ya kampeni za CCM kitaofa, Angela Kizigha na Christopher Ole Sendeka katika mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Nyag’wale katika mkoa huo.
 Swaga za wananchi a jimbo la Nyang’wale
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika jana katika jimbo la Nyang’wale mkoani Geita.
PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

No comments:

RAIS SAMIA AWAINUA PIKIKIPI 37 MAAFISA UGANI WA KILIMO KIBAHA TC

  NA VICTOR MASANGU, KIBAHA Halmashauri ya Kibaha mji imepokea jumla ya pikipiki zipatazo 37 kutoka serikalini kupitia Wizara ya kilimo ...