Saturday, October 10, 2015

KUGUNDULIKA KWA GESI BAGAMOYO KUTASAIDIA KUIMARISHA UJENZI WA VIWANDA NA UCHUMI

 Na Mwandishi Wetu, Bagamoyo
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John
Magufuli, amesema kugundulika kwa gesi ya Bagamoyo mkoani Pwani
itasaidia kuimarisha uchumi na ujenzi wa viwanda nchini.
Hayo ameyasema leo wilayani Bagamoyo katika mikutano yake
ya kampeni iliyofanyika katika majimbo ya Chalinze na Bagamoyo, ambapo
amesema gesi hiyo itasaidia ujenzi wa viwanda katika serikali take.
“Kwanza niwapongeze kwa kugundua gesi hapa Bagamoyo, tena
imegunduliwa katika eneo la ruvu. Na hii itakuwa na manufaa kwa uchumi
wa Taifa na kwa wananchi wa Pwani kwa ujumla.
“Gesi hii itasaidia sana ujenzi wa viwanda vya kisasa
katika serikali ya Magufuli ya awamu ya tano. Tutajenga viwanda na
tutatoa ajira za uhakika kwa vijana wa nchi hii pamoja na Tanzania
yote,” amesema Dk. Magufuli
 Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea ubunge wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa (kushoto) na jimbo la Chalinze Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
 Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge
wa jimbo la Bagamoyo Dk. Shukuru Kawambwa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
 Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge
wa jimbo  jimbo la Chalinze
Ndugu Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.
 
Mgombea ubunge
wa jimbo  jimbo la Chalinze
Ndugu Ridhiwani Kikwete akimnadi mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Majengo,Bagamoyo.

No comments:

Rais Samia Aongoza Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jijini Dodoma

Dodoma, 18 Januari 2025 – Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameo...