Wednesday, October 07, 2015

DK. JOHN POMBE MAGUFULI: NITASHUGHULIKA NA WANAOHUJUMU UMEME TANESCO, AWAAMBIA WATUBU DHAMBI ZAO KABLA HAJAINGIA IKULU

????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahesabia Pushup wananchi  waliojitokeza na kuamua kuunga mkono  (Magufulika Style) iliyoasisiwa na Dk. John Pombe Magufuli kuonyesha Ukakamavu hivi karibuni mjini Karagwe mkoani Kagera.
Magufurika Style hiyo imefanyika leo kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Ngareselo  Usa Liver wilaya ya Arumeru mkoani Arusha  wakati alipofanya mkutano wa kampeni na na  kuwaomba wananchi wa mji huo  kumpigia  kura za ndiyo ifikapo Oktoba 25 mwaka huu katika uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika nchini kote na kushirikisha vyama mbalimbali vya kisiasa.
Katika mkutano wake wa Moshi mjini Dk. Magufuli amewaonya watendaji wa Shirika la Umeme nchini TANESCO na kuwaambia kama wanazima umeme makusudi ili kuwafanya wananchi waichukie serikali wanafanya makosa na ole wao kwa vitendo hivyo visivyo vya kistaarabu, Amewaambia kwamba bado siku 17 za kampeni akichaguliwa na wananchi na kuapishwa atawashughulikia ipasavyo kwani  wanajulikana. Hivyo akawaambia  “Katika siku hizi zilizobaki watubu wafanye kazi umeme uwake bila kukatika na kusumbua wananchi vinginevyo akiingia ikulu atalala nao mbele”.
Mgombea huyo wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli amehutubia mikutano mbalimbali mkoani Arusha na Kilimanjaro katika miji ya Usa Liver, Siha, Hai, Uru Moshi vijijini na kufanya mkutano mkubwa ulioonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha Star TV mjini Moshi.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MOSHI)
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na  Wananchi hao wakionyesha alama ya Dole inayotumiwa na CCM mara baada ya kufanya Magufulika Style kwenye uwanja wa Ngareselo Usa Liver wilayani Arumeru.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa jiji la Moshi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mkoani Kilimanjaro.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwaimbisha wananchi katika mkutano huo baada ya kumwaga srea zake wakati akiomba kura kwa maelfu ya wananchi hao.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukiwa  umefurika kwenye mkutano huo wa CCM wa kampeni katika viwanja vya Mashujaa  jijini Moshi.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Moshi mjini Ndugu Davis Mosha wakimsikiliza Bw. Lema aliyekuwa kiongozi wa Chadema wilayani Hai wakati alipojiunga na CCM katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumkabidhi ilani ya uchaguzi Ndugu Davis Mosha mgombea ubunge jimbo la Moshi mjini.
????????????????????????????????????
Davis Mosha mgombea ubunge jimbo la Moshi mjini na madiwani wa Moshi mjini wakimagufulika jukwaani kuonyesha ukakamavu wao.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na mgombea ubunge wa jimbo la Moshi mjini wakiwapungia mikono wananchi wakati Dk. John Pombe Magufuli alipokuwa akimnadi mgombea huyo wa moshi mjini katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Bibi akionyesha ukakamavu wakati mkutano huo ukiendelea.
????????????????????????????????????
Nyomi ilivyokuwa katika viwanja vya Mashujaa mjini Moshi.
????????????????????????????????????
Dk. Emmanuel Nchini akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli mjini Moshi.
????????????????????????????????????
Mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka akimnadi Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli mjini Moshi leo.
????????????????????????????????????
Aliyekuwa Mjumbe wa Baraza kuu la Chadema kutoka wilaya ya Monduli ambaye amejiunga na CCM kwa sasa akimpigia debe Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
Mjumbe wa Kamti ya Ushindi ya CCM Ndugu Christopher Ole Sendeka akimsikiliza kwa makini Dk Emmanuel Nchimbi katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Siha.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa mji wa Same katika mkutano wa kampeni uliofanyika stendi ya Maroli mjini Hai.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi ukiwa umefurika katika mkutano huo uliofanyika kwenye stendi ya maroli mjini Hai mkoani Kilimanjaro leo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli alipkuwa akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Mashujaa mjini Moshi leo.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Siha Mh. Agrey Mwanri.
????????????????????????????????????
Umati wa wananchi waliojitokeza katika mkutano wa kampeni mjini Siha wakiwa katika mkutano huo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Siha.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akifurahia jambo wakati Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerari Mrisho Sarakikya akisalimiana na Alhaji Abdallah Bulembo Mjumbe wa Kamti ya Ushindi ya CCM ambaye anaongozana na msafara wa Dk. John Pombe Magufuli wakati msafara huo uliposimama Usa Liver kwa ajili ya kuwahutubia wananchi na kuomba kura.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza mgombea ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Bw. John Daniel Palangyo mjini Usa Liver Arumeru.
????????????????????????????????????
Baadhi ya wananchi wakifurahia hotuba ya Dk. John Pome Magufuli mjini Usa Liver Arumeru.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwanadi baadhi ya wagombea wa ubunge na udiwani mkoani Arusha 
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Dk. Emmanuel Nchimbi, katikati ni Alhaji Abdallah Bulembo.
????????????????????????????????????

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiimba wimbo maalum wa Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
????????????????????????????????????
Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli na viongozi mbalimbali wakishiriki kuimba wimbo huo.
????????????????????????????????????
????????????????????????????????????
Vijana wa Yamoto Bandi wakifanya vitu vyao jukwaani katika mkutano huo uliofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Rais wa Sierra Leone Awasili nchini

Rais wa Jamhuri ya Sierra Leone, Mheshimiwa Julius Maada Bio, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wak...