Thursday, July 29, 2010

Dk Slaa afunika Arusha


Mgombea wa urais wa Jamhuri wa Muungano kupitia Chama cha Deomkrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, akiwahutubia maelefu ya wakazi wa mji wa Arusha, ambao walijitokeza kumdhani, katika Uwanja wa NMC leo. Picha na Joseph Senga.

Kikwete awaapisha Naibu Makatibu Wakuu 9



RAIS Jakaya Kikwete jana amewaapisha Naibu Makatibu wakuu tisa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Walioapishwa katika halfa hiyo ni Hussein Katanga, Maria Bilia, Nuru Milao, Balozi Herbert Mrango, Balozi Rajab Gamaha, Dk Yohana Budeba, Mbogo Futakamba, Ngosi Mwihawa na Job Masima.
Uteuzi wa maofisa hao waandamizi wa serikali ulifanyika julai 15, 2010 na rais Kikwete na kutangazwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo julai 20 mwaka huu.
Kwa mujibu wa uteuzi huo Katanga anakuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Bilia anakuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Milao anakuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.
Balozi Mrango anakuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Balozi Gamaha anakuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Dk Budeba anakuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Futakamba anakuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mwihava anakuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na Masima anakuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Wakizungumza na Mwananchi mara baada ya kuapishwa, Dk Budeba alimshukuru rais Kikwete kwa kumteua na kusisitiza kuwa kilichokuwa mbele yake ni kuhakikisha kuwa anatekeleza majukumu yote ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Imeandikwa na
Fidelis Butahe. SOURCE: MWANANCHI

RAIS KIKWETE AKUTANA NA DR. ASHA ROSE MIGIRO IKULU.


Rais Jakaya Kikwete Akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rozi Migiro mara tu Baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es salaam na Kufanya naye Mazungumzo Leo 29.7.10 PICHA NA IKULU


Rais Jakaya Mrisho Kikwete Akimkaribisha Ikulu jijini Dar es salaam Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Dr. Asha Rozi Migiro leo asubuhi.

Fashion 4 Health with the Vodacom Foundation



• All set for the Black and Gold Gala event

• Top Models to Grace the Show

• Fashion For Health in aid of the Zanzibar Mental Hospital

VODACOM Tanzania, through Vodacom Foundation, will this year sponsor a charity fashion show (Fashion 4 Health black & gold gala night) by Mustafa Hassanali in aid of the Zanzibar Mental hospital in Zanzibar on July 30th.

The show is being in Zanzibar for the third year in a row and is organized by Explore Zanzibar.

“This is the third year in a row, we Hosting the Islands Premier and Biggest Fashion Show with Mustafa Hassanali , and we are All ready for Fridays Nights Gala SoirĂ©e”, said Maryam Olsen, Managing Director of Explore Zanzibar.

To support her calling, Vodacom Foundation and Mustafa Hassanali have joined forces to create a synergy that will benefit various people at the Zanzibar mental hospital.

“With The Best in Names from the Fashion Industry, Its My Responsibility as a creative entrepreneur to Give back to the Society in the smallest way possible, and together with various individuals From the Tanzanian Fashion Fraternity we lead the way”, stated Mustafa Hassanali, who together with Explore Zanzibar supports the work of the Mental Hospital of Zanzibar (Kidongo Chekundu).

Mustafa Hassanali, Tanzania’s most renowned fashion designer shall unveil his new creations Aptly named “Karafuu” inspired by the Cloves of Zanzibar at Zanzibar Serena Inn in Stone Town, with models from Dar es Salaam Like M’Net Face of Africa 2010 finalist Lillian Mduda, Kisura Tanzania 2009 Winner Diana Ibrahim amongst other top models and Former beauty queens. Also Part of this Event is Renowned Tanzanian Hair and Make up Artiste Rehema Samo.

For More Information just contact

Sitta aeleza alivyokamatwa na Takukuru




SIKU moja baada ya Takukuru mkoani Tabora kumnasa Waziri wa Maendeleo ya Jamiii Jinsia na Watoto Margaret Simwanza Sitta, jana aliibuka na kusema taasisi hiyo inawabambikia wananchi makosa ili waonekane wanafanya kazi.

Alisema kutokana na tukio lililompata juzi, sasa anawasiliana na wanasheria wake kuona achukue hatua gani dhidi ya maafisa wa Takukuru waliodai kumkamata kwa rushwa.

Waziri Sitta alisema kwamba juzi saa 7:30 usiku aliamshwa kwa mlio wa simu ya Catheri Sepetu iliyomwomba afike gesti ya Camise kuona mtoto mgonjwa. "Niliomba anielekeze gesti hiyo iko wapi ili niende kumwona huyo mgonjwa," alisema Mama Sitta.

Hata hivyo Magreti alidai kwamba kutokana kutoyafahamu maeneo hayo alimwomba katibu mwenenzi CCM manispaa Tabora wafuatane katika maeneo hayo aliyoambiwa na Sepetu.

Alisema alipofika karibu na njia ya kwenda katika gesti hiyo, wakatokea vijana zaidi ya sita na kusimamisha gari alipowahoji nyie ni nani ndipo walipotoa vitambulisho na kujitambulisha kwamba wao ni Takukuru na kwamba sasa yuko chini ya ulinzi.

Alisema walimchukua hadi ofisini kwao na kuanza kumpekua huku wakimwambia alikuwa akigawa rushwa kwa wajumbe.

"Nikahoji huyo ndiyo mgonjwa mliokuwa mnaniitia? Hawakumjibu badala yake waliendelea kunipekua mkoba wangu na mkoba wa mdogo wangu na kumwamrsisha katibu mwenezi Rashid Ramadhan akubali kwamba alikuwa akigawa fedha,"alisema Sitta.

"Katibu huyo alibaki anaduwaa kwani alichokuwa anajuwa ni kumsindikiza waziri kwa mgonjwa. Alishangaa kulazimishwa aandike maelezo kueleza kina nanni alikuwa anawagawia fedha. Akajibu siwezi kuandika wongo,"

Waziri Sitta aliendelea kueleza kuwa akiwa ofisini hapo, alimuuliza Sepetu kulikoni, naye alimjibu alilazimishwa kumpigia simu na baada ya kuwakatalia, walimpiga na kuchukua simu yake na kuanza kumpigia (Sitta) na ilipoita walimlazimisha aongee na waziri kwa maelekezo watakayompa.

"Niliwahoji iwapo mnafanya haya kwangu ambaye alau najua sheria kwa wale ambao hawajui inakuaje kama siyo kuwaonea wananchi na kupoteza fedha za serikali kuendesha kesi za kubambikiza."alieleza.

Waziri Sitta alisema iwapo viongozi wa Takukuru wataachwa kukemewa kuendelea na tabia hiyo, itakuwa vigumu kuelewa nani kabambikiwa kesi na nanni ana kesi halali. Habari ya Victor Kinambile. SOURCE:: MWANANCHI

Wednesday, July 28, 2010

Kura ya maoni yaiva Zanzibar



WAKATI ikiwa zimebaki siku mbili zipigwe visiwani Zanzibar heka heka zimeendelea huku pande mbili zinazovutana kuhusu kura hizo upande mmoja ukiwataka wananchi kutokubali kufitinishwa na kwa sababu za tofauti za kiitikadi kisiasa juu ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa na mwingine ukiipuuza.

Upande unaounga mkono kura hiyo umetoa ushauri jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Watu sita ya Baraza la Wawakilishi inayofuatilia kura za maoni, Ali Mzee Ali alisisitiza kura ya ndiyo ni muhimu alipokuwa akizungumza na wananchi mbalimbali katika kikao kilichoanza jana kisiwani humo.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja wa Madiwani na Masheha wa Mkoa wa Kusini Pemba jana Ali Mzee alisema kwamba hivi sasa kumeundwa utaratibu mmoja wa kuzika siasa za fitina, chuki na hasama ambazo zinahitaji kuepukwa kabisa na badala yake kujenga mustakabali mpya wenye matumaini wenye kuzingatia umoja na mshikamano kwa jamii.

“Nawasihi msikubali kufitinishwa mkapoteza watu wazuri kama ilivyotokea huko nyuma, nadhani nyote mnajua nini kilitokea kwa hivyo nasema tena nakuombeni sana msikubali kurudi katika balaa, tunahitaji umoja na amani zaidi kwa hivyo ni matarajio yangu kuwa mtatumia busara katika kupiga kura ya maoni kuchagua jambo jema na sio kurudi katika vurugu,” alisema Mwenyekiti huyo.

Wakati hayo yakiendelea baadhi ya watu wamekuwa wakisambaza mabango na baadhi ya vipeperushi wakipinga kura hizo za maoni Mjini Unguja. Bango limebandika katika maskani ya kaka ya Mwembe Kisonge ambayo ni kambi ya mmoja wa wagombea kila siku huwa kunaandikwa ujumbe unaofanana 'wana CCM Mseto ni hatari, kura ya maoni tia hapana.'
Mzee alisema Zanzibar hakuna upinzani bali kuna chuki na uhasama mkubwa miongoni mwa wananchi wa Unguja na Pemba hali ambayo inahtaji kurekebishwa na kuondolewa kabisa.

Alisema chaguzi zote zilizofanyika Zanzibar kuanzia Uchaguzi wa kwanza wa 1957 na zilizofuatia zilitawaliwa na vurugu na hata baada ya kurejea kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ushindani ulikuwa karibu sawa kwani katika matokeo ya Uchaguzi wa 1995 CCM ilishinda Viti 26 na CUF viti 24, lakini nchi haijatulia kabla na baada ya mapinduzi.

Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Juma Kassim Tindwa akizungumza katika mkutano huo, alisema Mapinduzi ya Januari 12, 1964 yalifanyika kuleta hali za watu sawa na kuondoa aina yoyote ya ubaguzi ambapo Afro Shiraz Party (ASP) hakikuwa na dhamira ya kuwafanya Waafrika kuwa juu ya watu wengine hivyo yanayotokea sasa ni kinyume na dhamira ya mapinduzi.

Aidha alisema Kisiwa cha Pemba kimepita katika kipindi kigumu sana cha kususiana mambo mbalimbali, vitendo vya kuhujumiana kuchomeana nyumba, kumwagiana tindikali mwilini na baadhi ya wanaume kuwapa talaka wake zao kutokana na ushabiki wa kisiasa. Imeandikwa na Salma Said. SOURCE:MWANANCHI

Tuesday, July 27, 2010

Dk Slaa atikisa Karatu



Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amkikabidhi fomu ya kugombea urais, kupitia chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa, wakati wa mkutano wa hadhara wa kuomba kudhaminiwa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu jana. Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Profesa Mwesiga Baregu.

Monday, July 26, 2010

Sita kortini kwa wizi wa fedha kimtandao




MHASIBU wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Justuce Katiti na wenzake watano jana walifikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka 10, likiwemo la kughushi na kujipatia Sh338.9 milioni kwa njia ya udanganyifu.
Kufikishwa mahakamani kwa wtau hao ni mwendelezo wa hatua zinazochukuliwa na mamlaka husika dhidi ya wizi wa kimafia wa mabilioni ya fedha ambao gazeti hili liliripoti katikati ya mwaka kuwa unafanyika kupitia taasisi mbalimbali za kifedha.
Wakili mwandamizi wa serikali, Fredrick Manyandahati, akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Aloyce Katemana, aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Fortunatus Muganzi, Robert Mbetwa na Gidion Otullo ambao ni wafanyakazi wa benki ya NBC.
Wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni mfanyakazi wa Barclays, Godwin Paulla na mfanyakazi wa kampuni ya Tourism Promotion Services (Tanzania) Limited, Joseph Kaplamai Rutto.
Manyanda alidai kuwa kati ya Septemba 29 na Oktoba 6, 2008 washtakiwa hao kwa pamoja walikula njama ya kuitapeli benki ya Baclays.
Alidai Septemba 29, 2008, kwa makusudi Godwin na Joseph walighushi nyaraka ya uhamisho wa fedha kwa njia ya mtandao (Request for Swift Tranfer form E. 17) wakijaribu kuonyesha kuwa kampuni ya Tourism Promotion Services (Tanzania) Limited imeomba Baclays kuilipa East Africa Procurement Services Limited Tanzania Sh338, 935,337.46 kama madai ya kuiuzia mahema na vifaa vya hoteli.
Wakili huyo wa serikali alidai washtakiwa hao waliwasilisha nyaraka hiyo Baclays na kujipatia kiasi hicho cha fedha kwa njia ya udanganyifu wakionyesha East Africa Procurement Services imelipwa fedha hizo na Tourism Promotion Services kwa kuuziwa mahema na vifaa hivyo vya hoteli.
Ilidaiwa kuwa Septemba 30 mwaka huo, Katiti alimdanganya mwajiri wake kinyume na Sheria namba 11 ya mwaka 2006 ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, kwa kuandaa taarifa potofu ya makusanyo ya fedha na kujaribu kuonyesha kuwa Tourism Promotion Services ilikuwa imelipa kodi ya Sh338.9 milioni kama ongezeko la thamani kwa mwezi Agosti.
Pia Katiti anadaiwa kughushi nyaraka nyingine Oktoba 6,2008 akionyesha kuwa kampuni hayo imelipa fedha hizo.
Manyanda alidai kuwa kati ya Septemba 29 na Oktoba 6, 2008 washtakiwa hao kwa pamoja walihamisha fedha haramu wakati wakijua kuwa chanzo chake ni kosa la jinai na kuzificha. Wanadaiwa kuzitoa fedha hizo kutoka akaunti namba 0121186000 iliyo CRDB kwenda akaunti namba 1065822 na 600283 za Baclays na nyingine namba 240603616 ya Benki ya Biashara ya Kenya (KCB).
Wote walikana mashtaka yote yanayowakabili na upande wa mashtaka uliomba kesi hiyo iahirishwe kwa sababu upelelezi upo katika hatua za mwisho na hakimu akaiahirisha hadi Agosti 9, huku washtakiwa wakinyimwa dhamana. Imeandikwa na Tausi Ally SOURCE: MWANANCHI

DC anaswa na rushwa




Dk Betty Machangu akifafanua jambo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuzungumzia tuhuma za kukamatwa na Takukuru akigawa rushwa kwa ajili ya kura za maoni za Ubunge viti maalumu mkoa Kilimanjaro. (Picha na Daniel Mjema)

&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&&

VITA dhidi ya rushwa ndani ya CCM vimezidi kushika kasi baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) kumtia mbaroni mkuu wa wilaya ya Kasulu, Betty Machangu akigawa rushwa kwa wajumbe.

Machangu ambaye anawania Ubunge wa viti maalumu kupitia mkoa Kilimanjaro, alinaswa na maofisa wa Takukuru sambamba na viongozi waandamizi wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) ngazi ya mkoa na Wilaya.

Kamanda wa Takukuru mkoa Kilimanjaro,Alexander Budigila, alisema tukio la kukamatwa kwa Machangu na viongozi hao lilitokea juzi saa 1:00 usiku katika Nyumba ya kulala wageni ya Safari Resort iliyopo Manispaa ya Moshi.

Machangu alinaswa na maofisa wa Takukuru akiwa amejifungia katika chumba namba 24 pamoja na viongozi hao ambapo baada ya maofisa hao kuingia ndani, walikuta vipeperushi vikiwa vimefichwa kwenye tanki la choo.

Pia katika chumba hicho, maofisa wa Takukuru walikamata bahasha ambazo juu zilikuwa zimeandikwa majina ya Wajumbe wa mkutano mkuu wa UWT wa uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika kesho mjini hapa.

Viongozi wanaoadaiwa kukamatwa pamoja na mkuu huyo wa wilaya ni Katibu wa UWT mkoani Kilimanjaro, Mariam Sagita, Katibu wa UWT wilaya ya Moshi mjini, Hadija Ramadhani na Hawa Sultani ambae ni mfanyabiashara.

Kwa mujibu wa Budigila, wajumbe ambao ni wapiga kura za maoni ya Ubunge viti maalumu walikuwa wakiingia kwa zamu katika chumba hicho ambapo walikuwa wakipewa kati ya sh50,000 na 100,000 kulingana na uzito wa mjumbe.

Hata hivyo akizungumza na waandishi wa habari baadae jana mchana katika Hosteli ya Umoja inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Machangu alikanusha tuhuma zote zilizoelezwa na Takukuru.

Machangu alifafanua kuwa siku hiyo akiwa njiani kuelekea katika hoteli hiyo saa 10:00 jioni, alikutana na watendaji hao wawili wa UWT mkoa na wilaya ambao waliona ni vyema wakapate chakula cha mchana pamoja.

“tulifika pale saa 10:00 na sio saa 8:00 kama Takukuru wanavyodai na tulipofika pale tukakuta eneo lote la hoteli liko full booked (limejaa) kwa hiyo kwa sababu za kiusalama nikaona nikodishe chumba kimoja tukitumie”alisema.

Dk.Machangu alisema sababu za kumfanya achukue tahadhari za kiusalama ni kutokana na tukio lililomtokea mwaka 2007 ambako alivamiwa na kunusurika kuuawa hivyo mahali popote anapokwenda anachukua tahadhari.

Alisema wakati chakula kilipokuja na kabla hawajaanza kula, ghafla mlango wa chumba walichokuwemo ulianza kugongwa katika hali ambayo haikuwa ya kistaarabu hali ambayo ilimfanya ahofie kufungua mlango huo.

“hakukuwa na suala lolote la rushwa kama Takukuru wanavyojaribu kuuleza umma…tatizo nimejengewa maadui wengi katika kinyang’anyiro hiki cha viti maalumu baada ya kuonekana nyota yangu inang’ara” alisema.

Alisema kutokana na nyota yake kung’ara, baadhi ya wagombea wanafanya mbinu za kummaliza kisiasa ili asiweze kushinda lakini akasema Mungu ndiye anayegawa riziki na anaamini wapiga kura wanaelewa kinachoendelea.

Alikanusha madai ya Takukuru kuwa amekuwa akitumia gari la ukuu wa wilaya ya Kasulu katika kampeni hizo na kusema gari hilo alilielegesha ofisi ya mkuu wa mkoa Kilimanjaro tangu Julai 12 aliporejea kutoka Dodoma.

Dk.Machangu aliitaka Takukuru kufanya uchunguzi wa kina katika suala hilo na kujiridhisha kabla ya kuamua kulipeleka suala hilo kwenye vyombo vya habari akisisitiza kuwa wakati wote amekuwa akisimamia maadili kikamilifu.

Sunday, July 25, 2010

MO apata ajali


Landcuiser (NYEKUNDU) ya mgombea ubunge Singida mjini,Hawa Ngulume,baada ya kugonga hiece kwa nyuma aliyokuwa amepanda mgombea mwingine Mohammed Dewji na kusababisha Dewji kurushwa na kugonga paa la hiece hiyo na kuumia. Picha na Gasper Andrew

Friday, July 23, 2010

Miss Vyuo Vikuu wa Vodacom 2010




Miss Vyuo Vikuu wa Vodacom 2010,Frola Martin akiwa ni mwenye furaha sana mara baada ya kutangazwa mshindi katika shindano hilo.

Askofu Desmond Tutu kustaafu shughuli za umma



Askofu mkuu wa kanisa la Kianglikana Desmond Tutu ametangaza kustaafu kwake kutoka shughuli za umma.

Mshindi huyo wa tuzo ya Nobel alikuwa mtetezi mkuu wa haki za binadamu na alipinga utawala wa ubaguzi wa rangi Aparthied nchini Afrika Kusini .

Desmond Tutu ametaja kilele cha kazi yake, kuwa siku aliyomtangaza Nelson Mandela kama rais wa kwanza wa Afrika Kusini aliyechaguliwa kidemokrasia, mwaka wa tisini na nne.

Aliwaambia wanahabari kuwa ananuia kupumzika na familia yake akitimia miaka sabini na tisa mwezi Oktoba mwaka huu.

Miaka michache kabla Nelson Mandela aachiwe huru, wakati harakati za ukombozi kutoka utawala wa ubaguzi wa rangi huko Afrika Kusini zili shika kasi, Askofu Desmond Tutu alikuwa mstari wa mbele.

Wakati wa maandamano ya kupinga serikali hiyo dhalimu, alijitokeza na vazi lake rasmi akiongoza waandamanaji. Mara kadhaa vurugu zilizuka na aliweka maisha yake hatarini akijaribu kutuliza pande zote mbili, hapo ikiwa ni vikosi vya usalama na wandamanaji waliokuwa na jazba mno. Na sio wakati wote alifaulu au hata kusikizwa.

Mara kadhaa askofu huyo kwa kanisa la Kianglikana aliikemea serikali na kuikumbusha kuwa sera zake zilikuwa zinakiuka upendo wa Mungu ndio maana akapewa jina la askofu wa wanasiasa. Ni juhudi hizo ambazo zilichangia yeye kupewa tuzo ya amani ya Nobel mwaka wa 84. Na kwa heshima hiyo Rais Nelson Mandela alimpa jukumu la kuongoza Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Afrika Kusini mwaka wa 95.

Monday, July 19, 2010

Nchunga, Mosha vigogo wa Yanga sasa



HATIMAYE Loyd Nchunga amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa klabu ya Yanga baada ya kushinda kwenye uchaguzi uliomalizika asubuhi hii ambao umefanyika kutoka siku ya jana na kuendelea mpaka leo katika ukumbi wa PTA viwanja vya Mwl. J.K.Nyerere barabara ya Kirwa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa ripota wetu na mdau wa Mzee wa Mshitu matokeo kamili yametangazwa na wingi wa kura zaidi ya 1500 zimemwendea Nchunga na nafasi ya makamu mwenyekiti tayari imeenda kwa mfanyabiashara wa mafuta Davis Mosha.

Mwisho Mwampamba aiwakilisha Tanzania big Brother


Mwisho Mwampamba akiingia ndani ya nyumbaa BBA na staili ya kufuga ndevu kwa chati...huku akisema kuwa siku hizi amekuwa bush man, mtu wa kijijini....! kutrokana na muwezo wam Mwisho Mwampamba kuvaa uhusika ni imani yetu kwamba anaweza kufika mbali katika shindano la BBA Stars mwaka huu tunamtakia kila mafanikio katika shindano hilo.

Sunday, July 18, 2010

CCM wameanza kampeni mapemaaaa




INAONEKANA Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameanza kampeni za mapema kabla hata ya kuruhusiwa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) baada ya kuwanadi wagombea katika mikoa mitatu sasa ikianziwa na Dodoma, ikafuata Zanzibar na sasa Dar es Salaam na wasipopigiwa kelele watazunguka tanzania nzima.

Leo Rais Kikwete kama inavyoonekana pichani katika viwanja vya Mnazi Mmoja amewanadi wagombea wake na kisha akawaonya vikali wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kupitia tiketi ya CCM, juu ya jaribio lolote la kujihusisha na vitendo vya rushwa.


Aliyesema yeyote atakayekamatwa akijibusisha na vitendo hivyo, hatasemahewa na badala yake ataishia mikononi mwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

''Fomu chukueni, lakini atakayebainika kupokea au kuchukua rushwa tutamkabidhi kwa Edward Hosea na timu yake wafanye kazi yao, sisi huko hatuko, tutakuwa tunafanya shughuli nyingine za kulijenga taifa,''alisema Rais Kikwete.

Katika hatua nyingine, mgombea huyo kupitia CCM aliwataka watendaji wa chama hicho wanaotarajia kuanza kazi ya kukabidhi fomu leo, kufanya hivyo bila upendeleo wa aina yoyote.

Alisema watendajia hao wasikubali kuegemea upande wowote na kwamba kinachotakiwa ni kuonyesha demokrasia ya kweli katika CCM, hasa ikizingatiwa kuwa muda wa makundi umekwisha.

''Mzee Msekwa alikuwa analala saa saba usiku kule Dodoma katika jitihada zake za kumaliza migogoro ndani ya chama, hivyo hatutegemei tena kusikia kuna makundi yanajitokeza ndani ya chama na wala hatutavumiliana,''alisema.

Alisema ni kweli kuwa kulikuwa na makundi ndani ya chama hicho lakini kutokana na jitihada za viongozi, tatizo hilo limemalizika.

Rais Kikwete aliwataka wagombea wa ngazi mbalimbali wa chama hicho na wabunge wahakikishe kuwa wanaoisoma vizuri ilani ya chama hicho na kuelezea mambo watakayowafanyia wananchi.

''Someni vizuri ilani ya chama muifahamu muwaelekeze wananchi katika kampeni zenu wajue mtawafanyia nini kipindi kijacho, ili wawaelewe na kama ulifanya vizuri watakukubali tu hivyo tujipange na tuitetee ilani yetu ,''alisema.

Kwa upande wake, mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya chama hicho, Dk Ali Mohamed Shein alitumia muda wake kumpongeza Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kwa kuwa kiongozi wa mafanikio.

Dk Shein alielezea maridhiano ya kisiasa yaliyofikiwa kati ya CCM na CUF, kuwa ni miongoni mwa matunda mazuri ya uongozi wa Rais Karume na kwamba atayaenzi.

Mizengwe Yanga Kifukwe ajitoa dakika za mwisho



Mgombea Uenyekiti wa timu ya Yanga Francis Kifukwe ametangaza kujitoa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa Yanga huku akisema," Mimi ni mtuhumiwa wa basi la Yanga nimeifanyia mengi Yanga, lakini mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kampeni nilidhani zimeisha tokea jana (juzi), lakini zinaendelea mpaka leo (jana)."

Baada ya kutangaza kujitoa vurugu zilitokea kwenye kambi ya Kifukwe ambapo watu wa kambi yake walianza kumtukana Ridhiwan na kulaani kauli aliyoitoa kwamba wanachama wasifanye makosa na kuchagua watu wanaokutana BAKURUTU.

Hata hivyo Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera aliingilia kati na kusema bado kamati haitambui mapinduzi ya Kifukwe kujitoa hivyo wale walio kambi ya Kifukwe watulie na uchaguzi uendelee na wanaomtaka Kifukwe wampigie kura na kama atashinda atatangazwa kuwa Mwenyekiti.

Bendera alifoka kwamba, "kuna njama zimepangwa na kikundi cha wanachama haiwezekani mtu ajitoe wengine mshikwe jazba, Kifukwe kajitoa muda ambao siyo muafaka, humu ndani Kifukwe hakuna kutoka mpaka kieleweke anayetaka kukupigia kura akupigie."

Baada ya Kifukwe kutangaza kujitoa mwanachama mmoja wa Yanga anayefahamika kwa jina la Hussein Makabureta aliangua kilio, huku wanachama wa kambi ya Kifukwe wengine waliondoka ukumbini bila kupiga kura na wengine walikuwa wakihamasishana kumpa Mbaraka Igangula kura zao.

Muda mfupi kupita Manji aliingia ndani akiwa na Kifukwe wanachama wanaompenda Kifukwe walimpigia makofi, lakini mfadhili huyo cha ajabu alitoka nje na wagombea wote wa nafasi ya mwenyekiti pamoja na Kifukwe halafu Manji akarudi tena akiwa na mabaunsa sita kwenda kupiga kura.

Inadaiwa kikao alichokifanya Manji na waliokuwa wakiwania nafasi ya mwenyekiti wa Yanga kilikuwa ni kuwashinikiza atakayechaguliwa kuwa mwenyekiti lazima amteue Kifukwe kuwa mjumbe wa baraza la wadhamini Yanga na Francis Kifukwe akichaguliwa kwenye nafasi hiyo lazima akubali ili kunusuru mpasuko ndani ya Yanga atakayekiuka Manji atajiondoa kuidhamini klabu hiyo. Taarifa zaidi baadaye

Wednesday, July 14, 2010

Soko la Pamoja EAC bado


NAIBU Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Beatrice Kiraso akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa idara ya habari maelezo ambapo amesema soko la pamoja la jumuiya hiyo bado halijaanza rasmi kama inavyodhaniwa kwasababu kuna mambo mengi ambayo hayajakamilika.

Kiraso ambaye anashughulikia shirikisho la kisiasa la jumuiya hiyo alisema jijini Dar es Salaam jana kuwa, soko hilo liliidhinishwa kuanza Julai Mosi mwaka huu lakini bado kuna mambo mengi ambayo hayajakamilika. (Picha na Mwanakombo Jumaa)-MAELEZO.

Breaking News Profesa Mwaikusa auawa na majambazi


Taarifa zilizotufikia muda mfupi uliopita zinaeleza kuwa yule nguli na mwanasheria ambaye pia ni Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu aliyetikisa katika kesi ya mgombea binafsi, Profesa Jwani Mwaikusa ameuawa kwa kupigwa risasi na majambazi waliovamia nyumbani kwake majira ya saa nne usiku.

Sambamba na mauaji ya Profesa huyo majambazi hayo pia yaliua mtoto aliyekuwamo ndani ya nyumba ya Profesa huyo na kisha kumuua jirani kwa kumpiga risasi, haijafahamika yamepora mali gani na nini lengolao hasa, mamlaka za serikali bado hazijathibitisha tukio hilli, taarifa hii imepatikana kutoka kwa ndugu wa karibu wa Profesa huyo.

Tuesday, July 13, 2010

Banda Samba Brazil LIVE in Dar es Salaam


DO NOT MISS THIS EXCITING,FANTASTIC SAMBA AND CAPOEIRA PERFORMANCE LIVE FOR THE FIRST TIME IN DAR ES SALAAM.THE SHOW WILL BE ON 16TH JULY FROM 20:00HRS..

FREE ENTRY

PLEASE SHARE THIS INFORMATION WITH YOUR FRIENDS.

Read the attached flier for more information

--
www.maishamusic.com
www.myspace.com/maishamusictz
www.youtube.com/maishamusictz
www.twitter.com/maishamusictz
www.facebook.com/group.php?gid=74932459086

Ajali ya basi la Hekima




Hivi ndivyo basi la Hekima Royal Class lenye namba za usajili T607 ARR lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Tunduma kupata ajali katika eneo la Ilula karibu na hoteli ya Al-Jaziira kabla ya kufika Mlima Kitonga kugongana na tela lililochomoka na kuacha njia wiki iliyopita.
Majeruhi wa ajali hiyo akiwemo dereva wa gari hilo walifikishwa katika hospitali mjini Iringa. Picha zote na Christina Njovu.

Monday, July 12, 2010

Mizigo sasa bila shaka haitarundikana bandarini


Winchi Panamax quay ya kampuni ya kupakua na kupakia makontena bandarini (TICTS) ikishushwa kutoka kwenye meli ya mizigo kwenye bandari ya Dar es Salaam jana, wichi hiyo ina uwezo wa kubeba kontena mbili za futi ishirini kwa wakati mmoja. Picha na Michael Jamson

Sabodo aigea Chadema Sh 100milioni


*ASIFU UMAKINI WAKE NDANI NA NJE YA BUNGE
*AWAPONGEZA MBOWE NA DR SLAA
*AAHIDI KUCHANGIA ZAIDI

Mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, Mustapha Jaffar Sabodo amekichangia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA shilingi milioni mia moja ili kuimarisha upinzani na demokrasia nchini.

Bw. Sabodo amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha leo jijini Dar kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe aliyeambatana na Katibu Mkuu wake Dr Wilibrod Slaa na Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho Bw. Antony Komu.

Akikabidhi hundi hiyo Bw. Sabodo amesema pamoja na kwamba yeye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi lakini anapenda kuona upinzani na demokrasia vinaimarika nchini huku akikitaja CHADEMA kuwa ni chama makini na safi cha upinzani.

Bw. Sabodo amekuwa mmoja wa wazee walio wazi katika kukosoa utendaji wa serikali ya chama chake CCM hasa inapokiuka misingi ya utawala bora iliyojengwa na Mwasisi wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.

“Mimi ni mwanachama wa CCM lakini napenda kuona demokrasia ikikua huku kambi ya upinzani ikiimarika kwa kuwa na wabunge wengi bungeni ili kushamirisha maendeleo nchini……na nawachangia CHADEMA kwa kuwa natambua umakini wenu katika siasa za hapa nchini na hasa Bungeni”, Alisema.

Bw. Sabodo amesema kuongezeka kwa wabunge wa upinzani bungeni ni jambo la muhimu katika kutoa upinzani kwa CCM na kusukuma maendeleo ya wananchi huku akikitaka CHADEMA kuongeza nguvu zaidi katika harakati zake za kisiasa na kumwelezea Dr Slaa kuwa ni mwanasiasa mwenye uchungu wa kweli na watanzania.

Aidha Bw. Sabodo amesema ana mpango wa kuichangia fedha zaidi CHADEMA ili kuimarisha harakati zake za kisiasa na kuahidi kufanya hivyo atakaporejea nchini akitokea India kwenye matibabu.

Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Bw. Sabodo Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameshukuru na kutaja msaada huo kuwa ni wa kihistoria katika siasa za vyama vingi nchini.

Amesema mara nyingi imekuwa ni vigumu kwa wafanyabiashara wakubwa wa kada ya Bw. Sabodo kuchangia kwa uwazi tena kiasi kikubwa cha fedha na kutaka hatua hiyo kuigwa na wafanyabiashara wengine nchini.

“Kwa kweli tunashukuru sana hii ni historia mpya katika siasa za vyama vingi nchini, ni wajibu wa wafanyabiashara wakubwa kuona umuhimu wa kusaidia vyama vyote makini nchini bili kuwa na ubaguzi wala woga, Mzee ameonyesha njia naamini itakuwa ni mfano kwa wengine wenye uwezo, Alisema Bw. Mbowe.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Dr Slaa ameshukuru kwa mchango huo na kudokeza kwamba mchango utatumika kwa kadiri ya vipaumbele vitakavyopangwa kwenye Kamati Kuu ya chama inayotarajiwa kufanyika tarehe 20 Julai 2010 ikilenga zaidi katika kutekeleza mipango endelevu ya kuimarisha chama kama Operesheni Sangara na utekelezaji wa mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

“Nawaomba watanzania wengine wa kada na uwezo mbalimbali kuichangia CHADEMA ili kuondokana na ukiritimba wa chama kimoja kwani ni hatari kwa maendeleo na usalama wa nchi kama michango yote ikielekezwa kwa chama tawala pekee.

"Natoa mwito kwa vyombo vya dola kuacha kuwatisha watanzania wenye mapenzi mema wanaochangia vyama mbadala kama CHADEMA kwani kufanya hivyo ni kuhujumu taifa na kukwamisha maendeleo ya nchi”, alisema


Imetolewa tarehe 12 Julai na:


Erasto Tumbo
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

Miss Africa USA 2010 GRAND FINALS AND CORONATION CEREMONY



Saturday July 24th 2010

A Cultural explosion of African heritage, high fashion, talent, models, entertainment.
A Night you cannot afford to miss.

Spotlight Africa LLC, African Women's Development Foundation Inc in Collaboration with
Montgomery County Government Presents Miss Africa USA 2010.

Montgomery County Tacoma Park / Silver Spring Performing Arts Center
7995 Georgia Avenue, Silver Spring, MD 20910
678-663-5892 or 678-886-5950

Show Time 6pm - 11pm

Tickets: $30 advance $40 at the Door

Maandalizi ya tamasha la tatu la ngoma za asili la kimataifa


Kikundi cha sanaa cha bendi ya Twetu Robo, wakifanya mazoezi kambini kwao Sinza jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni maandalizi ya tamasha la tatu la kimataifa kutafuta kikundi bora cha ngoma za asili litakalofanyika mjini Bagamoyo hivi karibuni. Picha na Venance Nestory
Mabasi ya mikoani
yaadimika Ubungo


ABIRIA wanaosafiri kutoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya bara wanalazimika kulipia nauli ya juu na wengine kukosa kabisa usafiri baada ya kutokea uhaba mkubwa wa mabasi kwenye Kituo Cha Mabasi cha Ubungo (UBT).
Kutokana na tatizo hilo magari madogo ya abiria maarufu kama daladala yamekuwa yakitumika kuwasafirisha baadhi ya abiria hao kutoka Dar es Salaam kwenda mikoani.
Habari zimeeleza kuwa tatizo hilo la kwanza kubwa kutokea limesababishwa na mabasi mengi makubwa kukodishwa na wamiliki wa shule mbalimbali za sekondari kwa ajili ya wanafunzi wao wanaotarajia kuanza masomo leo.
Gazeti hili ambalo jana lilikuwa kituoni hapo kwa takriban saa sita lilikuta abiria wengi wakirudi nyumbani kutokana na kukosa usafiri, huku baadhi wakionekana kukata tamaa kabisa.
Mkuu wa kikosi cha polisi wa usalama barabarani kituoni hapo, Hassan Hassan alisema usafiri kituoni hapo umekuwa wa taabu tangu Ijumaa iliyopita.
“Nimefanya kazi hapa kwa kipindi cha miaka minne, lakini sijawahi kuona idadi kubwa ya abiria kama niliyoiona safari hii wakishindwa kusafiri. Watu ni wengi ajabu; sijui ni kutokana na maonyesho ya Sabasaba au mabasi kukodiwa na wanafunzi lakini ukweli abiria ni wengi waliokwama,” alisema Hassan.
Abiria hao walilalamika kuwa upungufu wa mabasi umesababisha kupanda kwa nauli na kusababisha abiria kuitupia lawama Sumatra na Jeshi la Polisi kwa kushindwa kuchukua hatua kudhibiti ongezeko hilo la nauli.
“Tunakuja hapa tunaambiwa gari hakuna zipo coaster ambazo nauli yake ni Sh 30,000 hadi Sh35,000 gharama hizi ni kubwa na sisi tunashindwa kuzimudu,” alisema mama mmoja aliyekuwa akisubiri usafiri wa kwenda Arusha.
Hata hivyo mkuu huyo wa usalama barabarani kituoni hapo alisema tayari amekamata baadhi ya daladala hizo kwa kuwa hazina kibali cha kusafirisha abiria kwenda mikoani.
Alisema abiria wamekuwa wakirubuniwa na kukubali kutoa nauli kubwa lakini kwenye tiketi wanaandikiwa fedha kidogo, jambo linalotufanya askari kukosa ushahidi kwani kwenye risiti anaandikiwa Sh17,500 lakini anatoa Sh30,000 sasa utamsaidiaje huyu,” alisema Hassan.
Hassan alisema tatizo ni abiria kukubali kutoa fedha nyingi za nauli tofauti na nauli elekezi kutoka Sumtara.
Lakini mkuu huyo akasema kuwa upungufu wa ghafla wa mabasi umetokana na idadi ya abiria kuongezeka.
Alisema kutokana na sababu hiyo wakati mwingine ofisi yake imekuwa ikichelewa kuruhusu mabasi kutoka kituoni hapo kwa muda wa roba saa ili kusubili abiria ambao huchelewa kuingia kituoni humo kutokana na msongamano watu na magari.
Naye meneja mahusino kwa Umma wa Sumatra, David Mziray alisema ofisi yake haina taarifa juu ya tukio hilo na kuahidi kulifuatilia kuanzia leo. Imeandikwa na Geofrey Nyang’oro na Hussein Issa: SOURCE:MWANANCHI.

Mgombea Mwenza wa CCM ni Dk Gharib Bilal





BAADA ya kuangushwa mara tatu katika mbio za kuwania urais wa Zanzibar, nyota na nguvu za kisiasa za Dk Mohamed Gharib Bilal zilizidi kujidhirisha baada ya kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kwenye mbio za urais wa Muungano katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 31.
Uteuzi huo wa Dk Bilal, ambao ulitangazwa kwenye mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Kizota mjini Dodoma, umefanywa katika kipindi ambacho joto la kisiasa ndani ya CCM lilikuwa limepanda baada ya halmashauri kuu ya chama hicho kumtupa msomi huo kwa mara ya tatu kwenye mbio za urais.
"La mwisho kabla ya mwisho," alisema Kikwete na kuacha muda kidogo akisikiliza majibu yan wanachama ambao walipiga kelele kutaka kutangaziwa jina la mgombea mwenza atangazwe baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
"La mwisho kabla ya mwisho, nimemteua Dk Bilal kuwa mgombea mwenza."
Mara baada ya tamko hilo ukumbi mzima ulilipuka kelele za nderemo na vifijo, miruzi na maturumbeta mithili ya mavuvuzela huku Bilal akikumbatiwa na watu tofauti wakati akianza kuelekea kwenye meza kuu.
Wakati Bilal akipongezwa, kikundi cha muziki cha CCM, ToT Plus kilianza kutumbuiza huku Rais Kikwete akicheza muziki na uso wake ukiwa umepambwa kwa tabasamu kuonyesha kufurahishwa na kelele za wajumbe ambazo zilionyesha kukubali uteuzi huo.
Bilal alikwenda moja kwa moja kwenye meza kuu na kuwashika mikono viongozi wote, akimkumbatia Rais Kikwete na baadaye kwenda kwenye jukwaa lililokuwa likitumiwa kutoa hotuba kwa ajili ya kutoa shukrani. Hata hivyo, wajumbe waliendelea kujimwaga ukumbini kushangilia wakicheza muziki wa ToT.
Lakini wakati Dk Bilal akiendelea kusubiri wajumbe watulie ili azungumze, afisa mmoja alimwendea na kumnongeza jambo na ndipo waziri kiongozi huyo wa zamani wa Zanzibar alipoondoka na kurudi kwenye kiti chake.
Kabla ya kumtangaza Dk Bilal, Kikwete aliomba mkutano uende mapumziko kwa dakika 15 ili akutane na wajumbe wa kamati kuu, lakini kikao hicho kilichukua takriban nusu saa na aliporejea alianza na hotuba ndefu ya kueleza mafanikio na matatizo ambayo serikali ya awamu ya nne ilikutana nayo tangu mwaka 2006.
Awali majina mbalimbali yalikuwa yakihusishwa na nafasi hiyo, ikiwa ni pamoja na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha, waziri wa zamani wa fedha, Zakia Meghji, na Waziri wa Nchi, Mohamad Seif Khatibu ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais -Muungano kabla ya kitendawili hicho kuteguliwa saa 3:30 usiku. Imeandikwa na Exuper Kachenje, Dodoma na Ramadhan Semtawa, Dar. SOURCE: MWANANCHI.

Friday, July 09, 2010

Ajali haina kinga


Gari la kikosi cha zimamoto likiwa limepinduka katika eneo la Magomeni Mapipa, jijini Dar es Salaam jana , baada ya dereva kushindwa kulimudu wakati akijaribu kupishana na gari jingine. Picha ya Michael Jamson wa Mwananchi

Thursday, July 08, 2010

Kabudi: Propaganda inatumika EAC


Mkuu wa Kitivo cha Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mlimani(UDSM) Profesa Palamagamba Kabudi (katikati)akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa mkutano wa kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika soko la pamoja, kushoto ni kaimu mwenyekiti wa MCT na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi Theophil Makunga na kulia ni Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini, Neville Meena.Picha na Venance Nestory.
*************************************************
MSIMAMO wa Tanzania katika kuhakikisha inazilinda fursa mbalimbali zilizopo nchini ikiwemo ardhi, zinabaki kuwa chini ya miliki ya Watanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) umesababisha kuhujumiwa pamoja na kuenezwa propaganda chafu.
Propaganda hizo zinafuatia msimamo wa Tanzania kutokuwa tayari kufungua milango kwa nchi EAC kuingia nchini na kumiliki ardhi, kupewa ukazi wa kudumu pamoja na vitambulisho vya uraia kutumika kama pasipoti za kuingilia katika nchi hizo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na mjumbe wa Tanzania katika Kamati Maalumu ya majadiliano ya EAC, Profesa Palamagamba Kabudi katika mkutano wake na Jukwaa la Wahariri nchini.
Mkutano huo ulikuwa na lengo la kujua nafasi ya vyombo vya habari katika Soko la Pamoja la Afrika Mashariki lililoanza Julai Mosi mwaka huu.
Profesa Kabudi alisema baadhi ya nchi ndani ya jumuiya hiyo zinaisema vibaya Tanzania juu ya mambo zaidi ya saba ambayo hayamo kwenye jumuiya hiyo.
Profesa Kabudi ambaye pia ni Mkuu wa Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alifafanua kuwa katika suala la ardhi walikataa baada ya kuzingatia matokeo ya tafiti ambazo zilionyesha idadi kubwa ya Watanzania hawataki suala hilo kuingizwa katika ushirikiano.

Kuhusu suala la vitambulisho vya uraia kutumika kama pasi za kusafiria, alisema uamuzi huo ulifikiwa ili kulinda usalama wa nchi kutokana na Tanzania kuwa ndio nchi pekee barani Afrika kupakana na nchi kumi.

Kuhusu ukazi wa kudumu, Profesa Kabudi alisema kulingana na mazingira pamoja na jinsi fursa za ukazi zilivyo katika nchi za EAC, ni vigumu kwa Watanzania kwenda kuomba ukazi katika nchi hizo na kwamba wananchi wengi katika nchi hizo wangekimbilia nchini.

Hata hivyo, Profesa Kabudi alisema baadhi ya mambo ambayo Tanzania imefungua milango yake ni utoaji wa ajira, ujenzi wa hoteli za ghorofa pamoja na ujenzi wa shule.

Alisema uingizwaji wa masuala hayo katika Soko la Pamoja limezingatia maslahi ya taifa na hivyo Tanzania haipaswi kulaumiwa kwa lolote kwa kuwa hata katika mkataba wa EAC ibara namba 75 umeelekeza masuala mbalimbali yasiharakishwe kuingizwa katika ushirikiano.

Kuhusu kiwango cha elimu inayotolewa Tanzania alisema ni bora kuliko ya nchi nyingine isipokuwa wengi huishusha kwa kuithaminisha kwa lugha ya Kiingereza.
Alifafanua kuwa pamoja na kufunguliwa kwa itifaki ya soko hilo, Watanzania na nchi wanachama wasitegemee masuala yote yaliyokubaliwa kwenye soko hilo yatatekelezwa mara moja na kwamba mchakato wa utekelezaji wake utakwenda taratibu.
Alisema kila nchi inapofanya maamuzi juu ya suala lolote kwanza inazingatia maslahi yake na si vingenevyo.Imeandikwa na Sadick Mtulya na Hussein Kauli: SOURCE MWANANCHI

Ubunifu mpya huduma ya maji



Mkazi wa Temeke akiendesha Pikipiki aina ya Bajaji ikiwa na Tanki la maji safi tayari kwa kuuza mitaani, ambapo zimetolewa hivi kalibuni na Dawasco kwa ajili ya kurahisisha huduma ya maji kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, Picha na Elizabeth Suleyman.

Monday, July 05, 2010

Chissano ndani ya Bongo


Rais Jakaya Kikwete,akiwa na mgeni wake Rais mstaafu wa Msumbiji,Joachim Chisano,alipomtembelea Ikulu Dar es Salaam juzi kwa mazungumzo.(Picha na Yusuf Badi).

Sunday, July 04, 2010

Anayedaiwa kufa aibuka siku 40 baada ya kuzikwa




MAKAZI wa Msamvu mkoani Morogoro Khamisi Abdul  (47), aliyedaiwa kufariki Juni 9 mwaka huu na kuzikwa katika Makaburi ya Kola mjini humo, ameibuka huku akiwa hai.


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Bahati Abdul (24) ambaye ni mtoto wa Abdul alisema baba yake alifariki baada ya kujichoma na kisu tumboni na kwamba kabla ya mauti kumfika alipelekwa hospitalini na kulazwa.
 
"Baba alikuwa akijishughulisha na biashara  ya  kutembeza  sabuni mtaani  na alifariki Juni 9 baada ya kujichoma na kisu tumboni Mei 29 na ukweli hakuwa mgonjwa  wa  akili," alisema Bahati.
 

Akizungumza na waandishi wa habari jana Abdul ambaye alikuwa amepoteza  kumbukumbu  alisema anachokumbuka   ni kwamba alikuwa akilala  katika  pango lenye  nyoka na wanyama  wengi ambao hawakuweza kumdhuru.

 “ Mara nyingine nilikuwa natembea porini na kukutana na wanyama wakali, lakini cha kushangaza, wao ndio walikuwa wakinikimbia,” alisema Abdul
 
Alipoulizwa kuhusu familia  yake alisema anakumbuka alikuwa na watoto watatu kati  yao mmoja ndio wa kumzaa mwenyewe, wengine  wawili walikuwa watoto  wa  marehemu mkewe .
 
“Mtoto  wangu wa kumza anaitwa Muka Khamis,"  alisema Abdul kwa  shida .

Baadhi  ya  wafanyabiashara  katika soko la Sabasaba  ambako  Abdul  alikuwa akifanya biashara  walisema mara baada ta taarifa ya kifo cha Khamisi walitoa michango yao ya fedha.

Jalala  Uwezo  alisema alisema Khamisi alikufa mwezi Juni na walimzika katika makaburi ya Kola.
 
Tukio hilo lilivuta hisia za wengi mkoani humo, Nabii Joshua Aram wa  Kanisa  la Uponaji alimchukua  mtu  huyo na kwenda naye  maeneo ambayo anadaiwa  alikuwa akifanya biashara zake  kabla   ya kifo chake  ili kuthibitisha hali hiyo.

Akiwa huko kundi  la watu  walimzunguka  na kumshangaa  huku wengine  wakitokwa  na  machozi na kudai  kuwa alishakufa  na kwamba tangu alipofariki bado hazijatimia siku 40.
 
Akizungumzia  kupatikana kwa  Abdul, Nabii  Joshua   alisema wakiwa katika maombi  yao ya kawaida kuombea  wagonjwa nje  ya  uwanja  katika  eneo  la  Kihonda  Viwandani,   Abdul alitokea  akiwa katika  hali  kama   ya mgonjwa wa kichaa, akiwa na  nywele  na  ndevu  nyingi ambapo aliingia katikati  ya  uwanja  huku akipiga kelele.
 
Alisema   baadhi  ya waumini walidhani alikuwa  ni mtu mwenye matatizo  ya  akili,  lakini  waliendelea na  maombi  yao, ndipo mtu huyo alifika  katika eneo la mbele   la  maombi na kuanguka  chini .
 
“ Baada  ya  kuona  hali  hiyo  tuliendelea na maombi  mpaka hapo alipozinduka  na  kuanza kujishangaa  yeye mwenyewe. Wakati  huo hakuweza kuongea, hivyo  kuwafanya wanamaombi kuendelea  kumuombea",  alisema  Nabii  Joshua .
 
Alisema siku ya pili ya maombi  Abdul akiwa katika  uangalizi  wa kanisa  aliweza kujitambulisha, ndipo walipoamua kumpeleka nyumbani kwake na kubaini kuwa amefufuka. Imeandikwa na Lilian Lucas, Morogoro SOURCE: MWANANCHI

Friday, July 02, 2010

Serikali na mishangingi


Nina kumbukumbu kuwa waziri mkuu alionyesha uwezekano wa viongozi wa ngazi za juu serikalini kupunguza matumizi ya magari ya kifahari. Nazidi kujiuliza ni nani hasa anayeweza kutoa amri hiyo na watu wakatekeleza maana nimesikia tetesi kuwa yamenunuliwa tena. Hebu cheki mashangingi haya yaliyopigwa picha leo mchana na mpiga picha wa waziri mkuu yakiwa yameegeshwa kusubiri wakulu.
Hapo kwa jirani zetu kenya tunashuhudia gari aina ya Passat zikiwa tayari kwa kuwakabidhi viongozi wa ngazi za juu baada ya kurejesha yale ya kifahari. Inasemekana passat hizo zitaokoa zaidi ya nusu ya gharama za matumizi. Hivi hatuwezi kujifunza hata kwa mifano au tunaogopa kuiga? Na unajifunzaje bila kuiga? Hasa kwa mambo yenye faida?
Wadau mnaonaje siasa hizi au hadi tume iundwe kutafakari wazo ambalo kiongozi wa serikali ameliona! Nashindwa kupata jibu la nani anayeweza kufanya maamuzi haya! Karibuni! by ulimboka wa http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/42183-serikali-na-magari-ya-kifahari.html

Matata ya ufugaji




Kutokana na hali ya ukame unaosababishwa na upungufu wa mvua, wafugaji wamekuwa na hali duni ya kimaisha. Wafugaji hutegemea mvua na sehemu kubwa ya Tanzania haina vyanzo vya maji kama vile mito na maziwa ili kuweza kuota kwa malisho bora ya mifugo. Matokeo yake wafugaji mara nyingi huathirika kwa ukame kutokana na ukosefu wa mvua au upungufu, pichani wafugaji wanaonekana wakihangaika kuwaswaga mifugo wao kuelekea maeno yenye malisho katika moja ya picha zilizopigwa hivi karibuni.

Thursday, July 01, 2010

JK awatisha wagombea urais CCM




CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeandaa maandamano maalum kwa ajili ya kumsindikiza mgombea wake pekee wa urais kupitia chama hicho Jakaya Kikwete anayetarajia kurudisha fomu zake leo katika ofisi kuu chama hicho mjini hapa.

Katibu Mkuu wa Yusuf Makamba alisema jana kuwa anaamini Rais Kikwete atakuwa mgombea pekee wa urais katika chama hicho kwani hadi jana mchana hakukuwa na mtu mwingine aliyejitokeza.

“Niko ofisini kwa muda wote huo na sijamwona mtu mwingine, labda aje kesho (leo) asubuhi. Lakini hadi sasa Kikwete yuko pekee yake,” alisema Makamba.

Ikitokea amejitokeza mtu mwingine atatakiwa kuchukua, kuzijaza na kuzirudisha fomu hizo hapo hapo kwa kuwa muda utakuwa umekwisha, jambo ambalo ni gumu kwa sababu atakuwa hana muda wa kupata wadhamini 250 kutoka kila mkoa wa Tanzania.

Lakini Makamba alipotakia kueleza endapo CCM imeandaa sherehe zozote kwa ajili ya kusindikiza Kikwete alijibu “haya mengine mwulize Naibu Katibu Mkuu. Mimi siwezi kusema kwa kuwa ni mkurugenzi wa uchaguzi na bado nasubiri kama kuna wagombea wengine”.

Katibu wa Itikati na Uenezi wa CCM Kapteni John Chiligati aliweka bayana kuwa wanaCCM wameandaa sherehe na maandamano kwa ajili ya kumsindikiza Kikwete wakati anarudisha fomu hizo.

“Hawezi kurudisha fomu kimya kimya huyo ni mgombea wetu pekee. Shughuli zitaanza saa 4:00 na atasindikizwa hadi ofisini kwa katibu mkuu wa CCM ambako atarejesha fomu hizo,” alisema

Juni 21 mwaka huo Rais Jakaya Kikwete alichukua fomu za kuwania tena urais na kueleza kuwa serikali yake mpya itaongozwa na vipaumbele kadhaa vitavyosukumwa na misingi kumi.

Alitaja moja ya misingi hiyo kuwa ni kuongeza kasi ya mapambano ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka itakayoenda sambamba na kuimarisha utawala bora, utawala wa sheria, demokrasia na mapambano ya ubadhirifu wa mali za umma.

“Nitatumia bidii yangu yote kufanya kampeni ya kukipigania chama chetu kipate ushindi mkubwa na mara tutakapofanikiwa, vipaumbele vya serikali ijayo vitasukumwa na misingi kumi ifuatayo,” alisema Rais Kikwete.

“Kuhakikisha kwamba nchi inaendelea kuwa na umoja, amani na usalama, Kujenga msingi wa uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea kwa kuchukua hatua madhubuti za kuharakisha zaidi mapinduzi ya kilimo, ufugaji, uvuvi na viwanda.” SOURCE: MWANANCHI

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...