Sunday, July 04, 2010
Anayedaiwa kufa aibuka siku 40 baada ya kuzikwa
MAKAZI wa Msamvu mkoani Morogoro Khamisi Abdul (47), aliyedaiwa kufariki Juni 9 mwaka huu na kuzikwa katika Makaburi ya Kola mjini humo, ameibuka huku akiwa hai.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Bahati Abdul (24) ambaye ni mtoto wa Abdul alisema baba yake alifariki baada ya kujichoma na kisu tumboni na kwamba kabla ya mauti kumfika alipelekwa hospitalini na kulazwa.
"Baba alikuwa akijishughulisha na biashara ya kutembeza sabuni mtaani na alifariki Juni 9 baada ya kujichoma na kisu tumboni Mei 29 na ukweli hakuwa mgonjwa wa akili," alisema Bahati.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Abdul ambaye alikuwa amepoteza kumbukumbu alisema anachokumbuka ni kwamba alikuwa akilala katika pango lenye nyoka na wanyama wengi ambao hawakuweza kumdhuru.
“ Mara nyingine nilikuwa natembea porini na kukutana na wanyama wakali, lakini cha kushangaza, wao ndio walikuwa wakinikimbia,” alisema Abdul
Alipoulizwa kuhusu familia yake alisema anakumbuka alikuwa na watoto watatu kati yao mmoja ndio wa kumzaa mwenyewe, wengine wawili walikuwa watoto wa marehemu mkewe .
“Mtoto wangu wa kumza anaitwa Muka Khamis," alisema Abdul kwa shida .
Baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Sabasaba ambako Abdul alikuwa akifanya biashara walisema mara baada ta taarifa ya kifo cha Khamisi walitoa michango yao ya fedha.
Jalala Uwezo alisema alisema Khamisi alikufa mwezi Juni na walimzika katika makaburi ya Kola.
Tukio hilo lilivuta hisia za wengi mkoani humo, Nabii Joshua Aram wa Kanisa la Uponaji alimchukua mtu huyo na kwenda naye maeneo ambayo anadaiwa alikuwa akifanya biashara zake kabla ya kifo chake ili kuthibitisha hali hiyo.
Akiwa huko kundi la watu walimzunguka na kumshangaa huku wengine wakitokwa na machozi na kudai kuwa alishakufa na kwamba tangu alipofariki bado hazijatimia siku 40.
Akizungumzia kupatikana kwa Abdul, Nabii Joshua alisema wakiwa katika maombi yao ya kawaida kuombea wagonjwa nje ya uwanja katika eneo la Kihonda Viwandani, Abdul alitokea akiwa katika hali kama ya mgonjwa wa kichaa, akiwa na nywele na ndevu nyingi ambapo aliingia katikati ya uwanja huku akipiga kelele.
Alisema baadhi ya waumini walidhani alikuwa ni mtu mwenye matatizo ya akili, lakini waliendelea na maombi yao, ndipo mtu huyo alifika katika eneo la mbele la maombi na kuanguka chini .
“ Baada ya kuona hali hiyo tuliendelea na maombi mpaka hapo alipozinduka na kuanza kujishangaa yeye mwenyewe. Wakati huo hakuweza kuongea, hivyo kuwafanya wanamaombi kuendelea kumuombea", alisema Nabii Joshua .
Alisema siku ya pili ya maombi Abdul akiwa katika uangalizi wa kanisa aliweza kujitambulisha, ndipo walipoamua kumpeleka nyumbani kwake na kubaini kuwa amefufuka. Imeandikwa na Lilian Lucas, Morogoro SOURCE: MWANANCHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment