Thursday, July 29, 2010
Sitta aeleza alivyokamatwa na Takukuru
SIKU moja baada ya Takukuru mkoani Tabora kumnasa Waziri wa Maendeleo ya Jamiii Jinsia na Watoto Margaret Simwanza Sitta, jana aliibuka na kusema taasisi hiyo inawabambikia wananchi makosa ili waonekane wanafanya kazi.
Alisema kutokana na tukio lililompata juzi, sasa anawasiliana na wanasheria wake kuona achukue hatua gani dhidi ya maafisa wa Takukuru waliodai kumkamata kwa rushwa.
Waziri Sitta alisema kwamba juzi saa 7:30 usiku aliamshwa kwa mlio wa simu ya Catheri Sepetu iliyomwomba afike gesti ya Camise kuona mtoto mgonjwa. "Niliomba anielekeze gesti hiyo iko wapi ili niende kumwona huyo mgonjwa," alisema Mama Sitta.
Hata hivyo Magreti alidai kwamba kutokana kutoyafahamu maeneo hayo alimwomba katibu mwenenzi CCM manispaa Tabora wafuatane katika maeneo hayo aliyoambiwa na Sepetu.
Alisema alipofika karibu na njia ya kwenda katika gesti hiyo, wakatokea vijana zaidi ya sita na kusimamisha gari alipowahoji nyie ni nani ndipo walipotoa vitambulisho na kujitambulisha kwamba wao ni Takukuru na kwamba sasa yuko chini ya ulinzi.
Alisema walimchukua hadi ofisini kwao na kuanza kumpekua huku wakimwambia alikuwa akigawa rushwa kwa wajumbe.
"Nikahoji huyo ndiyo mgonjwa mliokuwa mnaniitia? Hawakumjibu badala yake waliendelea kunipekua mkoba wangu na mkoba wa mdogo wangu na kumwamrsisha katibu mwenezi Rashid Ramadhan akubali kwamba alikuwa akigawa fedha,"alisema Sitta.
"Katibu huyo alibaki anaduwaa kwani alichokuwa anajuwa ni kumsindikiza waziri kwa mgonjwa. Alishangaa kulazimishwa aandike maelezo kueleza kina nanni alikuwa anawagawia fedha. Akajibu siwezi kuandika wongo,"
Waziri Sitta aliendelea kueleza kuwa akiwa ofisini hapo, alimuuliza Sepetu kulikoni, naye alimjibu alilazimishwa kumpigia simu na baada ya kuwakatalia, walimpiga na kuchukua simu yake na kuanza kumpigia (Sitta) na ilipoita walimlazimisha aongee na waziri kwa maelekezo watakayompa.
"Niliwahoji iwapo mnafanya haya kwangu ambaye alau najua sheria kwa wale ambao hawajui inakuaje kama siyo kuwaonea wananchi na kupoteza fedha za serikali kuendesha kesi za kubambikiza."alieleza.
Waziri Sitta alisema iwapo viongozi wa Takukuru wataachwa kukemewa kuendelea na tabia hiyo, itakuwa vigumu kuelewa nani kabambikiwa kesi na nanni ana kesi halali. Habari ya Victor Kinambile. SOURCE:: MWANANCHI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment