Friday, July 02, 2010

Serikali na mishangingi


Nina kumbukumbu kuwa waziri mkuu alionyesha uwezekano wa viongozi wa ngazi za juu serikalini kupunguza matumizi ya magari ya kifahari. Nazidi kujiuliza ni nani hasa anayeweza kutoa amri hiyo na watu wakatekeleza maana nimesikia tetesi kuwa yamenunuliwa tena. Hebu cheki mashangingi haya yaliyopigwa picha leo mchana na mpiga picha wa waziri mkuu yakiwa yameegeshwa kusubiri wakulu.
Hapo kwa jirani zetu kenya tunashuhudia gari aina ya Passat zikiwa tayari kwa kuwakabidhi viongozi wa ngazi za juu baada ya kurejesha yale ya kifahari. Inasemekana passat hizo zitaokoa zaidi ya nusu ya gharama za matumizi. Hivi hatuwezi kujifunza hata kwa mifano au tunaogopa kuiga? Na unajifunzaje bila kuiga? Hasa kwa mambo yenye faida?
Wadau mnaonaje siasa hizi au hadi tume iundwe kutafakari wazo ambalo kiongozi wa serikali ameliona! Nashindwa kupata jibu la nani anayeweza kufanya maamuzi haya! Karibuni! by ulimboka wa http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/42183-serikali-na-magari-ya-kifahari.html

No comments: