Sunday, October 04, 2009

Miss Tanzania 2009





Mrembo toka Kanda ya Ziwa Miriam Gerald, akipungukia mkono mashabiki wake baada ya kutangazwa mshindi, huku akifuatiwa na mrembo wa nafasi ya pili kutokan Vyuo Vikuu,Beatrice Lukindo.








HATIMAYE taji la Vodacom Miss Tanzania 2009 limerudi tena jijini Mwanza, baada ya mrembo wa Kanda ya Ziwa Miriam Gerald alipoipuka mshindi wa taji hilo baada ya kuwabwaga warembo wenzake 28 ambao walikuwa wanagombea taji hilo.

Majaji tisa walimchagua Miriam kuwa Vodacom Miss Tanzania na ataiwakilisha Tanzania katika shindano la urembo la dunia, litakalofanyika baadaye mwaka huu. Nafasi ya pili ilitwaliwa na Beatrice Lukindo (Vyuo Vikuu) wakati mshindi wa tatu ni Julieth William na Sylvia Shally aliyeshika nafasi ya nne,wote wanaotoka Ilala.

Nafasi ya tano ilitwaliwa na Sia Ndasoki kutoka Temeke. Warembo hao jana walipewa zawadi zao katika Hoteli ya Giraffe na kuruhusiwa kurejea nyumbani.


Ukiacha hayo, Miriam pamoja na kupata tiketi ya urembo ya dunia, pia alizawadiwa Suzuki Grand Vitara lenye thamani ya shilingi milioni 53 na fedha taslimu shilingi milioni tisa pamoja na zawadi ya hereni na kidani cha dhahabu kutoka Tanzanite One na kutwaa taji la mrembo mwenye mvuto kwenye picha na kuzawadiwa Milioni moja..


Katika mashindano hayo, shoo nzima ya Miss Tanzania 2009 ilianza saa 4:45 usiku, ilifunguliwa na wasanii wa bongo fleva ambao ni Marlow, Alikiba, Hussein Machozi na Barnabas ambao waliimba wimbo wa pamoja uitwao Umoja Daima.


Baada ya hapo warembo 29 wanaowania taji hilo walipanda jukwaani kwa shoo yao ya ufunguzi ambayo waliimba nyimbo za Michael Jackson uitwao Human Neture na Bad ambayo walifundishwa na Sami Cool. Shoo ya ufunguzi ilikuwa kivutio cha aina yake.


Baada ya shoo hiyo, Wanne Stars alikamata jukwaa kabla ya warembo kurudi jukwaani wakiwa wamevalia vazi la ubunifu waliobuniwa na Ally Remtullah.


Saa 5:20usiku alirudi tema Barnabas na Pipi wakafuata Berry 9, Ally Kiba usinisemee na Marlow ambao waliwagoga mashabiki kwa nyimbo zao nzuri.


Saa 5:30usiku warembo walirudi tena wakiwa na vazi la ufukweni na 5.45usiku waliingia na vazi la usiku ambalo lilikuwa vazi la mwisho kabla ya kutajwa 10 bora wa Vodacom Miss Tanzania 2009. Habari ya Clara Alphonce.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...