Thursday, October 01, 2009

Michuano ya Netball







Wachezaji wa timu ya taifa ya Lesotho, wakikabiliana na wachezaji wa timu ya Namibia kwenye mechi ya kimataifa ya netiboli iliyofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo hii.Mechi hiyo ilisimama asubuhi kutokana na mvua iliyokuwa ikinyesha uwanjani hapo huku Lesotho wakiongoza kwa 17-15.

Katika michuano hiyo timu yetu ya Taifa ya Netbali, Taifa Queen, iliendelea kupokea kipigo baada ya kukubali kulala mbele ya majirani zao Uganda kwa mabao 42-30 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Taifa Queen licha ya kumtoa mfungaji Neema Emmanuel na kumuingiza Nyirabu Maximilian, lakini bado timu hiyo haikuweza kuimili mchezo huo.

Katika robo ya kwanza Taifa Queen ilikuwa 7-14 baada ya mapumziko timu ya Taifa Queen 19-24 na mpaka mchezo unakwisha Uganda waliibuka kidedea kwa bao 38- 24.

Mchezo wa pili uliikutanisha Afrika Kusini dhidi ya Malawi iliongoza kwa bao 50-32 katika robo ya kwanza Malawi ilikuwa mbele 12-8 mzunguko wa pili Malawi 26-14 kota ya tatu Malawi 37-21.

Kwa matokeo hayo inaifanya Taifa Queen kushika nafasi ya pili kutoka mwisho ilikiwa na pionti tatu baada ya kupoteza michezo yake mitatu na kushinda mmoja na kutoka droo mchezo mmoja.

Katika mchezo mwingine Malawi ilichakaza Zambia kwa mabao 63-39, robo ya kwanza Malawi walikuwa mbele 17-8, 36-18na 48-30. HAbari hii imendikwa na Jesca Nangawe na picha zote zimepigwa na Silvan Kiwale.

1 comment:

Anonymous said...

buy tramadol tramadol 80mg - tramadol hcl 93 58

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...