Monday, October 19, 2009

Meneja Uwanja Uhuru afariki dunia



"Nimesema mlango huu ufungwe, nataka watu watumie mlango ule...inakuwa vipi watu wanapitia mlango huu...nyie vipi bwana mnataka tuharibiane kazi...," ni kauli ya mara kwa mara ya Charles Celestine Masanja wakati wa mechi ama shughuli ya kitaifa kwenye Uwanja wa Taifa na sasa Uhuru.

Sasa kauli hiyo ya Masanja, Meneja wa Uwanja wa Uhuru sasa haitasikika tena.

Masanja alifariki saa 9 za usiku wa kuamkia jana wakati akitoka kwenye shughuli zake ikiwemo kusimamia mapato ya uwanja baada ya mechi kati ya Simba na Ruvu JKT juzi.

Katika mechi ile ambayo ni ya mwisho kwake, alikuwa akipambana na watu wa milangoni waliokuwa wakiingiza watu na fedha kuingia mifuko mwao.

Wengi watamkumbuka kuwa si meneja wa kukaa ofisini, alikuwa akihaha huku na huko kuhakikisha usalama unakuwepo uwanjani wakati wote.

Taarifa zilizopatikana jana nyumbani kwake, Kimara Korogwe, zilisema kuwa Masanja amefariki katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikopelekwa baada ya kuteleza na kuanguka nje ya uzio wa nyumba yake.

Mdogo wa marehemu, Greyson Selestine aliliambia Mwananchi kuwa kaka yake alipatwa na mkasa huo wakati akirejea nyumbani majira ya saa 9 za usiku akitokea katika shughuli zake za kawaida ambapo pia jioni ya siku hiyo alishihudia mpambano wa ligi kuu kati ya Simba na Timu ya JKT Ruvu uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru. Habari iemdaliwa na
Sosthenes Nyoni na Sweetbert Lukonge

1 comment:

Anonymous said...

I've read this sad news in today's media,kwakweli ni pigo kwa wadau wote wa michezo hapa nchini.
MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi..Amein

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...