Tuesday, May 19, 2009

Wanajeshi wamtwanga Trafiki

Picha ya Silvan Kiwale.

ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), leo asubuhi wamemshambulia na kumpiga askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Sajenti Thomas Mayapila, wakidai aliwachelewesha kupita eneo la Ubungo.

Tukio hilo lilitokea asubuhi wakati Thomas akiwa kazini kuongoza magari katika makutano ya Barabara ya Morogoro, Sam Nujoma na Mandela, Ubungo, eneo ambalo kwa kawaida huwa na misururu mirefu ya magari nyakati za asubuhi na jioni.

Tukio hilo lilitokea saa 1:35 asubuhi wakati trafiki huyo akiendelea na kazi yake ya kuongoza magari katika eneo hilo, akionekana kutofahamu kuwa kulikuwa na magari matatu ya JWTZ yaliyokuwa yakitokea Barabara ya Sam Nujoma na kuelekea Buguruni. habari zaidi soma Mwananchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...