Wednesday, May 27, 2009

Kenya, Uganda hatarini kuzichapa

BUNGE nchini hapa limempa baraka Rais Mwai Kibaki kuchukua hatua za kijeshi iwapo juhudi za kidiplomasia zinazoendelea katika mvutano kuhusu umiliki wa kisiwa cha Migingo katika Ziwa Victoria zitashindikana.

Bunge hilo pia limemruhusu Rais Kibaki kuomba msaada wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo mvutano huo utaonekana kutishia usalama wa kanda ya Afrika Mashariki.

Katika hoja hiyo iliyopitishwa na Bunge, wabunge walimtaka Kibaki ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu kutumia mamlaka yake na kufanya kila linalowezekana kulinda ardhi ya Kenya.

Hoja hiyo ambayo juzi ilikosa nguvu baada ya baadhi ya mawaziri kujaribu kuipinga, jana iliweza kupitishwa baada ya serikali kukosa idadi ya kura za kutosha kuipinga.

Wabunge hao walionyesha hisia za wazi wakati wa kujadili suala hilo, wakieleza umuhimu wa kuingia vitani iwapo itabidi, huku wakimtaka Rais Kibaki kuchukua mamlaka kuhusu mipaka ya nchi.

Juhudi za Waziri wa Mambo ya Nje, Moses Wetangula na Waziri wa Habari, Samuel Poghisio kujaribu kupinga hoja hiyo na kujaribu kutafuta upatanishi zaidi zilishindikana. Source: Daily Nation

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...