Sunday, May 31, 2009

Majenerali Waitara na Sayore ndani ya golf






Majenerali hawa wawili George Mwita Waitara na mtangulizi wake Gideon Waitara ni miongoni mwa wachezaji wa golf waliokuwapo katika michuano ya Golf ambapo zaidi ya 120 toka vilabu mbalimbali vya mchezo huo nchini, wanashiriki katika mashindano ya wazi ya Lugalo yanayotarajia kufanyika mwishoni mwa wiki hii.

Wachezaji hao wa ridhaa na wale wa kulipwa, wanatoka katika vilabu vikubwa vya mchezo huo vilivyopo Mufindi mkoani Iringa, TPC Moshi, Gymkhana Morogoro, Dar es salaam pamoja na wenyeji JWTZ Lugalo.

Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dr Husein Mwinyi ndie aliyefungua rasmi michuano hiyo, kwa mujibu wa katibu mkuu wa klabu ya golf ya Lugalo JWTZ John Nyalusi

Mashindano hayo yanadhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya zaid kwa kitita cha shilingi milioni saba, ambapo meneja masoko wa zain Costantine Magavila, amesema msisimko wa mashindano hayo ndio umewasukuma kujitosa katika kuyadhamini

Mashindano ya golf ya wazi ya Lugalo, ni miongoni mwa mashindano makubwa ya mchezo huo yanayotambuliwa na chama cha mchezo wa golf cha taifa TGU.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...