Wednesday, May 13, 2009

Hivi Rais Karume kwanini haudhurii vikao baraza la mawaziri


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha baraza la mawaziri ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi, hakika hiki ndicho chombo kikubwa kabisa humu nchini mwetu lakini cha kushangaza hebu angalia vizuri hiyo picha utaona kiti cha Rais wa Zanzibar Abeid mana Karume hakina mtu , mwenyewe hayupo sababu hatujui, na hatukuelezwa hivyo tunajiuliza hivi kwanini Rais Karume haudhurii vikao vya baraza la mawaziri??? maswali mengi yanaibuka kwetu (picha ni ya Freddy Maro)

2 comments:

Mzanzibar 100% said...

Mbona unauliza swali la lisilo na mantiki yoyote??? Hivi unajuwa unachouliza kweli??? Umeshasema RAIS wa Zanzibar sasa ahudhurie baradha la mawaziri ili iweje??? Mbona huulizi kwanini Rais wa Kenya hakuja kuhudhuria hicho kikao cha baraza la mawaziri wa Tanganyika??? Hivi upo timamu??? Hem subiri kikao cha baraza la mawaziri wa zanzibar kikifunguliwa, then ukiona Rais wa zanzibar hajaingia kufunguwa kikao cha baraza lake ndo uulize swali lako, hapo utakuwa unauliza swali lenye mantiki! Kwa taarifa yako tu Zanzibar ni NCHI na TAIFA huru kama ilivyo kenya, uganda n.k. Kama ulizani Rais wa zanzibar ana hadhi ya uwaziri wa Tanganyika hapo umeingia choo cha kike...! Habari ndo hiyooooooooo!

Anonymous said...

Wewe mzanzibari usimsakame huyo mwenye blogu jibu swali la msingi kwanza, huyo anajua anachokisema, Karume ni waziri tu kama wengine sababu Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, kama una upeo wa kutosha ungeangalia hiyo picha uone hilo jina lililopo kwenye hicho kiti kilichopo wazi ni la nani, kisha ujifunze namna ya kuargue.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...