Sunday, May 31, 2009

Meli yapinduka Zanzibar, watatu wafariki dunia



 
MELI ya mizigo ya inayomilikiwa na Kampuni ya Seagul, Mv Fatih imepinduka na kuzama katika Bandari ya Malindi Zanzibar usiku wa kuamkia jana na maiti za abiria watano zimepatikana huku juhudi za ukoaji zikiendelea.

Meli hiyo inayodaiwa kuwa na watu 27 na mizigo yenye uzito wa tani 76 ilipinduka na kuzama ikiwa tayari imekaribia kutia nanga katika Bandari ya Malindi mjini Zanzibar ikitokea Dar es Salaam.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Bakari Khatib Shaaban amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo ambapo alisema ilipinduka saa 4.00 juzi usiku katika bandari ya Malindi na abiria waliokuwemo walikuwa wanataka kushuka lakini ghafla ilipinduka na kuzama baharini.
 
Kamanda Shaaban alisema hadi jana mchana ni maiti tatu tu ndizo zilizoonekana ikiwamo ya mtoto mdogo wa kiume, na mwanamke na mwanaume ambao hawakuweza kufahamika majina yao kamili.
 
Waliookolewa katika ajali hiyo ni Machano Mkinai Mkaazi wa Mkwajuni na Kitiba Mussa Kitiba, Gamba Mkoa wa Kaskazini 'A' Unguja, Halima Mussa wa Arusha, Hassan Omar, Maulid Abdallah, wote wa Kisiju Mkoa wa Pwani.
Salma Said, Zanzibar soma kinagaubaga taarifa hapa
upate habari hizi kwa kina pia tutakuwa tukikuletea taarifa zinazoendelea kutokea visiwani humo

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...