Thursday, October 30, 2008
balaa la mvua
jamani hii ni hali livyokuwa ikionekana juzi baada ya kunyesha mvua jijini Dar es Salaam, ambapo katika eneo hilo la mto kizinga maji yalivunja daraja na watu wa huku kusafiri kwa shida kubwa wengi walikuwa wakibebwa na wengine kujitahidi kuogelea maji mafupi. Picha ya mdau Venance Nestory wa Mwananchi.
Wednesday, October 29, 2008
wazee afrika mashariki
VIGOGO wa serikali, mafisadi wenye mihele yao ya kufuru, mabalozi na wananchi wa kawaida jana walionjeshwa ukubwa wa machungu wanayopata wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakati wazee hao walipoweka kizuizi katika eneo la daraja la Sarenda na kusababisha magari kushindwa kuingia katikati ya jiji.
Eneo hilo, - makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa, ambako kuna kituo cha polisi cha Sarenda, ndilo njia kuu na pekee ya magari yote kutoka maeneo ya Oysterbay, Mikocheni, Msasani na Ada, ambako wanaishi viongozi na watendaji wakuu wa serikali, mabalozi na maofisa wengine wa taasisi za kimataifa.
Maeneo ya Kinondoni, Mwenge, Kawe, Tegeta na Mbezi ambako wanaishi wananchi wa kipato cha chini na kati, pia waliathirika na mbinu hiyo ya wastaafu wa EAC kuishinikiza serikali kuwalipa mafao yao baada ya jumuiya hiyo kuvunjika mwaka 1977.
Monday, October 27, 2008
World's heaviest man marries in Mexico
Mexico – The world's heaviest man has tied the knot. Manuel Uribe, who hasn't left his bed in six years, married his longtime girlfriend Claudia Solis Sunday in northern Mexico.
Wearing a white silk shirt with a sheet wrapped around his legs, Uribe smiled as Solis, 38, walked down a flight of stairs wearing a strapless ivory dress, a tiara and hot-pink lipstick.
He later broke into tears as a notary declared the couple husband and wife in a civil ceremony attended by more than 400 guests. For the traditional first dance as newlyweds, Uribe and Solis held hands and swayed to a romantic ballad.
A popular local norteno band played accordion-heavy tunes at the reception, which featured a banquet of meat and buttered vegetables.
Uribe's mother, Orquedia Garza, said the groom steered clear of the five-tier wedding cake.
"He didn't break his diet," she told The Associated Press. "His doctors are here and they are watching him very closely."

here comes swahili fashion week
moto mkali balaaa
Odemba ang'ara Miss Earth 2008
Sunday, October 26, 2008
Ali Choki atoka kivyake
Pamoja na unene alionao, Aisha Madinda bado anakandamiza misosi kwa kwenda mbele. Kamera yetu ilimnasa jana akikandamiza chips nyama choma alizoagiza nje ya hoteli hiyo kukwepa gharama. Aliyenaye ni mtoto wa kaka'ke.
Meneja wa bendi ya muziki wa dansi ya T-Respect, Ali Choki (wapili kutoka kulia) akiwa katika harakati za kurekodi picha za Video ya wimbo wake “Mfano kwa vijana” pamoja na wanenguaji maarufu kutoka bendi mbalimbali akiwemo Aisha Madina (Kulia) kutoka Afican Stars Twanga Pepeta. Hii ilikuwa ni jana ndani ya viunga vya Hotel ya kisasa ya Atriums Sinza Africa Sana Jijini Dar es Salaam. Kwa niaba ya Global Publishers.
Friday, October 24, 2008
Shirikisho Afrika
UAMUZI wa wakuu wa nchi 26 za Afrika kuunganisha soko la pamoja katika nchi hizo, umeondoa ndoto ya kuanzisha shirikisho la kisiasa la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hatua hiyo inatokana na mpango wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Soko la Pamoja kwa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (Comesa), kuanzisha mchakato huo ambao utameza mambo ya jumuiya hizo.
Shirikisho la Afrika Mashariki linahusisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi na Rwanda na tayari nchi hizo zilishapiga hatua kubwa kuelekea kuwa kitu kimoja, huku mabilioni ya fedha yakiwa yametumika katika mchakato huo, ambao pia ulihusisha kutafuta maoni kwa wananchi.
Baadhi ya taasisi za Shirikisho la Afrika Mashariki zilishaanza kufanya kazi, ikiwemo sekretarieti inayoratibu shughuli zote za shirikisho hilo, bunge, mahakama huku mamilioni mengine yakitumika kujenga ofisi za makao makuu mjini Arusha, lakini uamuzi uliofanywa juzi unaweza kuwa mwanzo za kuzorota kwa harakati hizo.
Akijibu swali kutoka gazeti hili kuhusu uamuzi huo wakuu wa nchi 26 uliofanywa nchini Uganda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe alisema ni dhahiri hapo baadaye kama mchakato utakwenda kama ulivyo, shirikisho hilo halitakuwepo.
Vigogo wa harakati za albino
Mwenyekiti wa Good Hope Star Foundation,Al-Shaymaa Kwegyir, akitoa taarifa ya asasi hiyo kabla ya kuzinduliwa rasmi na Rais Jakaya Kikwete
Mwanaharakati na mfanyabiashara mwenye ulemavu wa ngozi (albino) kutoka Canada, Peter Ash, ameiomba serikali kuingiza katika mitaala ya shule za msingi na sekondari elimu kuhusu albino ili kusaidia kupunguza mauaji yanayoendelea nchini.
Akizungumza katika mkutano wake na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Ali Iddi, Dar es Salaam jana, Ash aliyewasili nchini juzi na ujumbe wa watu watatu, alisema kinachoisumbua jamii ni uelewa mdogo kuhusu albino ni watu gani.
Alisema wameridhika na juhudi za Serikali ya Tanzania katika mapambano, zinazoongozwa na Rais Jakaya Kikwete na hatua zilizotangazwa kuwa zitachukuliwa kwa watakaobainika, lakini bado elimu kuanzia ngazi za shule za misingi inahitajika kwa manufaa ya kizazi kijacho.
“Kinachoonekana kwa mataifa mengi ni elimu duni kuhusu sisi tunatokeaje, wengi hawaelewi kwamba tu binadamu wa kawaida, tofauti yetu ni ngozi inayotokana na ukosefu wa vinasaba vya aina fulani katika miili yetu, hili linahitajika kufundishwa kwa mapana zaidi,” alisisitiza Ash.
Ash, ambaye anatarajia kwenda Mwanza kukutana na familia zilizoathirika kwa mauaji hayo, alisema binafsi kama mwanaharakati wa kupinga mauaji hayo ya kinyama, ataendelea kushirikiana kwa karibu na serikali, lakini pia pamoja na asasi za kijamii zinazoonyesha wazi kupambana na mauaji hayo.
Aliiomba serikali kutoa ulinzi imara kwa familia zenye albino na jamii kushiriki kuwafichua wauaji ili hatua zilizotajwa na Rais Kikwete zichukuliwe. Kwa mujibu wa Ash, ambaye pia ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa asasi ya kijamii ya Under the Same Sun inayohusika na haki za watu wenye ulemavu hususani albino nchini Canada, duniani wapo albino zaidi ya 5,000 na wengi wao wapo katika nchi za Kiafrika, Tanzania ikiwamo.
Kwa upande wake, Naibu Waziri, Balozi Iddi alimhakikishia Ash kuwa serikali itahakikisha usalama kwa albino na itachukua hatua kali dhidi ya watakaobainika kuhusika katika mauaji hayo.
Msafara wa rais
Wednesday, October 22, 2008
masikini Chipps
rais wa miss tourism world organisation john singh (kati) akipeana mikono na mh. aloyscious gonzaga mandago huku isaack kassanga akionesha mkataba ambao kampuni ya easy finance ambayo wao ni wakurugenzi imeingia na hiyo taasisi inayoendesha mashindano ya urembo ya utalii duniani. sherehe hii ilifanyika katika ofisi za easy finance iliyoko kinondoni, dar.
kwa mujibu wa makubaliano hayo, easy finance, ambayo pia ni mmoja wa wafadhili wakuu wa globu hii ya jamii, sasa itakuwa msimamizi wa mashindano ya miss tourism kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia januari 2009.
pia itasimamia na kuendesha, kupitia taasisi ingine ya nyumbani, mashindano ya miss tourism ya bongo. hal kadhalika itaandaa fainali za dunia za mashindano hapa bongo mwakani ambapo zaidi ya nchi 70 zitashiriki.
hii ina maana kwamba taasisi iliyokuwa ikiongozwa na gideon chipungahelo kwa miaka sita iliyopita haitohusika tena na uandaaji wa miss tourism hapa nyumbani.
habari zinasema taasisi mpya itayochukua nafasi ya ile ya chipungahelo imeshaanzishwa na easy finance na mambo yakienda mswano miss tanzania 1994 wa pili lucy ngongoseke kihwele ndiye atakayekuwa anaiongoza.

Jk akiwa kampala
Akihutubia mkutano wa wakuu wa mataifa takribani 16 ya Afrika ambapo amependekeza kuunganishwa kwa SADC, COMESSA na EAC
Rais Jakaya Kikwete akipokea maua kutaka kwa binti Abigairi Murungimara tu baada ya kuwasili kenye uwanja wa ndege entebe hukouganda,aliyesimama kulia ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi wauganda, mheshimiwa omara atubo PICHA NA JOHN LUKUWI WA MAELEZO Akibadilishana mawazo na Kibaki

Tuesday, October 21, 2008
Rais Khama awasili nchini
Rais Jakaya Kikwete Akimtambulisha Rais Seretse Khama Ian Khama kwa baadhi ya Mawaziri wa ke mara tu ya kuwasili Uwanjani hapo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini
Rais Seretse Khama Ian Khama Wa Botswana akipokea maua kutoka kwa Mtoto Sara Elias mara tu ya kuwasili kwenye Uwanja Wa Kimataifa Wa Kilimajaro Huku Pembe Akiwa na Mwenyeji Wake Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete Akimkaribisha Rais Seretse Khama Ian Khama Wa Botswana Alipowasili Punde baada ya kuwasili kwenye Uwanja Wa Ndege Cha Kimataifa Wa Kilimanjaro (KIA) kwa ziara ya kikazi ya siku Mbili nchini
Monday, October 20, 2008
Media Bonanza
Sunday, October 19, 2008
Obama aweka rekodi, akusanya dola 605 milioni za kampeni
Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Seneta Barack Obama akizungumza katika kampeni za urais huko St. Louis, jana. Picha na Reuters.
MGOMBEA wa Urais nchini Marekani, kwa tiketi ya chama cha Demokratic Barak Obama, amevunja rekodi kwa kukusanya dola za Marekani 150 milioni karibu paund 86 milioni katika kipindi cha mwezi Septemba.
Kiasi hicho kilichokusanywa na Obama kwa mwezi Septemba kinafanya jumla ya dola 605 milioni kukusanywa na mgombea huyo tangu kuanza kwa kampeni za kuchangia pesa za uchaguzi. Obama amekuwa mgombea wa kwanza kutochukua fedha za umma tangu mwaka 1970.
Wakati Obama akiwa amekusanya kiasi hicho, McCain ameacha kukusanya fedha kwa ajili kuzitumia kwenye uchaguzi huo, huku Obama kuanzia Agosti, mwaka huu, amekuwa akiwavutia wafadhili wapya na kuchangisha fedha zaidi.
Meneja kapteni wa Obama katika nyakati walisema kuwa hadi kufikia mwezi Septemba, mwaka huu, walikuwa na wafadhili wapya 632,000 na kufanya jumla ya wafadhili wa Obama kufikia zaidi ya milioni 3.1.
Meneja kampeni wa Obama, David Plouffe alisema, wastani wa wafadhili, wamekuwa wakijitokeza kupitia mtandao wa mgombea huyo na kwamba kiasi cha fedha zilizopokelewa na timu ya mgombea huyo, zimesadia chama hicho kufungua ofisi zaidi kwenye majimbo muhimu ya uchaguzi kuliko
Chama cha Republican na kununua zaidi muda wa hewani wa matangazo katika vutuo vya Televisheni.
Plouffe alisema Democrat kimeweza kununua dakika 30 kwa ajili ya matangazo kwa ajili ya Obama kutetea hoja zake wiki moja kabla ya wananchi wa Marekani kupiga kura Novemba 4, mwaka huu.
Zikiwa zimebaki siku 16 kabla ya wananchi wa Marekani hawajapiga kura Obama amekuwa akiongoza katika kura za maoni.
Thursday, October 16, 2008
Money in ZIMBABWE
500 million dollar bill, just printed in May 2008.....everybody can have it.... just
enough for breakfast/lunch (equal to about USD 2)
Everybody is a billionaire....
To buy tidbits in a plastic packet......you have to spend at least 10 million
To buy vegetables.....5 million
To buy eggs........6000 million
To buy chicken........how many million?
If you want to eat in a restaurant, please prepare the money.........
For a beer after office hours
Your monthly salary.........you need to hire a taxi or lorry to bring the money
home.....
Young kid - already a millionaire.......
If you don't want to carry a lot of money.....change it to USD
Nobody wants to count the money, just weigh it......
Otherwise, this is what you have to do every time you go to shop, market, bus
station etc.....
Wednesday, October 15, 2008
Mgomo wa walimu
Mmoja wa walimu akilia wakati wa makutano waaalimu katika ukumbi wa Diamond Jublee Dar es Salaam jana wakati wa makutano wa maamdalizi ya mgomo wa waalimu kwa nchi nzima uliokuwa uanze leo na kupigwa marufuku na Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi jana. Picha na Emmanuel Herman
Walimu waliojawa na jazba wakiwashutumu viongozi wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT), kwa kutaganza kusitishwa na mgomo kutokana na amri ya Mahakama.
Tuesday, October 14, 2008
Mwisho wa kumtaja Mkuchika leo
LEO itakuwa mwisho kwa jina la Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Kapteni George Mkuchika, kutajwa katika vyombo vya habari baada ya Wahariri kuamua kutoandika au kutangaza habari zake katika vyombo vya habari.
Wahariri wa vyombo vya habari nchini, wameamua kwa pamoja kususia kuandika habari zote zinazomuhusu waziri huyo kupinga hatua yake ya kulifungia gazeti la MwanaHalisi kutochapishwa kwa miezi mitatu..
Kauli hiyo ya pamoja, ilitolewa jana na Jukwaa la Wahariri nchini, katika mkutano wao uliofanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam na kutoa maamuzi yao juu ya kufungiwa kwa gazeti hilo bila ya kupewa muda wa kutosha kujitetea kuhusiana na walichokiandika.
Pamoja na uamuzi wa kutoandika habari za waziri huyo, pia wahariri hao wameamua, kufungua kesi ya kupinga kufungiwa kwa gazeti hilo, na kufanya maandamano siku ya Ijumaa kwa lengo la kuelezea kero zao na kuziandikia barua nchi wafadhili kuelezea jinsi Tanzania inavyoanza kuingilia uhuru wa vyombo vya habari.
Na Festo Polea

Nyerere Day
Monday, October 13, 2008
Serikali yalifungia Mwanahalisi
SERIKALI imelifungia gazeti la Mwanahalisi linalochapishwa na Kampuni ya Hali Halisi Publisher, kwa kwa madai ya kuandika habari za uchochezi.
Uamuzi huo ulitangazwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Kapteni George Mkuchika akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Kwa mujibu wa Waziri Mkuchika, serikali imeamua kulifungia gazeti hilo kwa muda wa miezi mitatu kutokana na wamiliki pamoja na mhariri wake kukataa kubadili mtindo wa kuandika habari za serikali na viongozi wakuu.
Alisema Gazeti hilo limekuwa likiandika habari za uchochezi mara kwa mara bila kujali maadili ya kazi yake na kudai kuwa ofisi yake imekuwa ikilionya mara kwa mara bila ya mafanikio.
“Ofisi yangu imeshamwita Mkurugenzi wa Kampuni ya Hali halisi na kumuonya zaidi ya mara tatu lakini hakuna mabadiliko yoyote kutoka katika gazeti hilo," alisema Mkuchika.
Waziri Mkuchika alisema uamuzi huo unafuatia gazeti hilo katika toleo lake namba 118 la Oktoba 8, 2008 kuandia habari yenye kichwa, “Njama za kung’oa Kikwete zafichuka-Mwanaye Ridhwani atumika –Watuhumiwa Ufisadi wajipanga” makala ambayo Mkuchika alidai kuwa inavunja sheria ya magazeti ya mwaka 1976 kifungu cha (31) (1), kifungu kidogo (d) na (e) na kifungu cha (32) (1) kifungu kidogo (c).imeandikwa na Geofrey Nyang'oro na Festo Polea

Subscribe to:
Posts (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...