Wednesday, October 29, 2008
wazee afrika mashariki
VIGOGO wa serikali, mafisadi wenye mihele yao ya kufuru, mabalozi na wananchi wa kawaida jana walionjeshwa ukubwa wa machungu wanayopata wastaafu wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wakati wazee hao walipoweka kizuizi katika eneo la daraja la Sarenda na kusababisha magari kushindwa kuingia katikati ya jiji.
Eneo hilo, - makutano ya Barabara ya Ali Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa, ambako kuna kituo cha polisi cha Sarenda, ndilo njia kuu na pekee ya magari yote kutoka maeneo ya Oysterbay, Mikocheni, Msasani na Ada, ambako wanaishi viongozi na watendaji wakuu wa serikali, mabalozi na maofisa wengine wa taasisi za kimataifa.
Maeneo ya Kinondoni, Mwenge, Kawe, Tegeta na Mbezi ambako wanaishi wananchi wa kipato cha chini na kati, pia waliathirika na mbinu hiyo ya wastaafu wa EAC kuishinikiza serikali kuwalipa mafao yao baada ya jumuiya hiyo kuvunjika mwaka 1977.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment