Sunday, October 19, 2008

Obama aweka rekodi, akusanya dola 605 milioni za kampeni


Mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic, Seneta Barack Obama akizungumza katika kampeni za urais huko St. Louis, jana. Picha na Reuters.

MGOMBEA wa Urais nchini Marekani, kwa tiketi ya chama cha Demokratic Barak Obama, amevunja rekodi kwa kukusanya dola za Marekani 150 milioni karibu paund 86 milioni katika kipindi cha mwezi Septemba.
Kiasi hicho kilichokusanywa na Obama kwa mwezi Septemba kinafanya jumla ya dola 605 milioni kukusanywa na mgombea huyo tangu kuanza kwa kampeni za kuchangia pesa za uchaguzi. Obama amekuwa mgombea wa kwanza kutochukua fedha za umma tangu mwaka 1970.
Wakati Obama akiwa amekusanya kiasi hicho, McCain ameacha kukusanya fedha kwa ajili kuzitumia kwenye uchaguzi huo, huku Obama kuanzia Agosti, mwaka huu, amekuwa akiwavutia wafadhili wapya na kuchangisha fedha zaidi.

Meneja kapteni wa Obama katika nyakati walisema kuwa hadi kufikia mwezi Septemba, mwaka huu, walikuwa na wafadhili wapya 632,000 na kufanya jumla ya wafadhili wa Obama kufikia zaidi ya milioni 3.1.
Meneja kampeni wa Obama, David Plouffe alisema, wastani wa wafadhili, wamekuwa wakijitokeza kupitia mtandao wa mgombea huyo na kwamba kiasi cha fedha zilizopokelewa na timu ya mgombea huyo, zimesadia chama hicho kufungua ofisi zaidi kwenye majimbo muhimu ya uchaguzi kuliko
Chama cha Republican na kununua zaidi muda wa hewani wa matangazo katika vutuo vya Televisheni.

Plouffe alisema Democrat kimeweza kununua dakika 30 kwa ajili ya matangazo kwa ajili ya Obama kutetea hoja zake wiki moja kabla ya wananchi wa Marekani kupiga kura Novemba 4, mwaka huu.

Zikiwa zimebaki siku 16 kabla ya wananchi wa Marekani hawajapiga kura Obama amekuwa akiongoza katika kura za maoni.

2 comments:

Anonymous said...

Ametoa wapi fedha kaka. follow the money then you will who really is helping him, and if so why are they doing that. Check www.vilagrablas.blogspot.com

Anonymous said...

Angalia vilevile,
http://www.haaretz.com/hasen/spages/1029302.html

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...