Wednesday, October 22, 2008

masikini Chipps

rais wa miss tourism world organisation john singh (kati) akipeana mikono na mh. aloyscious gonzaga mandago huku isaack kassanga akionesha mkataba ambao kampuni ya easy finance ambayo wao ni wakurugenzi imeingia na hiyo taasisi inayoendesha mashindano ya urembo ya utalii duniani. sherehe hii ilifanyika katika ofisi za easy finance iliyoko kinondoni, dar.
kwa mujibu wa makubaliano hayo, easy finance, ambayo pia ni mmoja wa wafadhili wakuu wa globu hii ya jamii, sasa itakuwa msimamizi wa mashindano ya miss tourism kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia januari 2009.
pia itasimamia na kuendesha, kupitia taasisi ingine ya nyumbani, mashindano ya miss tourism ya bongo. hal kadhalika itaandaa fainali za dunia za mashindano hapa bongo mwakani ambapo zaidi ya nchi 70 zitashiriki.
hii ina maana kwamba taasisi iliyokuwa ikiongozwa na gideon chipungahelo kwa miaka sita iliyopita haitohusika tena na uandaaji wa miss tourism hapa nyumbani.
habari zinasema taasisi mpya itayochukua nafasi ya ile ya chipungahelo imeshaanzishwa na easy finance na mambo yakienda mswano miss tanzania 1994 wa pili lucy ngongoseke kihwele ndiye atakayekuwa anaiongoza.


1 comment:

Anonymous said...

Huyo Tapeli number moja Tanzania Gonzaga hajafa tu!

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...