Tuesday, October 07, 2008

Happy Birthday Mheshimiwa Rais


Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo (Jumanne, Oktoba 7, 2008) ameadhimisha Siku yake ya kuzaliwa kwa kuhudhuria hafla fupi ya kushtukiziwa aliyoandaliwa na wafanyakazi wenzake wa Ikulu, Dar es Salaam.

Rais Kikwete amefikisha umri wa miaka 58 leo. Alizaliwa Oktoba 7, 1950 katika kijiji cha Msoga, Chalinze, Bagamoyo, Mkoa wa Pwani.

Katika halfa hiyo kwenye makazi yake rasmi, Rais Kikwete amepata nafasi ya kumsalimia binafsi kila mmoja wa wafanyakazi hao baada ya kuwa ameshiriki nao katika kuonja keki ya Siku hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi hao katika halfa hiyo fupi, Katibu Mkuu wa Ikulu, Michael Mwanda amempongeza Rais Kikwete kwa kufikisha umri wa miaka 58 na kumtakia afya njema na maisha marefu.

Naye Rais amewashukuru wafanyakazi hao akisema kuwa utawala wake usingepata mafanikio yaliyopatikana bila kazi kubwa inayofanywa na wafanyakazi hao.

“Nawashukuruni sana kwa kunisaidia kwa kiasi kikubwa. Nawashukuruni pia kwa kuniandalia hafla hii fupi ya kushtukizia kwa sababu kama unavyojua sisi watu tuliozaliwa vijijini hatuna utamaduni wa namna hii wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa ama kulishana keki.”

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

07 Oktoba, 2008

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...