Saturday, October 10, 2015

MAMA SAMIA AFUNIKA ILEMELA NA NYAMAGANA MKOANI MWANZA

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Oktoba 9, 2015 katika Viwanja vya Nyabogoya, eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.
 Wananchi wakimshangilia Mama Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia maelfu ya wananchi hao waliofurika
kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Oktoba 9, 2015 katika Viwanja vya Nyabogoya,
eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.
 Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM, Kitaifa, Christopher Ole Sendeka, katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika  Oktoba 9, 2015 katika Viwanja vya Nyabogoya, eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Maarufu wa jina la Msukuma, akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Mama Samia Suluhu Hassan Oktoba 9, 2015 katika Viwanja vya Nyabogoya,
eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.
 Kada wa CCM, Paul Makonda akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika Oktoba 9, 2015 katika Viwanja vya Nyabogoya,
eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.
 Kijana akiwa na Kufuli, kumpamba Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, katika mkutano wa kampeni Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika Oktoba 9, 2015 katika Viwanja vya Nyabogoya,
eneo la Bitimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana ambaye ni Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza Baraka Konisaga, akihutubia mkutano wa kampeni wa Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika  katika Viwanja vya Nyabogoya,
eneo la Butimba, Jimbo la Nyamagana, mkoani Mwanza. Konisaga amewataka wananchi wa mkoa wa Mwanza kutokuwa na hofu wakati wa kampeni zinazoendelea na wakati wa uchaguzi, kwa kuwa serikali katika mkoa huo imejiandaa kuhakikisha shughuli hizo zinafanyika na kumalizika kwa amani na utulivu.
 Baadhi ya viongozi wa CCM, wakiwa meza kuu wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza
 Wananchi wakimshangilia Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan aliphutubia mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza
 Wananchi wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati ya Kampeni za CCM Kitaifa, Chrisopher Ole Sendeka alipohutubia mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Ilemela  mkoani Mwanza
 Mwananchi akiwa kwenye kilele cha  jiwe, ili kumuona mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika  katikajimbo la Ilemela mkoani Mwanza
 Baadhi ya wanachi wakiwa kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika  katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofayika katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza
 Bango la Mgombea Ubunge jimbo la Ilemela, Angeline Mabula
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akisistiza jambo wakati akihutubia mktano wa kampeni uliofanyika katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza
 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge jimbo la Ilemela Angeline Mabula, katika mkutano wa kampeni uliofanyika  katika jimbo hilo.
 Vijana wakiwa kwenye pikipiki zao wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika leo katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza
 Mwenyekiti wa CCM, mkoa wa Mwanza maarufu kwa jina la Msukuma, akiwa na Kada wa CCM, Paul Makonda na Christopher Ole Sendeka wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika  Oktoba 9, 2015 katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.
PICHA ZOTE NABASHIR NKOROMO

No comments:

RAIS SAMIA APONGEZWA KUWEZESHA UJENZI OFISI KUU WMA

  ✅ Katibu Mkuu Viwanda na Biashara amshukuru Rais kutumia vyema fedha za Watanzania ✅Akagua ujenzi Jengo la WMA na kukiri kuridhishwa ✅Mten...