Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio (wa tatu kutoka kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kutoka kulia na Mwanasheria wa LHRC, Halord Sungusia, Mwakilishi wa Taasisi ya YPC, Maria Kayombo na Mwakiliashi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Melikizedeck Karol.
Saturday, October 31, 2015
TAARIFA ILIYOTOLEWA NA UMOJA WA VIJANA WA CCM KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 31 OKTOBA 2015 MAKAO MAKUU YA UVCCM DAR ES SALAAM
Ndugu Waandishi wa Habari,
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi unachukua nafasi hii kukipongeza kwa dhati Chama Cha Mapinduzi (CCM) na aliyekuwa mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais mteule Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na mgombea mwenza wake Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kupata ushindi wa kidemokrasia wa kishindo kwa kupata asilimia 58.46%.
Ushindi huo ni alama na kielelezo cha kuendelea kukubalika kwa CCM mbele ya Watanzania walio wengi kutokana na Sera zake, Mipango yake na mikakati ya kuwatumikia wananchi, kulinda amani, utulivu na kuendeleza Umoja wa Kitaifa nchini.
Ndugu waandishi wa habari,
Kwa upande mwingine tumelazimika kuwaita hapa leo kuelezea masuala muhimu kadhaa yaliyojitokeza katika Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, mwaka 2015.
Kama ilivyotolewa taarifa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha, kwamba Uchaguzi wa Zanzibar kwa sehemu kubwa ulikumbwa na kasoro nyingi za kimsingi ambazo zimesababisha Tume kufuta matokeo kwa nafasi za Urais, Wawakilishi na Madiwani.
Ndugu waandishi wa habari,
UVCCM tumefanya tathmini ya haraka na kina ili kujua kiini cha tatizo hilo ikiwemo kukusanya taarifa toka vyanzo mbalimbali ambapo tumebaini na kugundua madhaifu kadhaa yaliyojitokeza katika hatua za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa upande wa Zanzibar.
Tumepata wasiwasi wa suala zima la namna zabuni ya karatasi za kupigia kura ilivyotangazwa na kumpata mzabuni ambae alipewa kazi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Ni ukweli usiopingika kwamba ZEC ilizidiwa nguvu na wanasiasa wa Chama cha Upinzani cha CUF ambao kwa kiasi fulani wameshinikiza Tume ya Uchaguzi kwa namna moja au nyingine kuikubali Kampuni ya ya Afrika Kusini ambayo sifa zake zinafahamika kuwa ina matatizo.
UVCCM tuna mashaka na kampuni hiyo iliyopewa kazi ya kuchapisha vifaa vya Uchaguzi ambayo kumbukumbu zinaonyesha iliwahi kuomba kazi ya kutayarisha vifaa kama hivyo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na kupewa, lakini SMZ baada ya kugundua kampuni hiyo ina matatizo, ilivunja mkataba na karatasi za kura zilichapishwa hapa hapa nchini.
Kampuni hii inalalamikiwa kuwa chanzo cha kuvurugika kwa chaguzi mbalimbali katika nchi za Afrika ikiwemo Cameroon, Benin, Ivory Coast na baadhi ya nchi za Latini Amerika. UVCCM tumeshangazwa sana kuona ZEC wakiikubali Kampuni ambayo tayari SMZ mwaka 2005 waliikataa na kuvunja nayo mkataba.
Kampuni hii inasemekana kwamba imekuwa inashirikiana na vyama vya upinzani hasa katika nchi za Afrika chini ya mkakati wa kuvisaidia kushinda Uchaguzi.
Pia tumepata mashaka na watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ama walizembea au walikuwa sehemu ya njama za kutaka kuvuruga uchaguzi. Kwa nini tunasema hivyo? Ni kwa sababu watendaji wa Tume ya Uchaguzi wanaifahamu vyema Kampuni hii, matatizo yake, lakini wameshindwa kuishauri Serikali na matokeo yake kuiingiza nchi katika hasara na mkanganyiko wa kisiasa.
Tunawataka watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kujipima kama wanatosha kuendelea kuwa na sifa ya kuwa Watendaji wa Tume hii sambamba na Makamishna wao ambao nao hawakujituma zaidi kujiridhisha na utendaji kazi wa Kampuni hiyo kwa kuzingatia taarifa za nyuma za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hasa pale ilipovunja Mkataba.
Kwa mwenendo huo na mtazamo halisia ni wazi kuwa Chama cha CUF kimehusika na njama hizi za wizi wa kura na ndio maana Katibu Mkuu wake Seif Shariff Hamad akaamua kukiuka taratibu na kajitangazia ushindi kinyume na Katiba na Sheria za nchi wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea katika majimbo ya Pemba na Unguja. Ni kituko na mshangao kuona vyombo vya dola vikimtazama macho mgombea huyo aliyefanya kosa la jinai bila ya kumchukulia hatua za kisheria na kumfikisha kwenye mikono ya sheria.
Umoja wa Vijana wa CCM tunaitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kuunda Tume huru itakayochunguza kwa kina na undani wa kadhia hii ikiwemo suala zima la namna ilivyoendeshwa zabuni hadi kufikia kupatikana mzabuni na taarifa yake itolewe kwa umma.
Ndugu waandishi wa habari,
Tumekuwa tukisema mara kadhaa Chama cha CUF ni chama ambacho kimezoea kuwahamasisha wafuasi wao kufanya vurugu, ghilba, ubaguzi na masuala mengine ambayo hayaendani na kanuni za kidemokasia.
Katika kuyathibitisha haya, wakati wa kazi ya kupigakura na kuhesabu kura huko Kisiwani Pemba, wafuasi wa CUF wakiwa na jazba wamevamia vituo vya kupigia kura kinyume cha sheria na kuanza kuwashambulia kwa mapanga Mawakala wa Chama cha Mapinduzi na kuwatoa nje, huku wengi wao wakijeruhiwa vibaya.
Wafuasi hao wa CUF wakiwa katika makundi, wameyafanya hayo katika Vituo vya Majimbo ya Tumbe, Micheweni na Konde katika Mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo Mawakala wa CCM wamewapiga na kuwajeruhi na kusababisha kusimamishwa kwa kazi za kuhesabu kura.
Hadi sasa Mawakala wetu hali zao sio nzuri bado wapo hospitalini wakiendelea kupatiwa matibabu. Tumekuwa tukijiuliza inakuwaje Pemba CUF hawataki vyama vyengine kushiriki Uchaguzi kwa kuwafanyia vitendo vya kuwapiga, kuwabagua, kuwabughudhi wakati wao wanashiriki katika kila uchaguzi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Ndugu waandishi wa habari,
Haikuishia katika Majimbo hayo tu, bali uvunjaji wa sheria uliendelea katika sehemu mbalimbali za huko Pemba ambapo wafuasi wa CUF waliokuwa wamekaa pembezoni mwa barabara karibu na Vituo vya Makangale, Kisiwani kwa binti Abeid, Chonga, Mtambwe, Wete, Kojani, Mchangamdogo wafuasi hao wa CUF waliwazuia wana CCM wasiende kupigakura.
Mbali na kufanya hivyo, pia katika huduma za usafiri wafanyakazi wa gari za abiria za kutoka Wete kwenda Gando, Konde-Wete, Chake ? Wete kupitia njia kongwe waliwashusha wana CCM na huku katika vituo vyengine vya kupanda abiria wakiwakataa wana CCM wasipande magari yao
Hivi wanataka kutuambia kuwa CCM na vyama vyengine nje ya CUF havina haki ya kushiriki katika Siasa Kisiwani Pemba? Ubaguzi huu haukubaliki na tunawaomba wapenda demokrasia wote na Jumuiya za Kimataifa kuchukia vitendo vya kibaguzi na kihuni vinavyofanywa na wafuasi wa CUF kule Pemba.
Ndugu waandishi wa habari
Tangu siku ya Jumatatu wafuasi wa CUF kule Pemba wanachanganya maji na dawa ya kusafishia chooni au kwenye masinki ya kuoshea vyombo wanawamwagia wafuasi wa CCM ama katika makazi yao au usiku wakiwa wamelala wanawamwagia maji hayo ambayo yanawaletea madhara ya kuwashwa mwilini.
Ni dhahiri kuwa Chama cha CUF hakipati kura nyingi kule Pemba kwa ridhaa ya wapigakura, bali ni kwa kuwashurutisha wapigakura , kutoa vitisho na hata katika baadhi ya Majimbo wanawake wametishiwa na waume zao wasipopiga kura CUF watapewa talaka.
Hali kama hiyo pia imejitokeza katika Shehia za Kijini na Potoa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja ambapo wanaume waliwashurutisha wake zao kwamba watakapofika kituo cha kupigia kura wadai hawajui kusoma na kuandika au wana matatizo ya kutokuona vizuri ili waume zao wapige kura kwa Chama cha CUF. licha ya sheria kuzuia mikusanyiko ya watu karibu na vituo vya kupigia kura huko Pemba wafuasi wa CUF walikusanyika karibu na vituo vya kupigia kura Katika majimbo ya Ole, kojani, Chonga, Mkanyageni, Mtambwe, Wete, Jadida, na Konde,. Vituo vya shengejuu pujini, kiuyu, Minungw'ini kulikuwa na wafuasi wa CUF waliokusanyika na hata walipotakiwa kuondoka na polisi hawakutii.
Ndugu waandishi wa habari,
Yote hayo yametendeka mbele ya macho ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi na licha ya mawakala wetu kulalamikia ukiukwaji huo wa demokrasia hakuna aliyewasikiliza. Ni wazi kuwa kuliandaliwa mazingira ya wizi wa kura na ukiukwaji wa taratibu na sheria uliopewa baraka na baadhi ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi tunalaani vikali vitendo vya wafausi wa Chama cha CUF na tunaziomba pia Jumuiya za kimataifa kuungana nasi katika kulaani vitendo hivyo ambavyo havikubaliki hata kidogo.
Tunaviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuwasaka wale wote wanaohusika na uharamia huu na kuwafikisha katika vyombo vya kisheria.
Sote tunafahamu kuwa misingi ya uchaguzi huru ni pamoja na masuala mazima ya kutotishwa wapigakura, kutoshurutishwa kupiga kura kwa Chama fulani kwa maana mpigakura awe huru kuchagua Chama anachokitaka , kuwepo kwa mawakala na watazamaji wengine wa Uchaguzi mambo ambayo kwa sehemu kubwa hayazingatiwi katika Majimbo mengi kule Pemba.
Wakati tukijiandaa kurejea Uchaguzi wa Zanzibar UVCCM. Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuwa makini na watendaji wake hasa wasimamizi wa vituo kule Pemba ambao kwa namna moja au nyingine wanashirikiana na Chama cha CUF kuvihujumu Vyama vingine hasa Chama cha Mapinduzi.
Ndugu waandishi wa habari,
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na pengine ilijulikana mapema na waangalizi wa Uchaguzi, Makundi ya Waangalizi wa
Uchaguzi hasa wale wa Kimataifa walikipa kisogo Kisiwa cha Pemba. Tujiulizeni kwa nini waangalizi wengi walisalia katika Kisiwa cha Unguja na kukiacha Kisiwa cha Pemba?
Hata hivyo tunazo taarifa za uhakika kuwa baadhi ya waandishi wa habari nao waliondolewa kwa hila na vitisho huko Pemba kwa madai kuwa kungeweza kutokea machafuko ambayo yangehatarisha aidha maisha au usalama wao .
Mpango huo wa vitisho tumepata ushahidi umeratibiwa na kusimamiwa ipasavyo kwa karibu na waandishi wawili wa habari wa kike ambao ni wafuasi na mashabiki wa CUF waliokuwa wakipokea maelekezo kutoka kwa Kiongozi mmoja wa Upinzani huko Zanzibar.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
KAIMU KATIBU MKUU
ANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA HAPA
Baraza la Mitihani Tanzania - NECTA limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba iliyofanyika September 9 na 10 mwaka huu ambapo mikoa ya kanda ya ziwa imefanya vizuri ikilinganishwa na mikoa mingine nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk. Charles Msonde amesema jijini Dar es salaam kuwa jumla ya watahiniwa 51,8034 kati ya 76,3602 wamefaulu sawa na asilimia 67.84, ambapo kati yao wasichana wamefaulu kwa asilimia 64.60 na wavulana asilimia 71.58 huku kiwango hicho cha kikiongezeka kwa asilimia 10.85 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana wa asilimia 56.99.
Dk. Monde amezitaja shule zilizofanikiwa kuingia kumi bora kitaifa mwaka huu ni pamoja na shule ya Waja Springs ya Geita iliyoshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Enyamai ya Mara na Twibhoki pia ya Mara katika nafasi ya tatu huku zikifuatiwa na shule nyingine 7 zote kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. Shule ya Mwashigini ya mkoani shinyanga imetajwa kushika nafasi ya mwisho.
Katika hatua nyingine Dk. Msonde amezungumzia pia kukamilika kwa maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne ambayo itafanyika kuanzia nov mbili hadi 27 mwaka huu na kuwataka wasimamizi pamoja na watahiniwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ili kuepuka kufutiwa mitihani hiyo.
Kwa kuwa mitihani hiyo inafanyika tanzania bara na visiwani Dk Msonde amewatoa hofu watahiniwa wa Zanzibar ambako kuna hofu ya uvunjifu wa amani kutokana na masuala ya kisiasa kuwa mitihani hiyo itaendelea kama kawaida kwani suala la ulinzi limeimarishwa.
Kwa kuwa mitihani hiyo inafanyika tanzania bara na visiwani Dk Msonde amewatoa hofu watahiniwa wa Zanzibar ambako kuna hofu ya uvunjifu wa amani kutokana na masuala ya kisiasa kuwa mitihani hiyo itaendelea kama kawaida kwani suala la ulinzi limeimarishwa.
BOFYA jina la Mkoa kupata matokeo yake
ARUSHA | DAR ES SALAAM | DODOMA |
IRINGA | KAGERA | KIGOMA |
KILIMANJARO | LINDI | MARA |
MBEYA | MOROGORO | MTWARA |
MWANZA | PWANI | RUKWA |
RUVUMA | SHINYANGA | SINGIDA |
TABORA | TANGA | MANYARA |
GEITA | KATAVI | NJOMBE |
SIMIYU |
MAGUFULI AWASHUKURU WAPIGA KURA
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wapenzi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla fupi ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa uliofanyika oktoba 25 mwaka 2015.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana(katikati) pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakati wa sherehe ndogo ya kushukuru wapiga kura walioipa CCM ushindi.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote
waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwa wananchi waliojitokeza kumpongeza nje ya Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akionyesha cheti alichokabidhiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kushinda kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.
Mama Samia Suluhu aliyekuwa Mgombea Mwenza akionyesha cheti chake cha Umakamu wa Rais kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mke wake Janeth Magufuli mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mteule wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza kwenye hafla hiyo ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya Ofisi Ndogo CCM Lumumba.
Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa jiji la Dar es Salaam mara baada ya kumalizika hafla ya kuwasalimu na kuwashukuru kwa kumpigia kura zilizompa ushindi wa kiti cha Urais.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya ofisi ndogo CCM Lumumba. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
MAMBO YALIVYOKUWA KWENYE HAFLA YA KUKABIDHIWA CHETI CHA URAIS DKT MAGUFULI NA MAKAMU WAKE MHE SAMIA SULUHU HASSAN
Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mhe. Anna Mghwira na wagombea wengine wakiwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na wagombea wengine wakielekea ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan na Mhe Anna Mghwira na wagombea wengine wakielekea ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan na Mhe Anna Mghwira na wagombea wengine wakielekea ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Jaji Damia Lubuva wakiwa tayari katika sehemu yao
Meza kuu
Mke wa Rais Mteule Mama Janet Mgufuli akisalimiana na Waziri wakuu wastaafu Mzee John Malecela na Jaji Joseph Sinde Warioba
Mama Janet Magufuli akisalimiana na Mama Salma Kikwete
Subscribe to:
Posts (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...