Sunday, September 26, 2010

Shule ya Sekondari Tabora Girls





Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora (pichani juu) iko karibu na shhule niliyosoma miye ya Tabora Boys, ni miongoni mwa shule kongwe, zilizosifika na bado inaendelea kusifika kwa kiwango cha elimu watoacho.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1928 kama shule ya msingi kwa wakati huo wa ukoloni, ilijulikana kwa jina la African Girls School. Shule hiyo yenye ukubwa wa hekta zaidi ya 97, ilianzishwa na wakoloni wa Kiingereza kwa madhumuni ya kutoa elimu kwa watoto wa kike wa machifu.

Mwaka 1957, shule ilipewa hadhi ya kuwa sekondari ya wasichana ambapo mwaka 1972 ilianza kusajili wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo wenye ulemavu wa ngozi (albino) na wasioona.

Kaulimbiu ya shule ni strive to excel yaani kazana ufanikiwe, huu ni ukweli unaobainishwa na uwepo wa wanataaluma waliobobea katika fani ya sheria, udaktari, uhandisi, ualimu na hata katika siasa waliosoma katika shule hiyo.

Miongoni mwa viongozi waliosoma katika shule hiyo ni pamoja na Mke wa Rais mstaafu na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa sawa kwa Wote (EOTF), Mama Anna Mkapa, aliyewahi kuwa Rais wa Bunge la Afrika na Mbunge wa Ukerewe, Getrude Mongella.

Wengine ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Margareth Sitta na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Batilda Buriani.

Pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Celina Kombani, aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT- Taifa) Anna Abdallah, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Dk. Joyce Ndalichako.

Wamo pia Jaji mstaafu Julie Manning, Jaji wa Mahakama Kuu, Eusebia Munuo na aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Makazi Duniani (UN Habitat), Profesa Anna Tibaijuka. Nidhamu ya shule hiyo ni jambo ambalo linawasaidia wanafunzi wasomao shuleni hapo kuwafungulia milango ya mafanikio katika maisha yao. PICHA KWA HISANI YA CONSTANCIA MGIMWA NA JANETH WASSIRA.

Mtoto wa Mkulima yuko Iowa


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Senetor wa Jimbo la Aiwa nchini Marekani, Chuck Grassley wakati lipozungumza na wanachama wa Shirika lisilo la Kiserikali la Empower Tanzania kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Aiowa,leo.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Dean of Students wa Iowa State University of Agriculture and Life Science, Windy Wintersteen kwenye ukumbi wa Chuo hicho nchini Marekani, leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiendesha trekta kubwa la kulimia aina ya John Deere wakati alipotembelea shamba la mahindi la Summit katika jimbo la Iowa nchini Marekani. Kampuni hiyo inakusudia kuwekeza katika kilimo nchini. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Wednesday, September 22, 2010

Meja Jenerali Natepe afariki dunia


MMOJA wa viongozi 14 walioasisi na kutekeleza Mapinduzi ya Januari 12, 1964 yaliyoindoa serikali ya Kisultani visiwani Zanzibar Meja Jenerali Abdallah Said Natepe amefariki dunia jana mchana katika hospitali kuu ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, kifo hicho kimetokea jana mchana katika hospitali hiyo kuu ya jeshi la wananchi.

Taarifa hiyo ilimnukuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akieleza kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha mwanamapinduzi huyo na alimtumia salamu za rambirambi Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuelezea jinsi alivyoguswa na kifo hicho cha Mzee Natepe.

“Kifo kimemchukua mwanamapinduzi, mzalendo na mwanachama wetu mwaminifu katika kipindi ambacho taifa na Chama bado kinamhitaji sana, kifo kimetunyang’anya tunu wakati huu tunaoelekea Uchaguzi Mkuu, ni huzuni kubwa kwetu, ni majonzi makubwa na hatuna neno kubwa linaloweza kuelezea huzuni hii,” Rais Kikwete alisema.

Rais alipokea taarifa za kifo cha Mzee Natepe leo mchana akiwa Njombe mkoani Iringa ambako yuko kwa ajili ya shughuli za kampeni.

Rais, kupitia kwa Katibu Mkuu wa CCM, pia alituma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu na jamaa wa Marehemu Natepe.

“Mzee Natepe amekua sehemu ya maisha yangu ya kisiasa, kijamii na amenipa malezi na maelekezo mengi nikiwa kama kijana wake na amekua moja ya nguzo yangu kubwa katika shughuli zangu za kisiasa na kikazi katika maeneo yote niliyotumikia nchi yangu," alisema Rais na kuelezea kwa masikitiko huzuni aliyonayo na kuwahakikishia kuwa yuko nao katika kipindi hiki kigumu.

“Tunamshukuru mwenyezi Mungu kwa kutupa nafasi ya kuishi na Mzee Natepe na kufanya naye kazi, tunamuomba Mungu amlaze Mzee wetu mahali pema peponi na kumpa pumziko la milele, Amina”.

Tuesday, September 21, 2010

Rage Hoyeeee, ndivyo anavyoonekana kusema Dk Bilal


Mgombea Mwenza wa Urais Kupitia tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Tabora mjini, Aden Ismail Rage, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwrnye Uwanja wa Shule ya Sekondari Uyui jana Sept 21.

Rais Kikwete ahudhuria msiba wa Julius Msekwa


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Julius Msekwa ambaye ni mtoto wa Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa nyumbani kwao Bongoyo Oysterbay, jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Julius Msekwa ambaye ni mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu , Bongoyo Oysterbay jijini Dar es Salaam jana jioni. Marehemu Julius Msekwa aliyefariki wiki iliyopita huko Nicosia Cyprus ambapo alikuwa akifanya kazi ya mtaalamu Mshauri bingwa katika fani ya teknolojia ya Mawasiliano, alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete,(wapili kushoto) Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa(kushoto) na mkewe Mama Anna Abdallah (watatu kushoto) pamoja na Rais mstaafu awamu ya tatu Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia) wakishiriki ibada ya mazishi ya kumuombea Marehemu Julius Msekwa aliyefariki huko Nicosia Cyprus wiki iliyopita na kuzikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.(picha zotena Freddy Maro).

Monday, September 20, 2010

Kampeni za vyama vingine bwana!!!


Katibu Mkuu wa chama cha Alliance for Tanzania Farmers Party Rashid Ligania Rai (kulia) akimnadi mgombea urais wa Zanzibar kupitia chama hicho, Said Soud kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho cha wakulima kwenye uwanja wa Komba wapya mjini Zanzibar jana.

Wamasai waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama cha wakulima cha, Alliance for Tanzania Farmers Party ambapo mgombea urais wa Zanzibar wa chama hicho, Said Soud amelaani tabia ya uongozi wa baraza la manispa la kuwanyanyasa wamasai wanaofanyabiashara kwenye mji wa Zanzibar.

3611: Mgombea Urais wa zanzibar kupitia chama ca Alliance for Tanzania Farmers Party, Said Soud (kushoto) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Rashid Ligania Rai wakati wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwenye uwanja wa Komba wapya mjini Zanzibar jana. Picha zote na Martin Kabemba.

Ethiopian Airways yapata bosi mpya


BODI ya uendeshaji wa Shirika la ndege ya Ethiopian Airlines imeteua Ato Tewolde G. Mariam kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo.

Tewolde ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa katika nyadhifa mbalimbali katika shirika hilo, na kuendesha ofisi mbalimbali za shirika hilo duniani ikiwemo India, Saudi Arabia na Marekani anachukua nafasi ya Ato Gilma Ako kuanzia Januari 2011.

Mbali na nafasi hizo Tewolde alikuwa Afisa Mtendaji wa Masoko na mauzo wa Ethiopian Airlines na anaelezwa na Mwenyekiti wa bodi kuwa aliweza kukuza faida ya shirika hilo na kuliwezesha kuwa shuirika linalojiweza Afrika.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekti wa Bodi hiyo, Ato Seyoum Mesfin imeeleza kuwa imempongeza Ato Girma wake kwakuwweza kuendesha shirika hilo kama Afisa mtendaji Mkuu tokea mwaka 2004 na kufanya shirika kukua na kujenaga heshima kwa kipindi chote hicho.

“Ato Girma amewezesha shirika kukuwa katia historia la Shirika kutokana na Mpango 2010 uliowezesha shirika hilo kuwa la 16 katika mashirika yanayopata faida duniani”.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa imechukua uamuzi huo ili kuwezesha shirika hilo kutekeleza kikamilifu mpango wa 2025 ambapo linahitaji kujitanua zaidi na hivyo kuteua mtu anayefaa kuweza kuendesha shirika hjilo wakati Ato Girma anastaafu.

“Kwa kuwa atio Girma amefanya kazi kwa muda wa miaka 37 , muda umefika kwake kustaafu na Ato Tewolder Gebremariam ameteuliwa kama Mtendaji Mkuu mteule mpaka Desemba 2010 kabla ya kuanza kazi rasmi”.

Jk akutana na majaji


The President of the African Court on Human and People’s Rights , Jean Mutsinzi presents a copy of the protocol establishing
the African Court on human and Peoples’ rights to President Jakaya Mrisho Kikwete during the opening of the 18th Ordinary session of the Court held at the Golden Tulip Hotel in Dar es Salaam this morning (photos by Freddy Maro)

Saturday, September 18, 2010

Dk Slaa aiteka Karatu


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu leo. (Picha na Joseph Senga)

Tuesday, September 14, 2010

Mpango wa TWENDE




Stella Kibonde (right) explains a point to one of the journalists at 361 degrees Office during the press conference with journalists on the importance of participating in TWENDE. Farha Sultan (Left), Shamsa Hamud (Middle)

Monday, September 13, 2010

Dk Slaa afunika Bunda


Mgombea Urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ),Dk.Willibrod Slaa,akiwahutubia maelfu ya Wananchi wa mji wa Bunda, Kwenye uwanja wa Sabasaba katika mfululizo wa kampeni zake jana.Picha na Joseph Senga

Sunday, September 12, 2010

Mambo ya Chadema hayo


Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk Willibrod Slaa (wa nne kushoto), akiwaongoza wagombea wa ubunge na udiwani, kuwaaga wananchi kijiji cha Igombe katika jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, baada ya mkutano wake wa kampeni jana. (Picha na Joseph Senga)

Miss Tanzania 2010



Genevieve Emmanuel

Genevieve Emmanuel ndiye Vodacom Miss Tanzania 2010, mshindi wa pili ni Glory Mwanga na wa tatu ni Consolata Lukosi.Picha zote na Venance Nestory.

Watoto wafa kwenye disko mkesha wa Idd


WATOTO wawili wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa vibaya baada ya kukosa hewa ukumbini walikokuwa wamejazana kusherehekea sherehe za Idd.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa tukio hilo la pili kutokea wakati wa sherehe za Idd, lilitokea usiku wa kuamkia jana katika ukumbi wa disko wa Luxury Pub ulioko Temeke, jijini Dar es Salaam.

Oktoba mosi mwaka 2008, maafa ya aina hiyo yalitokea mkoani Tabora ambako watoto 19 walifariki dunia kwa kukosa hewa kwenye ukumbi wa Disco wa Bubbles unaomilikiwa na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, David Misime aliliambia gazeti hili jana kuwa tukio lililoua watoto wawili mkoani Dar es Salaam, lilitokea saa 2:30 usiku baada ya umeme kuzima.

"Baada ya umeme kuzimia watoto hao walianza kujazana kwenye mlango wa dharura ili watokea nje kufuatia geti kubwa kufungwa. Kimsingi walikufa kwa kukosa hewa na kukanyagana," alisema Kamanda Msime.

Kamanda Msime aliwataja watoto waliopoteza maisha katika tukio hilo kuwa ni Lilian Ellysangu (8) na Amina Ramadhani (7).

Kamanda Msime pia aliwataja watoto waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni Salia Hemed (6) Issa Said (10) Bernad Joseph (6), Adina Adam (9), Rukia Hemed (14) na Hashimu Shamte(17) na kueleza kuwa wote wamelazwa katika hospitali ya Temeke.

Kwa mujibu wa kamanda huyo, baadhi ya majeruhi hao wametibiwa na kuruhusiwa lakini, Omari Athumani (18), Latifah Balawa (13), Abdalah Muhaji (10), Lissah Mwamba (10), Abdalah Mlaji (10) na Mohamed Ally (14) wanaendeleana matibabu hospitalini hapo.

"Polisi inawashikilia watu kumi kufuatia tukio hilo na tayari tumeufunga ukumbi huo kwa muda usiojulikana huku tukiendelea na uchunguzi," alisema kamanda Msime.

Aliongeza: “Tunafanya uchunguzi tuone kama kuna uzembe ili tujue cha kufanya kwa kufuata sheria”.

Akisimulia kuhusu tukio hilo, Kamanda Msime alisema baada ya umeme kukatika watu walijazana katika mlangoni wa ukumbi hivyo kushindwa kutoka nje ya ukumbi kwa vile walikuwa wanatumia mlango mmoja ambao ni mdogo badala ya mkubwa.

Kamanda huyo alibainisha kuwa kisheria wamiliki wengi wa kumbi za starehe za watoto sheria wanatakiwa kufunge saa 12:00 jioni ili kuwapa fursa watoto hao kurudi nyumbani mapema.

"Tukio hili limetokea zaidi ya muda huu unaotakiwa kisheria. Hapa inaonyesha wenye kumbi za starehe wanajali pesa zaidi kuliko maisha ya watu na mali zao," alisema Kamanda huyo.

Baadhi ya watoto waliojeruhiwa katika tukio hilo waliliambia gazeti hili wakiwa hospitalini wanakoendelea na matibabu kuwa ndani ya umbi huo pia kulikuwa na watu wazima.

“Mara baada ya umeme kukatika tu watu walianza kurusha chupa za bia ambazo ziliwaumiza baadhi yao na kuwafanya wakimbilie mlangoni na kuanza kukanyagana,” alisema Rukia Hemed.

Alisema walipokuwa wanajaribu kutoka nje ya ukumbi huo, mlinzi aliwazuia mlangoni akieleza kuwa anahofia wezi kuingia ndani ya ukumbi.

Hashimu Shamte ambaye alivunjika mguu alisema umeme ulikuwa umezima ndani tu kwani walipotoka nje walikuta taa zikiendelea kuwaka
Alisema hali hiyo inamaanisha kuwa waliozima umeme ni watu waliokuwa wanahusika na ukumbi na wala sio kukatika kwa umeme wa Tanesco.

Mmoja wa marehemu Amina Ramadhani, alizikwa jana saa 7:00 mchana katika makaburi ya Mbagala jijini Dar es Salaam wakati mazishi ya Lilian Ellysangu yanasubiri mama yake mzazi ambaye yuko Arusha kwa matibabu.

Shangazi wa marehemu Lilian Ellysangu, Amina Athumani ndiye aliyetoa taarifa za mazishi hayo kufanyika baada ya mama mzazi wa marehemu.
Habari hii imeandaliwa na Hussein Issa, Pamela Chilongola na Hermenegildus Rwihula

Saturday, September 11, 2010

tigo wazindua huduma yao ya tigo pesa kwa kishindo coco beach

Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva Joe Makini akikamua jioni ya leo wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Tigo iitwayo Tigo Pesa ndani ya Coco Beach jijini Dar ambao maelfu ya watu walijitokeza kushuhudia uzinduzi huo uliofana kwa kiasi kikubwa.

Maelfu ya watu kutoka vitongoji mbalimbali vya jiji la Dar jioni ya leo

Mwanamuziki machachari Dully Sykes akiwaimbisha watazamaji wimbo wake wa Shikide jioni ya leo Picha na habari zaidi

http://michuzijr.blogspot.com/2010/09/tigo-wazindua-huduma-yao-ya-tigo-pesa.html

Friday, September 10, 2010

JK atoa mkono wa IDD

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu muda mfupi baada ya kumalizika kwa swalla ya Iddi iliyoswaliwa katika Msikiti Mkuu wa Riyadh mjini Tanga leo asubuhi.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono wa Iddi na Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakati wa Swalla ya Iddi iliyoswaliwa katika Msikiti mkuu wa Riyadh mjini Tanga.Mzee Mwinyi ndiye mgeni Rasmi katika baraza la Iddi litakalofanyika kitaifa mjini Tanga.Picha za freddy Maro wa Ikulu.

Thursday, September 09, 2010

Futari Zanzibari



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Amani Abeid Karume,akisalimianana Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad, baada kufutari pamoja na wananchi wa Mikoa mitatu ya Unguja, futari hiyo iliandaliwa na Rais huko Ikulu ya Zanzibar.

Baadhi ya wake wa viongozi waliohudhuria katika futari iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Amani Abeid Karume, kwa mikoa mittu ya Unguja huko Ikulu mjini Zanzibar.

Picha na Ramadhan Othman Ikulu.

Wednesday, September 08, 2010

Ujumbe wa Eid el-Fitr


Balozi Alfonso E. Lenhardt

Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni muda ambao Waislamu duniani kote wanafunga, wanaswali na kufanya matendo mema. Aidha, ni wakati wa kutafakari na kuimarisha imani zao, kutenda mema, kuwasaidia wenye shida na kuwa na huruma. Kwa niaba ya Watu wa Marekani, ninapenda kuwatakia Waislamu wote wa Tanzania Eid el-Fitr njema. Muda huu wa kujitafakari unatukumbusha kuwa maadili ya Uislamu - wema, kujali wengine, kuhudumia jamii, ushirikiano na huruma ni amali ambazo sisi kama Wamarekani tunazithamini sana na ambazo kwa hakika zimechangia sana katika tamaduni nyingi duniani kote.
Kama alivyosema Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Bibi Hillary Rodham Clinton hapo tarehe 7 September katika hafla ya Iftar iliyoandaliwa na Wizara yake, historia ya Uislamu Marekani inaweza kupatikana nchini kote Marekani. Nchi yangu imejaaliwa kuwa na Waislamu waliozaliwa nchini Marekani pamoja na wale waliohamia kutoka duniani kote ikiwemo Tanzania. Dhamira yetu ya kulinda na kudumisha uvumilivu wa kidini ilianza toka mwanzoni kabisa mwa uanzishwaji wa taifa letu. Mabadiliko ya Kwanza ya Katiba ya Marekani yalipiga marufuku kuanzishwa kwa sheria yoyote inayokwaza uhuru wa mtu kufuata mafundisho ya dini yake na hivyo kuhakikisha kuwepo kwa uhuru wa kuabudu nchini kote. Kama alivyosema Rais Barack Obama wakati wa hafla ya Iftar iliyofanyika katika Ikulu ya Marekani hapo Agosti 13 mwaka huu, Balozi wa kwanza Muislamu nchini Marekani ambaye alikuwa akitoka Tunisia alialikwa na Rais Thomas Jefferson, ambaye aliandaa chakula cha jioni kwa wageni wake wakati wa magharibi kwa sababu kipindi hicho kilikuwa ni cha Ramadhani - na kufanya tukio hilo kuwa Iftar ya kwanza kuandaliwa na Ikulu ya Marekani - hiyo ilikuwa zaidi ya miaka 200 iliyopita. 
Katika ziara zangu kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi hii nzuri ya Tanzania nilipata heshima kubwa ya kutembelea Misikiti, kukutana na viongozi wa kidini na waumini wa Kiislamu ili kukuza urafiki na ushirikiano wetu. Niliguswa sana kuona utulivu na uzalendo wa hali ya juu miongoni mwa Watanzania wa imani zote.  Pengine jambo hili ni mojawapo kati ya mafanikio makubwa zaidi ya taifa hili, kama inavyoashiriwa na jina la moja ya miji yake mikuu - "bandari ya salama."   Wakati Ramadhani ikielekea ukingoni, tudumishe moyo huo wa kushirikiana na kusaidiana kama jamii moja ili watoto wetu, bila kujali wamezaliwa wapi na wanaabudu vipi waweze kupata fursa ya kuwa vile walivyopangiwa kuwa kwa jina la Mwenyeezi Mungu, na katika kuimarisha utu wetu.
Eid Mubarak.

Alfonso E. Lenhardt ni Balozi wa Marekani katika Jamhuri ya Muungano waTanzania

Midahalo sumu kwa CCM



Wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wakiwa nje wa hoteli huku wakifurahia mara baada ya kumalizika mdahalo wa Wagombea wa ubunge wa jimbo la Arusha Mjini uliofanyika katika hoteli ya Golden Rose mjini Arusha, mdahalo huo ulikuwa ukirushwa na Shirika la Utangazaji nchini (TBC1) na mgombea wa CCM katika jimbo hilo Batilda Burian aliingia mitini, taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza kuwa wagombea wote wa CCM wamepigwa marufuku kushiriki midahalo ya aina hiyo kwa kuwa inawapotezea pointi baada ya mgombea wa ubunge jimbo la Ubungo, Hawa Nghumbi kuchemka kujibu maswali katika mdahalo uliopita(PICHA NA MOSES MASHALLA)

Tuesday, September 07, 2010

Mzee wa mshituuzzz akiwa mzigoni

Mzee wa Mshitu, Yahya Charahani, (kushoto) akiwaelezea wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Loyola ya jijini Dar es Salaam, umuhimu wa vyombo vya habari, wakati walipofanya ziara ya kimasomo makao makuu ya gazeti hili jana wa pili kushoto ni mwandishi, Felix Mwagara. Picha na Zacharia Osanga

Ngoma za kwetuuuzzz


Wasanii wa ngoma za asili wa kikundi cha Dhahabu wakitumbuiza kwenye mkutano wa wadau kujadili mambo muhimu ya Katiba ya Jamhuri ya muungano na mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Michael Jamson

Mkurugenzi mpya wa Zain Tanzania


A new Managing Director of Zain Tanzania, Sam Elangalloor address the reporter from The Citizen daily newspaper during the special interview at his Head Office in Dar es Salaam. PHOTO/VENANCE NESTORY

MWISHO AND PALOMA UP FOR EVICTION AS MERYL SAVES HERSELF

Tanzania’s Mwisho and Zambia ’s Paloma up for eviction this week on M-Net’s Big Brother All Stars after Monday’s (6 September) nominations. For the first time in five consecutive weeks, Munya is not in danger of leaving the Big Brother All Stars House this weekend – while Paloma finds herself up for eviction for the first time since week one, when all the housemates stood the chance of leaving.

Once all the nominations were in, Big Brother told the Housemates that Head of House Meryl and her beau Mwisho had received the most nods from the Housemates. Summoned to the Diary Room to make her Head of House decision, Meryl hovered outside the door and asked to go to the toilet before heading inside. Once she was in the Diary Room, she was clearly distressed at having to choose between herself and ‘boyfriend’ Mwisho. She asked Big Brother for a moment after declaring “I can’t do this!”. After much hand-wringing, she decided to save herself and put Paloma up in her place.

· Earlier in the day, Munya had changed his mind after nominating Uti and Mwisho, and put Meryl in Mwisho’s place. Munya has been using the same strategy at nomination since week one, nominating the Housemates who come from the countries furthest from Zimbabwe . At first he said he was nominating Meryl because she was one of the Housemates that came from a country furthest from Zimbabwe but Big Brother would not accept that reason. He then said that his instinct was that “In the best interest of the game, if people I want to stay are to stay then I should nominate her,” he said.

Big Brother All Stars is broadcast live 24/7 for the next 41 days on DStv Channel 198, with edited highlights shows every day of the week on M-Net and later on AfricaMagic. Big Brother All Stars is also available on DStv Mobile in Ghana , Kenya , Namibia and Nigeria .

huyu ndiye Dustan Kitandula


Maneno mingi hapana, picha inaongea watu wa jimbo la Mkinga kazi kwao najua si wengi wenye access na mtandao. But wale wenye access habari ndo hiyo.

Monday, September 06, 2010

Vuvuzela Original


Mzee wa Kabila la Wahehe, Lucas Mtumbuka (74), akipuliza vuvuzela la kienyeji linalotambulika kwa jina la Baragumu, wakati wa makaribisho ya Mgombea Mwenza Dk Mohamed Gharib Bilal, alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Manispaa ya Iringa jana Sept 05 kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa mjini, Monica Mbega.

Tumbaku na uvutaji sigara


Mzee aliyetambuliwa kwa jina la Mussa Ali akiuza tumbaku katika soko la kijiji cha Nyangao Lindi vijijini. Picha na Elias Msuya

******************************************
Tumbaku ndio inayotumika vibaya ikilinganishwa na madawa mengine. Kuvuta sigara au kiko husababisha magonjwa haya, ugonjwa wa moyo, pigo, ugonjwa wa mapafu, saratani ya koo, kibofu cha mkojo, firigisi n.k

Watu wengi wanaovuta sigara wanajua kuwa ni mbaya kwa afya yao, jaribu kuwacha au usianze kuvuta.

Ukweli kuhusu tumbaku:
Tumbaku huleta saratani yam domo, ulimi, na 80% ya watu wanaovuta sigara walianza wakiwa vijana.
Kampuni za sigara huongeza madini ya ammonia kwa hivyo ubongo hufunikwa na nikotini.

Wananchi wamwambia Kikwete tunataka shamba letuu


Urais kupitia CCM, Jakaya Kikwete akiwajibu wananchi wa Mvomero baada ya kuombwa awarejeshee shamba analomiliki Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye alipokuwa kwenye ziara yake kampeni ya uchaguzi mkuu mkoani Morogoro jana. Picha na Edwin Mjwahuzi.

Saturday, September 04, 2010

Kinyang'anyiro cha kumsaka balozi wa Redd's





Baadhi ya Warembo watakaoshiriki shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010,ambao pia usiku wa kuamkia leo walikua katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Balozi wa Redd's 2o1o katika fukwe za Mbalamwezi Beach Mikocheni jijini Dar,Wageni waalikwa mbalimbali walihudhulia tukio hilo.

Mama na baba Slaa wakijinadi

Dk Slaa anamtambulisha mgombea ubunge wa Hanang na aliyekuwa mkewe, Rose Kamili, katika eneo la Endosak, jirani na nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye

Umati Mkubwa ulijitokeza kumlaki Dk. Slaa katika eneo la Haydom, jimboni Mbulu.
-----------------------
Dk. Slaa ameiteka Manyara.Na wananchi wa Manyara wamemteka pia.Ilikuwaje? Kwanza, walijaa katika mikutano yake katika majimbo ya Hanang na Mbulu.Pili, walizuia misafara yake kokote alikopita wakitaka awahutubie, walau kwa dakika moja tu! Tatu, walimwahidi kufanya mabadiliko makubwa mwaka huu kwa kuchagua wabunge na madiwani wa Chadema, ili kukifanya CCM kuwa chama cha upinzani. Kipya ni kwamba alitumia usafiri wa Kipanya (Hiace) badala ya helikopta kutoka Babati hadi Mbulu, kwa sababu helikopta ilipata hitilafu kidogo siku ya Jumatano mara baada ya kutua mjini Babati ikitokea eneo la Bashnet.Habari na Picha na Mdau Asbert Ngurumo..

Kikwete ahutubia Ngerengere leo


Baadhi ya wananchi wa Kata ya Ngerengere Morogoro vijijini wakimsalimia kwa shauku mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi kabla ya mgombea huyo kuwahutubia katika mkutano wa hadhara wa kampeni leo asubuhi (picha na Freddy Maro)

Friday, September 03, 2010

Dk Bilal kampeni Songea


Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akifurahia vazi la asili ya kabila la Wangoni na silaha ya Kinjenje, baada ya kukabidhiwa na wazee wa kabila hilo, Aidan Mbano (kushoto) na Joachim Silo, wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Bombambili mjini Songea jana.

Thursday, September 02, 2010

Nyumba ya mwalimu




Nyumba anayoishi mtumishi wa Serikali Mwalimu Domisiana Mpenda wa shule ya Msingi Iyenge iliyopo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma. Picha na Israel Mgussi.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...