Tuesday, September 21, 2010
Rais Kikwete ahudhuria msiba wa Julius Msekwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo wakati alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Julius Msekwa ambaye ni mtoto wa Makamu mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa nyumbani kwao Bongoyo Oysterbay, jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Julius Msekwa ambaye ni mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa wazazi wa marehemu , Bongoyo Oysterbay jijini Dar es Salaam jana jioni. Marehemu Julius Msekwa aliyefariki wiki iliyopita huko Nicosia Cyprus ambapo alikuwa akifanya kazi ya mtaalamu Mshauri bingwa katika fani ya teknolojia ya Mawasiliano, alizikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete,(wapili kushoto) Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Pius Msekwa(kushoto) na mkewe Mama Anna Abdallah (watatu kushoto) pamoja na Rais mstaafu awamu ya tatu Mzee Ali Hassan Mwinyi (kulia) wakishiriki ibada ya mazishi ya kumuombea Marehemu Julius Msekwa aliyefariki huko Nicosia Cyprus wiki iliyopita na kuzikwa jana katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.(picha zotena Freddy Maro).
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
1 comment:
huyu jamaa msekwa kama unavyojua wameuza nchi kusaidia familia zao, jiulize kwa nini mwanae kafia nje, kama alivyosema Malcom X ikifika jioni vifaranga hurudi nyumbani na mama, mungu anamwonyesha dhuluma zake!!!!!
Post a Comment