Tuesday, June 02, 2009

Wanachama wa Deci marufuku kuandamana kesho

*Kova aitisha kikao cha dharura na viongozi wao

*Watakiwa kukwepa wanasiasa wenye mlengo binafsi

JESHI la polisi Kanada maalum ya Dar es salaam, limepiga marufuku
mikusanyiko na maandamao yaliyopangwa na wanachama wa mchezo wa upatu unaoendeshwa na taasisi ya Development of Entrepreneurship for Community Initiative (DECI), kufanyika kesho hadi ofisi ya Waziri wa Fedha, Mustapha Mkullo kushinikiza madai ya hatma ya fedha zao.

Kauli hiyo ya onyo ilitolewa leo hii na Kamanda wa Kanda hiyo, Suleiman Kova, mara baada ya kuitisha kikao cha dharura kati yake, uongozi wa Deci na Kamati ya muda ya wanachama wa mchezo huo wa upatu, kilichofanyika kwa muda wa masaa mawili na robo, kuanzia saa 8.00 hadi saa 10.15 jioni.

Kova alisema kutokana na maadhimio waliyofikia katika kikao hicho cha dharura amegundua kuwa hakuna ulazima wa wanachama hao kuandamana wala kufanya makundi ambayo yatachafua amani ya nchi, huku hali hadhma yao ni kutaka kufikisha malalamiko yao kwa waziri na kamati iliyoundwa kuchunguza sakata lao.

“Nimekaa nao na baada ya kuwasikiliza tumegundua kuwa maandamano yao waliyotaka kuyafanya leo yamelenga kutaka kufikisha ujumbe wao juu ya hadma ya fedhya zao walizopanda jambo ambalo nimewaeleza kuwa ofisi yangu itakuwa njia ya kupitishia malalamiko yao kwa lengo la kuyafikisha sehemu husika ambayo ni serikalini,” alisema Kova. Taarifa ya Festo Polea.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...