Thursday, June 18, 2009

Bamaga jana

MOTO uliozuka jana saa 3:00 asubuhi katika kituo cha mafuta cha T.S.N. Bamaga kilichopo katika makutano ya barabara ya New Bagamoyo na Shekilango jijini Da es Salaam, unadaiwa kusababisha hasara kubwa.
Akizungumza baada ya tukio hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Faruku Ahmed, alisema moto huo uliunguza gari la kubeba mafuta aina ya Benz lenye tanki lake pamoja na jenereta ndogo.

Hata hivyo kiasi kamili hakikutajwa, ingwa mwenyekituo alisema moto umesababisha hasara ya mamilioni ya Shilingi.

Moto huo ulidaiwa kusababishwa na hitilafu katika mashine ya jenereta iliyokuwa ikipampu mafuta kutoka kwenye kisima cha mafuta ya taa na kuhamishia katika gari kwa ajili ya kuyapeleka katika kituo kingine cha kampuni hiyo kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Mi nasema kama hii mitungi ya gesi ingefanya umbagala fulani sijui leio ingekuwaje ama wananchi wa jirani nao wangepatiwa fidia kama Mbagala? kwa habari zaidi mtembelee Mzsee wa Sumo huku http://mpoki.blogspot.com/2009/06/mlipuko.html

1 comment:

Rashid Mkwinda said...

Poleni sanna maana mlikuwa mbio mbio kweli ni hatari,ni muhimu vyombo vinavyohusika na watu wanaohusika kuwa na tahadhari kabla haijatokea hatari kama hii

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...