Luis Cabral ambaye aliiongoza Guinea-Bissau mara baada ya kupata uhuru amefariki dunia akiwa nchini Ureno ambako amekuwa akiishi kama mkimbizi tangu kutimuliwa madarakani mwaka wa 1980.
Bwana Cabral ambaye alichukuwa wadhifa wa urais mnamo mwaka wa 1974 aling’olewa madarakani na Joao Bernardo Vieira ambaye aliuawa mwezi Machi mwaka huu.
Kabla ya kuhamia mjini Lisbon, Ureno, Bwana Cabral alikimbilia Cuba.
Taarifa ya serikali ilisema, “Serikali na wananchi wa Guinea-Bissau wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa Luis Cabral.”
Serikali inatarajiwa kuandaa kikao cha dharura kuandaa siku tatu za maombolezo ya kitaifa.
Habari kutoka BBC.
No comments:
Post a Comment