Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), kimezindua tawi la chuo hicho Dar es Salaam ambalo linatoa Shahada ya Uzamili na Uzamivu wa Mawasiliano ya Umma. Tawi hilo lilianza kutoa mafunzo mwaka jana.
Akizindua chuo hicho sambamba na jarida la mawasiliano barani Afrika linaloandaliwa na wanafunzi wa chuo hicho, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alisema lengo la Chuo kikuu hicho ni kujenga jiji la Mungu kwa kutoa elimu yenye ubora wa hali ya juu pia akasema lengo kubwa ni kuwafikia watanzania popote walipo.
2 comments:
Wadau naomba kuuliza, hiki chuo kipo wapi hapa Dar es salaam, na je wanatoa MBA hapa kwenye tawi lao la Dar? Nawasilisha
Chuo hiki ni sehemu ya Chuo cha Mtakatifu Augustino cha Mwanza na kwa hapa Dar es Salaam kipo ndani ya eneo la Msimbazi centre, kwa sasa chuo hiki kinatoa MA za Mass communication tu na baadae mwaka huu kitatoa shahada ya uzamivu kwenye mass communication.
Post a Comment