Monday, June 08, 2009

Mustafa Hassanali kuonyesha mavazi "wiki ya mitindo Afrika"



MUSTAFA HASSANALI KUONYESHA MAVAZI KWENYE “WIKI YA
MITINDO AFRIKA” NCHNI AFRIKA KUSINI.KUONYESHA“READY TO WEAR COLLECTION”
LIITWALO “MDUARA”.

Kampuni ya Africa Fashion International imemualika mbunifu mahari wa mavazi kutoka Tanzania kuonyesha mitindo yake kwenye maonyesho ya mawazi iliyopewa jina la ARISE Afrika Fashion Week.
Maonyesho hayo yanatajiwa kufatafanyika juni 12-19 huko Sandton Convention Centre, Johannesburg, Afrika kusini. Maonyesho hayo yatawashirikisha wabunifu 52 kutoka nchi 21 barani Afrika yatakayodumu kwa muda wa siku 8.

Miongoni mwao ni Mustafa Hassanali akiwa mbunifu pekee kutoka nchini Tanzania hii ikiwa ni mara yake ya saba kushiriki. Miongoni mwa maonyesho aliyowahi kushiriki nchini Afrika Kusini ni pamoja na “M'NET Face of Africa Finals Novemba 2008 Sun City”, Tanzanite One Jewellery Showing, Cape Town kwenye mkutano wa Mining Indaba 2007, Durban Fashion week 2006, Cape Town Fashion week 2005 & 2006 na Vukani Fashion Fair and awards, Pretoria 2004.

Mustafa Hassanali anasema “Hii ni fursa maridhawa si kwa kuweza kufahamiana na wabunifu na wadau wengine bali pia ni wakati muafaka kuweza kutafuta masoko kwa ajili ya mavazi yangu”.


Mustafa Hassanali atazindua nguo zake za majira ya kiangazi/kipupwe ya 2009/10 iitwayo MDUARA ambayo yana vionjo na mguso wa utamaduni wa jamii ya kiswahili ya kitanzania. Mustafa aongeza “Imani ya muziki asilia wa mduara umechangia kwa kiasi kikubwa katika mitindo yangu ya kipindi hiki ambayo ni mchanganyiko wa vionjo asilia vya pwani vilivyoboreshwa”.

Mutafa Hassanali amedhamiria kuitangaza fani ya ubunifu wa mavazi Tanzania na pia kuhamasisha watu kupenda vitu ambavyo vimebuniwa na kutengenezwa hapa. Akiwa anaipeperusha bendera ya Tanzania nchini Afrika Kusini, Mustafa Hassanali atafuatana na wanahabari ambao watahudhuria maonyesho yake yatakayofanyika tarehe 14 Juni na pia kufuatilia yaliyojiri nyuma ya kamera kwa kipindi chote cha Arise Africa Fashion Week.

Safari ya wanahabari hao kwenda nchini Afrika kusini
imedhaminiwa na

Vodacom Tanzania
www.vodacom.co.tz
Tanzania Broadcasting Corporation
www.tbccorp.org
1Time Airline
www.1time.co.za

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...