Thursday, January 08, 2009

Sophia Simba mwenyekiti UWT


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa taifa wa Umoja wa wanawake wa CCM (UWT).
Akitangaza matokea ya uchaguzi huo, mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Seif Khatibu alimtangaza Simba kuwa alikuwa amepata kura 470 sawa na asilimia 54.5 ya kura zote zilizopigwa na kuwaacha washindani wake, Janet Kahama aliyepata kura 383 sawa na asilimia 48.4 na Joyce Masunga aliyeambulia kura 10 sawa na asilimia 1.1 kati ya kura halali 862 zilizopigwa.

Nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti ilikwenda kwa Asha Bakari Makame ambaye alikuwa mgombea pekee, aliyepata kura 736 sawa na asilimia 60.3 na kura 70 zilimkataa.

Kwa upande wa wajumbe wa Baraza Kuu kutoka Tanzania bara walioshinda ni Betty Machangu, Magret Mkanga, Sifa Swai, kutoka Zanzibar ni Ratifa Nasoro, Subira Ally, Mtumwa Yusufu, Lilian Limo na Catherin Nao.

Kwa upande wa wawakilishi wa jumuiya za CCM walioshinda na Martha Mlata ambaye atakuwa ni mwakilishi kwa Jumuiya ya wazazi na upande wa vijana alichaguliwa Shy-Rose Bhanji ambaye alimshinda mbali mkuu wa wilaya ya Mpwapwa, Halima Dendego.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...