Wednesday, January 07, 2009

Kilimanjaro Stars yatisha Kampala


IKICHEZA soka safi na la kujiamini lililowalazimisha Waganda kuishangilia, Kilimanjaro Stars ilitandika bila huruma Rwanda kwa mabao 2-0 na kujisafishia njia, wakati wapinzani wa Uganda wakisambaratisha Somalia 4-0.
Ushindi huo umeifanya Stars kufikisha pointi sita na kuongoza kundi kwa muda, huku kiungo wake, Athuman Idd akinyemelea ufungaji bora kwa mabao mawili aliyonayo.
Stars ambayo ilianza mchezo huo kwa kushambulia kwa nguvu, iliandika bao la kwanza dakika ya nane kupitia kwa winga wake Mrisho Ngassa ambaye alipiga 'tiktak' iliyogonga besela na kutinga wavuni.
Rwanda ambayo ilicheza soka la pasi nyingi fupi fupi na kushambulia kwa kushtukiza, ilijipanga na kupandisha shambulizi kali dakika ya 10 na kupangua ukuta wa Stars, lakini Lomani Jean akachachawa na kupaisha.
Washambuliaji wa Stars walizidi kuishambulia Rwanda, ambapo dakika 23 Henry Joseph alipiga shuti kipa akatema, lakini Mrisho Ngassa akaichelewa kumalizia.
Stars ambayo wachezaji wake walikuwa wakikaba kwa nguvu, kwa kujiamini na kutowapa nafasi Rwandakukaa na mpira, ilizidi kushambulia huku wachezajiwake wakionana vizuri na kuandika bao la pili dakika ya37 kupitia kwa Athuman Iddi 'chuji'.Taarifa ya Michael Momburi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...