Monday, January 05, 2009

Mwinyi azindua kampeni kama baba wa taifa



RAIS mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi, ambaye Chadema iliilitishia kumchafua kama angekubali kuzindua kampeni za uchaguzi za CCM mkoani Mbeya, jana alijivisha jukumu la Baba wa Taifa wakati alipotumia muda mwingi wa hotuba yake kuelezea umuhimu kwa wananchi kumchagua mtu anayeona anafaa kwenye jimbo hilo, badala ya kumpigia debe mgombea wa CCM.

Mwinyi, ambaye anajulikana kama 'Mzee wa Ruksa' kutokana na kuongoza nchi wakati wa mageuzi yaliyoruhusu ushindani wa vyama vya kisiasa, hakuonyesha unazi kwa CCM wala mgombea wake wakati alipozindua kampeni za chama hicho jana katika kata ya Kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini.

Badala yake, Mwinyi alisisitiza amani, mshikamano na maendeleo ya wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwataka wananchi wa eneo hilo kuhakikisha wanabakia na mshikamano wakati wanasiasa watakapoondoka jimboni humo baada ya purukushani za uchaguzi.

Mwinyi alisema vyama vyote vya siasa nchini lazima vilenge katika kutoa majibu ya kisera kwa matatizo yanayowakabili wananchi ili kuwaletea maendeleo yakayowafanya kuwa na maisha bora.

Alisema kuwa moja ya sababu kubwa za kuanzisha siasa ya vyama vingi ni kuwapa
wananchi fursa ya kushindanisha sera za vyama mbalimbali ili wananchi waweze
kuchagua sera wazipendazo na viongozi wa kuziwasilisha, kuzitetea na kuzitekeleza.

1 comment:

Anonymous said...

mzee ruksa wewe ni mstaarabu,muungwana, na mwenye hekima nyingi,ukitaka mfano wa ile methali isemayo utuuzima dawa basi ni mzee ruksa.kila la kheri mzee wetu.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...