Monday, October 29, 2007

Waziri Simba


WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (Pichani kitandani) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal anaendelea vizuri.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili hospitalini hapo, Simba alisema hali yake ilikuwa imeimarika kuliko ilivyokuwa juzi.

"Mimi ni mzima, afya yangu inaendelea vema," Waziri Simba aliwaambia waandishi wa gazeti hili mara tu walipoingia katika wodi alipolazwa.

Kauli ya Simba ilionyesha kutokana na kuwepo watu wengi waliofika kumjulia hali siku ya jana. Watu hao walifika ikiwa ni pamoja na taarifa za vyombo vya habari kuwa, hakuweza kuhudhuria mazishi ya Naibu Waziri wake Salome Mbatia kutokana na ugonjwa.

Baadhi ya Mawaziri waliofika hospitalini hapo kumjulia hali ni Zakia Meghji na Mary Nagu ambao walifika majira ya jioni.

Wengine waliokuwepo ni wanafamilia ambao pia walitakiwa kuondoka nje ya chumba alimolazwa kutokana na chumba hicho kuwa na wageni wengi hali iliyosababisha kukosa hewa kwa mgonjwa.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...