Wednesday, October 10, 2007

Rais Kikwete azungumzia tuhuma za ufisadi

Rais Jakaya Kikwete ameonya tabia inayotaka kujengeka miongoni mwa wananchi na hususani wanasiasa ya kugeuka kuwa wapelelezi, wakamataji, waendesha mashtaka na watoa hukumu, na tena wakizitoa huku hizo bila ya watuhumiwa kuwapo.

Amesema tabia hiyo ikiachwa kuendelea siyo tu itaipeleka nchi pabaya, lakini itawatisha wananchi, itawatia hofu na kujenga chuki kati ya mtu na mtu hali ambayo amesema haiendani na taratibu za kuendesha nchi kwa misingi ya kufuata kanuni, taratibu, na sheria za nchi.

Amebainisha kwamba tabia hiyo ya wanasiasa kujigeuza kuwa wao ndio wapelelezi, wakamataji, waendesha mashtaka na watoa hukumu kuwa haimtendei haki mtuhumiwa ambaye naye ana haki yake ya msingi ya kulindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Rais Kikwete ameeleza kuwa kila taarifa inayohusu rushwa au tuhumu za mtu kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa, zitachunguzwa kwa kuzingatia misingi ya sheria za nchi na vyombo vinavyohusika na si vinginevyo na kuongeza kwamba yeyote atakayethibitishwa na mamlaka halali kwamba ama ametoa rushwa au kupokea rushwa atachukuliwa hatua za kisheria bila ya kujali nafasi na madaraka aliyonayo. ukitaka kusoma zaidi cheki TAARIFA YA IKULU HAPA

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...