Wednesday, October 24, 2007
Wahadzabe walia njaa, wamkumbuka Nyerere
WAHADZABE wanaoishi katika Bonde la Yaeda chini, wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara wanakabiliwa na njaa hivyo maisha yao kuwa hatarini.
Wakizungumza na waandishi wa habari na ujumbe wa viongozi wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) juzi katika Kijiji cha Sanora, wilayani hapa, Wahazdabe hao walisema kutokana na njaa kali na kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii, watoto wao wamekumbwa na magonjwa ya kuharisha na kutapika.
Wakizungumza kwa shida huku baadhi yao wananchi hao walimkumbuka hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye walisema alikuwa akiwapatia chakula na kwamba aliwahi kuwatembelea.
Walisema wanaamini kama Nyerere angekuwa hai wasingekuwa kwenye taabu ambayo wanaipata kwa sasa.
Mmoja wa wananchi hao, Tale Mudenda, alisema hivi sasa wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula katika jamii hiyo baada ya kupungua kwa wanyama kutokana na eneo lao kuvamiwa na wafugaji na kusitishwa kwa huduma za kitalii katika bonde hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...
-
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu na timu ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa akiwa katika ...
-
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA PSLE-2014 EXAMINATION RESULTS ARUSHA DAR ES SALAAM DODOMA IRINGA KAGERA KIGOMA ...
-
Adam Malima James Wanyancha Hamis Kagasheki RAIS Jakaya Kikwete ameteua Baraza la Mawaziri, huku likiwa na sura na damu mchanganyiko. Bar...
No comments:
Post a Comment