Tuesday, October 23, 2007

Karamagi asaini Buzwagi nyingine



SERIKALI imesaini mkataba wa miaka kumi na moja na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbon&Power (Tanzania) Limited ya Dubai ili kufanya utafiti wa mafuta katika Bonde la mto Ruvu.

Mkataba huo ulisainiwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Hasu Masrani.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini mkataba huo, Waziri Karamagi alisema kuwa awamu ya kwanza ya zoezi hilo itakayodumu kwa kipindi cha miaka minne itatumia dola za kimarekani 31.5milioni ambazo ni sawa na Sh34.7 bilioni. (Dola moja ya Kimarekani sasa inabadilishwa kwa Sh1,100)

“Mkataba huu ni wa miaka kumi na moja na Mkandarasi Dodsal anatarajiwa kutumia kiasi kisichopungua dola za Marekani 31.5milioni,” alisema Karamagi. kwa habari zaidi soma Mwananchi.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...