Friday, October 19, 2007

Nyumba ya Mbunge yachomwa moto

Na Muhibu Said wa Mwananchi

MVUTANO wa bei ya korosho, mkoani Mtwara, umechukua sura mpya, baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni wakulima katika Wilaya ya Tandahimba, kuichoma moto nyumba ya Mbunge wa Jimbo hilo, Juma Njwayo, wakipinga kuuza zao hilo kwa mkopo.

Vilevile watu hao wameripotiwa kukata mikorosho kadhaa, ikiwamo mikorosho zaidi ya 25 inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tandahimba (TAFA), Adinani Mbwana.

Mbali na hujuma hizo, watu hao pia wameripotiwa kuchinja mifugo mbalimbali ikiwamo bata, kuku na mbuzi wa dereva wa mkuu wa wilaya na kufunga kwa kufuli maghala yote ya vyama vya msingi vya ushirika wilayani humo yanayotumika kuhifadhi na kuuzia korosho.

Habari kutoka Tandahimba zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Miti Francis, zinaeleza kuwa hujuma hizo zimefanyika siku chache baada ya wakulima wa zao hilo kufanya maandamano makubwa hivi karibuni kupinga suala hilo. Soma GAZETI LA MWANANCHI upate taarifa zaidi.

1 comment:

Anonymous said...

Muy buena entrada!!!

Me gustó el artículo que posteaste.

Ya que pasaba te invito a conocer el sitio sobre motos modificadas que hicimos con unos amigos:

http://www.Tuneadas.com

Espero que te pases! Besos!

Moto tuning http://www.Tuneadas.com motos modificadas motos tuning tuning de motos motocicletas tuneadas foros noticias tuning cómo tunear tu moto consejos moto tuning accesorios tuning y más.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...