Tuesday, October 30, 2007

Mzee Malechela



Uchaguzi keshokutwa ambapo bila shaka inatarajiwa Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mzee John malechela maarufu kama babu kwamba anaweza kuachia ngazi na kuendelea kubakia kama mshauri na kuwaachia vijana waendeleze libeneke, picha hii imenaswa juzi nyumbani kwake. Uchaguzi una mambo yake huenda ukaibuka na sura mpya kibao ikiwamo kubwagwa mzee Makamba.

Gongo yamuua akishangilia ushindi wa CCM

Na Abdallah Nsabi wa Mwananchi

FURAHA ya ushindi wa Chama cha Mapinduzi CCM kupata ushindi wa Udiwani imemtokea puani mkazi wa kata ya Nguliguli Wilayani Maswa Lonjini Petro (54) baada ya kunywa lita tatu za pombe aina ya gongo na kufariki dunia.

Tukio hilo lilitokea juzi katika kata hiyo baada ya kutangazwa matokeo ya ushindi wa chama hicho ndipo Petro alipokwenda nyumbani kwa Gumba Mboje na kuangiza lita tatu za gongo ili anywe afurahie ushindi huo ambao alikuwa anausubiri kwa hamu na kukutwa na mauti.

Chanzo cha habari kutoka katika eneo hilo kilisema kuwa Petro aliwekeana ahadi na mtu mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana kuwa iwapo chama cha CCM kingeshinda wangenunuliana pombe aina ya gongo na kunywa mpaka asubuhi.

Pia ilieleza kuwa Mara baada ya ushindi wa chama cha Mapinduzi CCM, marehemu aliamua kujikita katika moja ya nyumba ambayo wanafanya biashara hiyo na kisha kuanza kunywa pombe hiyo haramu hadi kukutwa na umauti papo papo.

Habari hizo zinaeleza kuwa marehemu ambaye enzi za uhai wake alikuwa kada wa chama hicho siku hiyo alionekana kuwa na furaha ya ushindi mara baada ya chama chake kutangazwa kushinda ndipo alipoamua kwenda kufakamia kinywaji hicho kwa majigambo kuwa amefurahi kushinda kwa mgombea wao.

Wakazi wa kata hiyo mara baada ya kumwona mwenzao amezidiwa kwa kinywaji hicho kutokana na kuanguka chini kwa kuzimia walianza kumwagia maji ya baridi huku wakimpepea lakini baada ya muda mfupi aliaga dunia.

Ilielezwa kuwa marehemu Petro alikuwa na kawaida ya kunywa pombe, lakini akuwahi kulewa sana kama ilivyotokea siku hiyo ambayo alikuwa akisherehekea ushindi wa chama chake hicho alichokuwa akikiunga mkono pamoja na kuwa na uanachama wa muda mrefu.

Mbunge wa jimbo la Maswa John Shibuda alithibitisha kutokea kwa kifo hicho cha mwanachama wa CCM na kuongeza kuwa hali hiyo ilimtokea wakati akishangilia ushindi wa mgombea wa CCM.

Hebu cheki hapa jumba limebomolewa


Kalikuwa kaugomvi kadogo pale Mbezi katika ya Miliki mmoja na mwingine, na hatimaye aliyewahi akajenda, kuona hivyo yule aliyechelewa akaona hakuwa na ujanja kwa maana hiyo akaamua kuibomoa nyumba ya mwenziua kwa kutumia tinga tinga la kukodi huku akijifanya kuwatumia maafisa wa usalama wa taifa. Cheki hasara washikaji msijenge maeneo unplanned.

Jenerali Ulimwengu ajiengua Habari Corporation

ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Habari Corperation, Jenerali Ulimwengu amejitoa katika kampuni hiyo na kuanzisha gazeti lake lingine.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ulimwengu alisema wamejitoa katika kampuni hiyo kwa sababu za kibiashara na kwamba gazeti hilo la wiki litajulikana kama ‘Raia Mwema’.

“Sababu za kibishara zimefanya kujitoa Habari Corporation,” alisema Ulimwengu.

Alisema gazeti hilo litaanza kutoka kesho na litaendeshwa na kusimamiwa na waandishi, John Bwire, Johnson Mbwambo, Mbaraka Islam, Francis Chirwa na Shaban Kanua.

“Gazeti hili halina uhusiano wowote na Habari Corporation, tumeuza hisa zetu na tumeona tuanzishe gazeti lingine, nguvu zetu zote zitaelekezwa katika gazeti hilo na tutakuwa makini,” alisema Ulimwengu.

Alisema gazeti hilo likizingatia maadili ya taaluma ya uandishi wa habari na kwamba litasomwa Tanzania na Afrika Mashariki yote.

Ulimwengu alisema pamoja na Tanzania kupiga hatua kubwa katika sekta ya habari, bado mchango unahitajika ili kuendeleza sekta hiyo nchini.

Alitoa wito kwa vijana nchini kujitokeza na kuanzisha vyombo vya habari kwani bado kuna nafasi ya kuueleza umma mambo mbalimbali yanayotokea nchini na duniani kwa ujumla.

Ulimwengu alisema gazeti hilo, litakuwa likitoka mara moja kila wiki na litakuwa likiandika habari za kisiasa na michezo.

Alisema kuwa gazeti hilo halijaanzishwa kwaajili ya kuishambulia serikali na kwamba litakuwa likiandika makala na habari za kuisifia au kuikoa serikali pale inapostahili.

“Tunataka tutoe mchango wetu katika jamii kwaajili ya maendeleo ya nchi yangu na wala hatuanzishi ‘Raia Mwema’ ili kuziba mapengo ya uandishi,” alisema Ulimwengu.

Monday, October 29, 2007

Barrick Gold Tanania yatimua wafanyakazi 900

Kampuni ya Barrick Gold Tanzania leo imetangaza rasmi kuwa imewasimamisha kazi wafanyakazi takribani 900 katika mgodi wa wa Bulyanhulu uliopo Wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga na siyo 700 kama ilivyokuwa .

Wafanyakaazi walioathirika na kusimamishwa kazi ni wale waliojisusisha na mgomo batili ulioitishwa na Chama cha Wafanyakazi wa Migodi na Ujenzi (TAMICO) jioni ya tarehe 24,October,2007.

Menejimenti ya mgodi wa Bulyanhulu imetoa taarifa kwa wafanyakazi wote ikiwaataarifu kuwa, wafanyakazi wote walioshindwa kurudi kazini kama walivyoagizwa wamesimamiswa kazi na nafasi zao zitatangazwa upya.

Menejimenti pia imefafanua kuwa waajiriwa wote wa hapo awali hawatabaguliwa kwa namna yeyote na kwamba kila mmoja anayo haki ya kuomba kazi kwa nafasi zitakazo tangazwa upya. habari zaidi soma hapa hebu mchekini Teweli Teweli anasemaje ili mpate taarifa zaidi.

Jamani mama na watoto wazuri, baba hataki


Jamami hebu chekini binti mrembo watoto wazuri, lakini baba wa watoto hawataki, amewakimbia Binti huyu mkazi wa jijini Dar es Salaam, Tunu Mrisho (28), anaomba msaada wa matunzo ya watoto wake mapacha watatu baada ya mwanaume anayedai kuzaa naye kukataa kuhusika kumpa ujauzito wa watoto hao.

Tunu ambaye anaishi Kigogo First Inn kwa dada yake, Zubeda Hamisi, anadai kuwa mwanaume huyo (jina tunalo), mkazi wa kijiji cha Matombo, mkoani Morogoro, alikataa kuhusika kumpa ujauzito huo tangu ulipokuwa wa miezi mitano.

"Kabla ya hapo, (baba ya mapacha hao) alikuwa akifika nyumbani kama kawaida. Nilipobainika kuwa nina mimba ya miezi mitano, nilimweleza. Kufanya hivyo, akaacha kufika nyumbani na kuanzia siku hiyo sijamwona tena hadi sasa," alisema Tunu.

Akizungumza katika ofisi za Mwananchi Jumamosi wiki iliyopita, Tunu alisema mwanaume huyo alikataa kuhusika na suala hilo kwa maandishi mbele ya balozi wa nyumba kumi, kijijini hapo

Waziri Simba


WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba (Pichani kitandani) ambaye amelazwa katika Hospitali ya Hindu Mandal anaendelea vizuri.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili hospitalini hapo, Simba alisema hali yake ilikuwa imeimarika kuliko ilivyokuwa juzi.

"Mimi ni mzima, afya yangu inaendelea vema," Waziri Simba aliwaambia waandishi wa gazeti hili mara tu walipoingia katika wodi alipolazwa.

Kauli ya Simba ilionyesha kutokana na kuwepo watu wengi waliofika kumjulia hali siku ya jana. Watu hao walifika ikiwa ni pamoja na taarifa za vyombo vya habari kuwa, hakuweza kuhudhuria mazishi ya Naibu Waziri wake Salome Mbatia kutokana na ugonjwa.

Baadhi ya Mawaziri waliofika hospitalini hapo kumjulia hali ni Zakia Meghji na Mary Nagu ambao walifika majira ya jioni.

Wengine waliokuwepo ni wanafamilia ambao pia walitakiwa kuondoka nje ya chumba alimolazwa kutokana na chumba hicho kuwa na wageni wengi hali iliyosababisha kukosa hewa kwa mgonjwa.

Safari ya mwisho ya Mbatia









Safari ya mwisho duniani ya Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Salome Mbatia ilivyohitimishwa katika makaburi ya Kanisa Katoliki Parokia ya Mbokomu na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji. Picha kwa hisani ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Friday, October 26, 2007

uwanjani Kilimanjaro

Kijana wa kiume wa mama mbatia akisindikizwa na baadhidhi ya Waombolezaji wakitoka katika uwanja wa KIA baada ya kuupokea mwili wa Salome Mbatia picha ya mdau Ally Sonda wa Moshi.

Msafara wa hayati Mbatia KIA


Magari yaliyobeba mwili marehemu Mbatia yakitoka katika uwanja wa KIA baada ya kuupokea mwili wa
Salome Mbatia picha ya mdau Ally Sonda.

Salome Kilimanjaro


Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa Salome Mbatia ulipowasili katika uwanja wa Kilimanjaro International Airport (KIA) leo mchana picha katuletea mdau Ally Sonda

pole sana


Rais Jakaya Kikwete akimpa pole mtoto wa Marehemu Mbatia.


Baadhi ya mawaziri wakiupokea jeneza lililobeba mwili wa hayati salome mbatia uwanja wa ndege wa julius nyerere dar, jana kufuatia ajali mbaya ya barabarani ambapo watu watatu walikufa papo hapo. habari toka iringa zinasema dereva wa lori la fuso lililoigonga nissan ya hayati mbatia hakufa na aliyekufa ni utingo wake. yeye dereva ametoweka na bado hajulikani aliko. Picha ya mpoki Bukuku. hebu mchekini HAPA ili mpate picha nyingi na kiboko zaidi.

Thursday, October 25, 2007

Waziri Salome Mbatia afariki dunia



Wasamaria wema wakimchomoa dereva

Mama Mbatia



Eneo la Ajali


PICHA HIZI ZIMEPIGWA NA ZITTO KABWE

Na Waandishi Wetu, Dar, Iringa

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bibi Salome Mbatia, amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana saa 10: 45 eneo la Kibena Factory wilayani Njombe
mkoani Iringa.

Akithibitisha kutokea kifo hicho kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Dkt. David Mathayo, alisema marehemu Mbatia alikumbwa na mkasa huo akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Njombe, akiwa katika gari lake binafsi, Nissan Patrol namba T 724 AGZ.

"Tupo hapa tunajaribu kukata bati tuwatoe, ni kweli wamekufa alikuwa kwenye gari lake binafsi, Nissan Patrol yeye na dereva wake, "alisema Dkt. Mathayo. Alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya lori aina ya Mitsubishi Fusso lenye namba T 299

AFJ lililokuwa likitoka Njombe kwenda Makambako kuhama njia yakena kugongana uso kwa uso na gari la waziri huyo.

Wednesday, October 24, 2007

Gwiji la mapicha amerejea

Nadhani bila shaka mtakuwa mkijiuliza hivi huyu Mpoki Bukuku, Mwandishi wa habari mwandamizi na mpiga picha wa siku nyingi yupo wapi?, msihofu bwana huyu jama a yupo na leo kanambia kwamba amerejea full mass nondo na akanipa salamu niwaambieni kina Haki Ngowi, Jeff Msangi, Muhidin Michuzi, Freddy Macha, na wengine kibao maana nikianza kuwataja wote hapa patakuwa hapatoshi, by the way karejea hebu mchekini HAPA ili mpate picha nyingi na kiboko zaidi.

Wahadzabe walia njaa, wamkumbuka Nyerere



WAHADZABE wanaoishi katika Bonde la Yaeda chini, wilayani Mbulu, Mkoa wa Manyara wanakabiliwa na njaa hivyo maisha yao kuwa hatarini.
 
Wakizungumza na waandishi wa habari na ujumbe wa viongozi wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) juzi katika Kijiji cha Sanora, wilayani hapa, Wahazdabe hao walisema kutokana na njaa kali na kukosekana kwa huduma muhimu za kijamii, watoto wao wamekumbwa na magonjwa ya kuharisha na kutapika.
 
Wakizungumza kwa shida huku baadhi yao wananchi hao walimkumbuka hayati Mwalimu Julius Nyerere, ambaye walisema alikuwa akiwapatia chakula na kwamba aliwahi kuwatembelea.

Walisema wanaamini kama Nyerere angekuwa hai wasingekuwa kwenye taabu ambayo wanaipata kwa sasa.
 
Mmoja wa wananchi hao, Tale Mudenda, alisema hivi sasa wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula katika jamii hiyo baada ya kupungua kwa wanyama kutokana na eneo lao kuvamiwa na wafugaji na kusitishwa kwa huduma za kitalii katika bonde hilo.

Tuesday, October 23, 2007

Karamagi asaini Buzwagi nyingine



SERIKALI imesaini mkataba wa miaka kumi na moja na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbon&Power (Tanzania) Limited ya Dubai ili kufanya utafiti wa mafuta katika Bonde la mto Ruvu.

Mkataba huo ulisainiwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Hasu Masrani.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini mkataba huo, Waziri Karamagi alisema kuwa awamu ya kwanza ya zoezi hilo itakayodumu kwa kipindi cha miaka minne itatumia dola za kimarekani 31.5milioni ambazo ni sawa na Sh34.7 bilioni. (Dola moja ya Kimarekani sasa inabadilishwa kwa Sh1,100)

“Mkataba huu ni wa miaka kumi na moja na Mkandarasi Dodsal anatarajiwa kutumia kiasi kisichopungua dola za Marekani 31.5milioni,” alisema Karamagi. kwa habari zaidi soma Mwananchi.

Gazeti jipya mtaani



Nimepata ujumbe ufuatao:-

Gazeti jipya kabisa la Kiswahili linatarajiwa kuingia katika vibanda, maofisi, na mitaa ya Tanzania kuanzia tarehe 31 Oktoba mwaka huu. Jarida hilo la "Raia Mwema" litakuwa na habari mbalimbali zikiwemo za uchunguzi, utafiti, siasa, biashara, maoni n.k Jarida hilo liitwalo "Raia Mwema" limeanzishwa kutokana michango ya hali, mali, na vipaji ambavyo vimekusanywa chini ya Mhariri wake Mtendaji John Bwire

Kuanzishwa kwa jarida hilo ni alama ya kuvunjika rasmi kwa ndoa ya gazeti lililosifika sana nchini miaka hiyo la "Rai".
Waandishi waanzilishi wa gazeti la Rai - ukiondoa Dr. Shoo na Salva - na waandishi wengine ndani na nje ya Tanzania wamefikia uamuzi wa kuanzisha gazeti hilo wakizingatia haja ya kupanua uhuru wa maoni, habari na mawazo na kuchangia kwa namna ya pekee kuhamasisha kizazi kipya cha "Raia Wema". Gazeti hilo litakuwa linatolewa kila wiki. Angalia mfano wake hapa: http://www.akili.biz/raiamwema/

Gazeti hilo litajumuisha waandishi mbalimbali wakiwemo:

Jenerali Ulimwengu
Issa Shivji
Padre Karugendo
Prof. Haroub Othman
Maggid Mjenga
Joseph Mihangwa

Na wenu mtiifu, na wengine wengi ambao mtapata bahati ya kusoma kazi zao kwenye gazeti hilo ambalo litapatikana pia kwenye mtandao wakati huo.

Napenda kutoa pongezi kwa ushirikiano wote wa wale ambao wamewezesha gazeti hili kupata mtaji, kibali, na nyenzo za kutendea kazi.. Natarajia kuwa toleo la kwanza litaiweka fani ya uandishi katika ngazi nyingine kabisa nchini.


Tafadhali copy na watumie wabongo walioko kwenye orodha yako ya anuani.

Ndugu yenu,

M. M.

Ofunneka, Maureen and Tatiana are up for eviction

Tatiana decides not to save herself from possible eviction. She refuses to replace herself with Richard, according to her "Richard has been up many times."

How they nominated

Richard nominates Maureen and Ofunneka. He says Maureen is having problems with getting attention in the House. As regards Ofunneka, Richard says he cannot nominate Tatiana, though Ofunneka is her friend.

Ofunneka puts up Richard and Tatiana because there are few Housemates left in the House. She nominates Tatiana because, as the Head of House, she will be able to save herself from possible eviction.

Maureen nominates Ofunneka and Tatiana. She says that Ofunneka has changed towards her and Tatiana will be able to save herself.

Tatiana puts up Ofunneka and Maureen. She simply says she cannot nominate Richard.

To see the Housemate you want evicted from the House, vote here.

What you think of Tatiana's decision: Wonderful gesture of love or cynical act of gamesmanship? Get to our forum and share your thoughts. Soma HAPA upate taarifa zaidi za BBA II.

Monday, October 22, 2007

Chissano anyakua tuzo ya Mo Ibrahim


RAIS mstaafu wa Msumbiji Joaqium Chissano, amewabwaga Marais wengine 12 akiwemo Benjamin Mkapa wa Tanzania, katika kinyang'anyiro cha Tuzo ya Rais bora wa Afrika.

Ushindi wa Chissano umetangazwa mjini London jana na Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa (UN), Kofi Annan.

Tuzo hiyo ambayo imetolewa na Taasisi ya Mohamed Ibrahim, bilionea mzaliwa wa Sudan, msingi wake ni mambo matatu, Kukuza Demokrasi, Utawala Bora na Maendeleo katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Soma HAPA upate taarifa zaidi za kiongozi huyu wa Msumbiji.

Richard ayakaribia mamilioni ya BBA II



Mwakilishi Wetu katika jumba la Big Brother anaendelea kutesa tu na hii ni mara ya tano tangu wampendekeze kutoka, lakini wameshindwa richard bado amebakia ndani ya jumba la big brother na Code wa Malawi kuchomolewa bila shaka huenda huyu jamaa akanyakua dhawadi jamani hebu tuendeleeni kuwa-vote out washamba wengine ndani ya nyumba tubaki na Rich tuuuuu

habari kamili za kutolewa nishai kwa code Soma HAPA upate taarifa zaidi

Bwagamoyo



Angalau hawa jamaaa wqanajitahidi kufanya mambo, bongo siku hizi ukitaka kupumzika unachum tu maeneo haya unapata utulivu wa nguvu mzeee. Hapa ni Oceanic Bay.

Safari ya Zanzibar



Nje kidogo ya bandari.

Zanzibar



Nambieni hapa ni wapi?

Safari na muziki


Hapa ni karibu kidogo ba bandari ya Zanzibar.

Saturday, October 20, 2007

Ndesamburo amtaka kikwete kuvunja baraza la mawaziri

Na Ally Sonda, Moshi wa Mwananchi

MBUNGE wa Moshi Mjini (CHADEMA) , Phillemon Ndesamburo amemuomba Rais Jakaya Kikwete kuvunja Baraza la Mawaziri na kuendesha nchi kwa kuwatumia Makatibu wakuu wa wizara,ili kutoa nafasi ya kuunda serikali yake upya.

Mbunge huyo alitoa ombi hilo jana wakati akihojiwa na Mwananchi,nyumbani kwake mtaa wa Mbokomu mjini hapa Mkoa wa Kilimanjaro wakati akizungumzia tuhuma za ufisadi dhidi ya viongozi wa serikali.

Ndesamburo aliwashambulia Jaji Joseph Warioba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Siasa), Kingunge Ngombale Mwiru kwa madai kuwa kauli zao zinatetea ufisadi nchini.

mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Kilimanjaro, aliwataka Warioba na Kingunge kuondoa laana katika makaburi yao pindi watakapokufa kutokana na kutetea udhalimu uliofanywa na baadhi ya vigogo wa serikali kwa kuitia hasara nchi wakati wananchi wengi ni maskini.

Akizungumzia uimara wa Serikali ya Kikwete, Ndesamburo, alisema imepwaya kutokana na viongozi wake muhimu kutuhumiwa kwa rushwa na kushindwa kuwachukulia hatua za kinidhamu dhidi yao.

Alionya kama Kikwete hatavunja Baraza la Mawaziri waliotajwa kwenye kashfa ya ufisadi na a na kufanya kazi na makatibu wakuu, nchi inaweza kuingia kwenye vurugu.

Vilevile alitakawote waliotajwa kuhusika na rushwa za mikataba ya madini na zile za ulaji wa mabilioni ya fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kuchunguzwa na taasisi binafsi, zikiwemo za kimataifa.

Kwa upande mwingine, alisema kitendo cha Kikwete kuacha kuzunguzia suala la ufisadi na kuamua kusafiri nje ya nchi ni kielelezo tosha kuwa, anaogopa kuwachukulia hatua za kinidhamu waliotajwa kuhusiana nao.

Alisema Kikwete anapaswa kuheshimu kauli na mawazo yaliyotolewa na viongozi waandamizi waliowahi kuingoza Tanzania kama vile Alli Hassan Mwinyi, Dk Salim Ahmed Salim, Jaji Paul Bomani na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, John Malecela.

Alisema Watanzania wakiwamo viongozi wa vyama vya upinzani wanamuombea kila la kheri na afya njema Kikwete ili aweze kuongoza nchi kwa amani na utulivu hadi mwaka 2010.

Friday, October 19, 2007

Magari ya Zimamoto feki

Magari mawili ambayo yalinunuliwa na mwaka 2005 na Jiji la Dar es Salaam kwa zaidi ya Sh350 milioni yameshindwa kufanya kazi kutokana na kutopata usajili mpaka sasa.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Muandamizi wa Zimamoto, Fikiri Salla kuwa kwa sasa kikosi hicho kina magari mawili tu yanayofanya kazi kati ya magari tisa yaliyopo.

"Hadi leo magari hayo hayajaanza kufanya kazi kutokana na malumbano yaliyopo kati ya Wizara ya Miundombinu na Manispaa ya Temeke, pamoja na ucheleweshwaji katika usajili wa gari la zimamoto la Manispaa ya Ilala.

Waandishi walishuhudia magari hayo yakiwa yameegeshwa katika makao Makuu ya kikosi hiho, huku moja likiwa halina namba na lingine likitumia namba injini (chasis nunmber)

Awali Mkuu wa Chuo hicho, Kamishina Msaidizi Omary Mrisi, alisema licha ya kupokea maombi kutoka nchi mbalimbali ya kujiunga na chuo hicho wameshindwa kuwapokea kutokana na uduni ya vitendea kazi.

Awali Kamati ya ya Ulinzi na Usalama ya Bunge iliyotembelea kikosi hicho imesema hali ya Kikosi cha Zimamoto nchini kimeshindwa kufanya kazi katika viwango vinavyostahili na kwamba hata chuo chake kikachotoa mafunzo ya zimamoto hakina hadhi.

Wabunge hao walisema hayo jana kamati hiyo ilipotembelea Makao Makuu ya kikosi hicho pamoja na Chuo cha Zimamoto ili kujionea shughuli zinazofanywa na kikosi hicho.

Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, na Mbunge wa Newala, Kapteni Goerge Mkuchika (CCM), alisema kuwa ni aibu kwa kikosi hicho kinachohudumia Jiji linalokadiriwa kuwa na watu milioni 3.5 kuwa na magari mabovu yasiyo na uwezo wa kutoa huduma hiyo.

Mkuchika alisema hayo kufuatia taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam iliyosomwa kwa niaba yake na Afisa Muandamizi wa Zimamoto, Fikiri Salla kuwa kwa sasa kikosi hicho kina magari mawili tu yanayofanya kazi kati ya magari tisa yaliyopo.

Nyumba ya Mbunge yachomwa moto

Na Muhibu Said wa Mwananchi

MVUTANO wa bei ya korosho, mkoani Mtwara, umechukua sura mpya, baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni wakulima katika Wilaya ya Tandahimba, kuichoma moto nyumba ya Mbunge wa Jimbo hilo, Juma Njwayo, wakipinga kuuza zao hilo kwa mkopo.

Vilevile watu hao wameripotiwa kukata mikorosho kadhaa, ikiwamo mikorosho zaidi ya 25 inayomilikiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima Tandahimba (TAFA), Adinani Mbwana.

Mbali na hujuma hizo, watu hao pia wameripotiwa kuchinja mifugo mbalimbali ikiwamo bata, kuku na mbuzi wa dereva wa mkuu wa wilaya na kufunga kwa kufuli maghala yote ya vyama vya msingi vya ushirika wilayani humo yanayotumika kuhifadhi na kuuzia korosho.

Habari kutoka Tandahimba zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Miti Francis, zinaeleza kuwa hujuma hizo zimefanyika siku chache baada ya wakulima wa zao hilo kufanya maandamano makubwa hivi karibuni kupinga suala hilo. Soma GAZETI LA MWANANCHI upate taarifa zaidi.

Papa Benedict 16 kuja bongo



KIONGOZI wa Kanisa Katoliki duniani Baba Mtakatifu, Papa Benedict 16, amekubali mwaliko wa Rais Jakaya Kikwete kuitembelea Tanzania katika ziara yake anayotarajia kuifanya hivi karibuni katika nchi za bara la Afrika.

Rais Kikwete alitoa mwaliko huo jana wakati wa mazungumzo yake na Baba Mtakatifu yaliyofanyika katika maktaba yake iliyoko katika Makao Makuu ya Kanisa Katoliki, Vatican, Italia.

Akizungumza katika mkutano huo Papa Benedict 16 alisema ataitembelea Tanzania katika ziara yake hiyo ili kuendeleza uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili ulioanza tangu enzi za uhai wa baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

"Tanzania tunaipa umuhimu wa pekee, ni nchi ambayo haina matatizo ya watu kugombana kwa sababu ya tofauti ya dini au rangi zao, ninafurahishwa sana na hali ya watu kuishi kwa pamoja na kwa amani na ninakupongeza kwa kuendeleza hali hii, hili ni jambo linalonifurahisha. Nitaendelea kuiombea Tanzania ili iendelee kuwa nchi ya amani," alisema Baba Mtakatifu huyo.

Mbali na kukubali wito huo Baba Mtakatifu alimwahidi rais Kikwete kuwa Kanisa Katoliki Duniani litaendelea kuisadia Tanzania kwa kuchangia huduma muhimu za maendeleo bila kujali tofauti za dini baina ya wananchi.

Alisema Tanzania ni nchi ambayo inahitaji msaada hasa katika upatikanaji wa elimu kwa wananchi ili kuwawezesha kukabiliana na janga la ukimwi kwa ufanisi.

Rais Kikwete alipata fursa ya kuzungumza na Baba Mtakatifu huyo kwa mwaliko wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kimataifa wa madhehebu mbalimbnali ya dini duniani katika mkutano uliofanyika Napoli.

Akazungumza katika mkutano huo Baba Mtakatifu alimpongeza Rais Kikwete kwa kuendeleza amani na utulivu nchini Tanzania

Aliisifia Tanzania kwa kuendelea kuwa kama ilivyo kwa kuwa viongozi wake wameendelea na kuienzi misingi mizuri ya uongozi ambayo iliasisiswa na hayati Mwalimu Nyerere.

amka mzee mkapaaaaa

Wednesday, October 17, 2007

Mahakama yamwachia huru Lwakatare

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kagera imemwachia huru Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Wilfred Lwakatale, katika shtaka lililokuwa likimkabili la kumshambulia na kumjeruhi Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Renatus Mutabuzi, kwa sharti la kutotenda kosa lolote la jinai ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu wa Mkazi wa mahakama hiyo, Cleophace Waane, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashtaka na kwa kuzingatia maombi ya wakili wa mshtakiwa huyo, Twaha Tasilima, yaliyotolewa kabla ya hukumu hiyo kutolewa.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Waane alisema kuwa mahakama imeona baadhi ya maombi yaliyoombwa na wakili wa mshtakiwa ambayo aliomba yazingatiwe na mahakama wakati wa kutoa hukumu ni ya muhimu, hivyo kuamua kutoa adhabu ndogo kwa mshtakiwa huyo. Bonyeza GAZETI LA MWANANCHI upate taarifa zaidi.

'Sekta ya madini haijasaidia Tanzania'

TANZANIA licha ya kuwa na utajiri wa madini bado imeshindwa kunufaika kwa kiwango kikubwa, kutokana na kukosekana mipango iliyowazi katika kudhibiti sekta hiyo.

Akitoa tathimini kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emanuel Ole Naiko, juu ya Ripoti ya Uwekezaji ya Dunia ya mwaka 2007, Mkurugenzi wa Utafiti na Mawasiliano wa kituo hicho, John Kyaruzi, alisema ipo haja ya kufanyika kazi ya ziada kuona madini yanatumika kupunguza umasikini kwa Watanzania.

Kyaruzi alifafanua kwamba baadhi ya makampuni yanayochimba madini yamekuwa na ajenda zao za kibiashara na kwamba kazi kubwa kwa serikali ni kutokubaliana na mambo yasiyo na manufaa kwa nchi.

Alifafanua kwamba, sekta ya madini imekuwa ikitarajiwa kufungua milango zaidi ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) na kusaidia nchi zenye utajiri huo kuendelea, lakini kwa Tanzania bado haijafanya vizuri hasa katika mipango.
Bonyeza GAZETI LA MWANANCHI upate taarifa zaidi.

Tuesday, October 16, 2007

Jakaya: Freedom from hunger is 'basic human right'



Speaking at Tuesday's ceremony, Tanzanian President Jakaya Mrisho Kikwete said that in sub-Saharan Africa, which along with southern Asia suffers the brunt of the scourge of hunger, "we see some light at the end of the tunnel."

But in order to "consign hunger to history" in Africa, the continent needs a "green revolution" involving a major increase in irrigation-based agriculture, widely available and affordable higher-yielding seeds and other inputs, he said.

"All countries are capable of guaranteeing the right to food to their people," Kikwete said. "However, for most of our people in the South this will be possible only by revolutionising our agricultural production."

He added: "All that is required is the reliability ... on the part of the donors to support and complement our efforts."

The FAO laments that despite the 1996 World Food Summit's pledge to reduce the number of undernourished people by half by 2015, the number of hungry people continues to rise.

"Keeping the summit pledge would require reducing the number of undernourished by 31 million every year until 2015, whereas the number of hungry is currently climbing at the rate of some four million a year," the FAO said when it released the 2006 report on the state of world food insecurity.

Developing countries reduced the overall number of undernourished by three million to 820 million from the baseline period of 1990-92. But that figure was reduced by 100 million in the 1980s and 37 million in the previous decade, the FAO noted.
"40,000 children die every day throughout the world due to malnutrition and related diseases. These are the people who are being denied the right to food. These are the people who are the subject of this year's World Food Day," Tanzanian Jakaya Mrisho Kikwete said in his speech.

Aliyejenga hifadhi ya barabara kulipwa Sh15 bilioni

MAHAKAMA imeiamuru Serikali kuilipa kampuni ya Mansoor Oil Industries Ltd (MOIL) ya jijini Mwanza jumla ya Sh14.7bilioni
kutokana na uamuzi uliotolewa na Waziri wa Ujenzi wakati huo John Pombe Magufuli wa kuvunja kituo cha mafuta cha kampuni hiyo.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi ya madai namba 2 ya mwaka 2002 ambapo
kampuni hiyo ilikuwa ikiwashitaki Waziri Magufuli, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (wakati
huo) Brigedia Hassani Ngwilizi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Andrew Chenge pamoja na Halmashauri ya Jiji
la Mwanza.

Katika kesi hiyo madai ya kampuni hiyo ya MOIL kwa serikali yalikuwa jumla ya Sh.18bilioni kutokana na kuvunjiwa kituo hicho cha mafuta kilichokuwa kimejengwa katika kiwanja namba 178 Kitalu ‘A’ eneo la Kirumba kando ya barabara ya Makongoro.

Katika madai hayo, kampuni hiyo iliomba kulipwa kiasi cha Sh 593milioni kama thamani ya jengo ambalo lilibomolewa kwa amri ya Waziri Magufuli, Sh13.4 bilioni ikiwa ni kiasi cha faida ambacho ingekipata katika kipindi cha miaka 33 ambacho ilitarajiwa kufanya biashara na Sh 4 bilioni kama hasara ya jumla ya mradi huo. kwa taarifa zaidi soma Mwananchi

Balozi wa Uholanzi anusurika ajalini



BALOZI wa Uholanzi nchini, Karel van Keresteren, amenusurika kwenye ajali ya gari iliyotokea mkoani Morogoro, Jumamosi wiki iliyopita baada ya gari yake kugongwa na lori la mizigo.

Balozi huyo pamoja na mkewe walikuwa njiani kuelekea mjini Morogoro ndipo walipopata ajali hiyo iliyotokea wakiwa karibu kufika mjini humo na kimsababishia Balozi Keresteren maumivu ya viungo.

Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Uchumi na Biashara kwenye ubalozi wa nchi hiyo, Steef van den Berg, alisema balozi huyo alipata ajali hiyo Jumamosi majira ya saa saba mchana.

Alisema ajali hiyo ilitokea baada ya gari alilokuwa akisafiria balozi huyo kupita kwenye kizuizi cha Polisi wa Usalama Barabarani, ambapo lori hilo ambalo pia liliruhusiwa lililigonga kwa nyuma na kumsababishia mshituko katika baadhi ya maeneo ya mwili wake. Kwa taarifa zaidi soma Mwananchi

Monday, October 15, 2007

Mwamunyange awavisha vyeo makamanda JWTZ

Na Kizitto Noya

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange, amewavisha vyeo vipya maafisa wakuu 19 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopandishwa vyeo mwishoni mwa wiki iliyopita na Rais Jakaya Kikwete.

Jenerali Mwamunyange aliwavisha vyeo hivyo jana na kuwapangia nyadhifa mpya maafisa wanane kati yao katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Waliopangiwa nyadhifa mpya ni Meja Jenerali Wyanjones Kisamba, aliyekuwa Kamanda wa Brigedi ya Kaskazini Arusha, ambaye sasa anakuwa mkuu wa kwanza wa Kamandi mpya ya Majeshi ya Nchi Kavu ambayo imeundwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa JWTZ mwaka 1964.

Kabla ya kuundwa kwa kamandi hiyo ,JWTZ ilikuwa na komandi mbili ambazo ni Navy, kwa ajili ya vikosi vya maji, Kamandi ya Ulinzi wa Anga kwa ajili ya vikosi vya Anga na brigedi za vikosi vya nchi Kavu.

Kamandi mpya iliyoundwa itaunganisha brigedi zote za askari wa miguu pamoja na vikosi vya vifaru, mizinga na uhandisi wa medani.

Maafisa wengine waliopangiwa nyadhifa mpya ni aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanawake Jeshini, Meja Jenerali Zawadi Madawili ambaye sasa ni Mkuu wa tawi la Mgambo, Brigedia Jenerali Vicent Mritaba anayekuwa Kamanda wa Brigedi ya Magharibi Tabora na Brigedia Jenerali Charles Kitenga aliyeteuliwa kuwa Kamanda wa Brigedi ya Kaskazini badala ya Meja Jenerali Kisamba.

Wengine ni Brigedia Jenerali Patrick Mlowezi aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Shule ya Huduma Pangawe, Brigedia Jenerali Charles Mzanila anayekuwa Meneja Mkuu wa kiwanda cha mazao Morogoro, Brigedia Jenerali Lilian Kingazi kuwa Mkurugenzi wa Utumishi jeshini na Brigedia Jenerali Grace Mwakipunda kuwa Mkurugenzi wa Musuala ya wanawake jeshini.

Maafisa wakuu waliobaki ambao wanaendelea na nyadhifa zao za awali ni Msemaji wa Wizara ya Ulinzi na JKT, Meja Jenerali Alfred Mbowe, Kamanda wa Brigedi ya Mashariki, Dar es Salaam, Meja Jenerali Servas Hinda na Mabrigedia Jenerali Kelvin Msemwa, Albert Kigadye, Sebastian Chiwangu, DAniel Igoti, Salum Kijuu, Farrah Mohamed, Gerald Kiswaga, Julius Mbilinyi na Mabula Mashauri.

Chuo Kikuu cha Ardhi



Unapoingia katika lango la kuelekea Chuo Kikuu cha Ardhi zamani UCLAS mambo yako hivi, jamani bongo siku hizi watu wanakata nyanga hawana mfano yaani ni elimu kwa kwenda mbele watru washashitukia ujinga picha hii kwa niaba ya mdau wangu Faraja Jube.

Jiji la Mwanza



Hivi vichuguu ndani ya ziwa nadhani bila shaka mnavifahamu vimepigwa picha na mdau wangu mmoja kwa mbaali unaweza kuona jiji la mwanza.

vimbwete



Hivi vijiwe vinajulikana kama vimbwete vipo pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na vinasambaa kwa kasi kila chuo kikuu, hebu nambieni hivi tunakwenda wapi, hapa ni chuo kikuu cha ardhi.

Saturday, October 13, 2007

Eid Mubaraka



Jamani wadau nawatakieni Eid mubarak kokote mlipo duniani

Pwani ya Kilwa



Hebu cheki ilivyo mwanana, hivi ni pwani ngapi za hapa nchini ambazo ni safi na mwanana kama hivi

Idd el Fitr


waislamu wakiswali swala ya Idd katika viwanja vya Jangwani juzi.

Thursday, October 11, 2007

Mwalimu Nyerere



Mwalimu Nyerere aligoma kuchongewa sanamu hebu cheki hii hapa.

Maamuzi Mazito CCM


Leo mchana kamati kuu ya halmashauri kuu imetoa maamuzi mazito manne, mojawapo likiwa ni kuwatosa wale wabunge watuhumiwa wa Arusha na kisha kuanza mchakato mpya wa kuwasaka wasafi, wamezungumza mengi stay tuned.

Futari


Makamu wa Rais Dk Alli Mohammed Shein ( wa pili kushoto) akishiriki futari aliyowaandalia wananchi wa Dar es Salaam nyumbani kwake Oysterbay jana. Wa kwanza kushoto ni Waziri Mkuu Edward Lowassa. Picha ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

Rais Kikwete Nyumbani



Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na mtoto yatima mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, Mohammed ambaye anamlea nyumbani kwake Ikulu baada ya kutupwa na mama yake baada ya kuzaliwa. Mama Salma alimchukua mtoto huyo katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mburahati jijini Dar es Salaam. Picha ya Ikulu.

Wednesday, October 10, 2007

Rais Kikwete azungumzia tuhuma za ufisadi

Rais Jakaya Kikwete ameonya tabia inayotaka kujengeka miongoni mwa wananchi na hususani wanasiasa ya kugeuka kuwa wapelelezi, wakamataji, waendesha mashtaka na watoa hukumu, na tena wakizitoa huku hizo bila ya watuhumiwa kuwapo.

Amesema tabia hiyo ikiachwa kuendelea siyo tu itaipeleka nchi pabaya, lakini itawatisha wananchi, itawatia hofu na kujenga chuki kati ya mtu na mtu hali ambayo amesema haiendani na taratibu za kuendesha nchi kwa misingi ya kufuata kanuni, taratibu, na sheria za nchi.

Amebainisha kwamba tabia hiyo ya wanasiasa kujigeuza kuwa wao ndio wapelelezi, wakamataji, waendesha mashtaka na watoa hukumu kuwa haimtendei haki mtuhumiwa ambaye naye ana haki yake ya msingi ya kulindwa kwa mujibu wa sheria za nchi.

Rais Kikwete ameeleza kuwa kila taarifa inayohusu rushwa au tuhumu za mtu kutuhumiwa kuhusika na vitendo vya rushwa, zitachunguzwa kwa kuzingatia misingi ya sheria za nchi na vyombo vinavyohusika na si vinginevyo na kuongeza kwamba yeyote atakayethibitishwa na mamlaka halali kwamba ama ametoa rushwa au kupokea rushwa atachukuliwa hatua za kisheria bila ya kujali nafasi na madaraka aliyonayo. ukitaka kusoma zaidi cheki TAARIFA YA IKULU HAPA

Chuo Kikuu leo



Mazingira ya Chuo kikuu leo hapa ni maeneo ya pale utawala wadau mnasemaje.

Tuesday, October 09, 2007

Jijini Dar es Salaam

 

This is what baba Zakaria's (Benjamin Thomson camera got into during his Dar Zanzibar Dar Flight this week.

Stay tuned for more next week



Jamani changamkieni fursa Marekani

Jamani changamkieni tenda hiyo nafasi kibaoo zaidi ya 200 kwa Watanzania kwenda Marekani kufanya kazi na kuishi huwezi kushinda mchezo wa bahati na sibu kama hujacheza. Link zifuatazo hapa chini zitakuwezesha wewe kuingia ktk bahati na sibu hiyo BILA GHARAMA YOYOTE, angalieni asiwatapeli mtu....HAKUNA CHA AGENT................its very simple fuata maelekezo, fill in the forms tuma application yako instantly online:

fungua hii link ya kwanza halafu ujaze fomu, link nyingine mbili chini yake ni kukupa maelezo zaidi kwa ajili ya kuelewa nini unafanya: KUMBUKA KUFUATA MAELEKEZO especially ktk picha. Hebu chekini humu.

http://www.dvlottery.state.gov/


http://travel.state.gov/visa/immigra...ypes_1318.html


http://www.usimmigrationsupport.org/...rdlottery.html

Mzee Kassum



Mzee Alnoor Kassum akisalimiana na mama Maria Nyerere jana ikulu alipozindua kitabu kiitwacho 'africa's wind of change' kilichoandika Kassum ambaye ni mmoja wa mawaziri waliokuwa kwenye kabineti ya awamu ya kwanza. ukitaka kuona picha zaidi nenda kwa Haki Ngowi upate habari zaidi.

Monday, October 08, 2007

Kima cha chini sekta binafsi juu



NI kama vile taarifa ya kufurahisha, lakini iliyojaa mzaha mwingi na yenye lengo bila shaka la kufuta hasira za walalala hoi wa mitaani wanaotaabika kwa udi na uvumba wakisaka mkate wao wa kila siku. Serikali imetangaza rasmi kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi huku wafanyakazi wa majumbani wakipangiwa Sh 65,000, wafanyakazi wa sekta ya madini Sh 350,000 na wahudumu wa baa na nyumba za kulala wageni Sh 80,000 kwa mwezi na kitaanza kutumika rasmi Novemba Mosi.

Viwango hivyo vipya vimetokana na utafiti uliofanywa na Bodi ya Uchunguzi wa Mishahara katika sekta binafsi, ambayo iliteuliwa Aprili mwaka huu na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, John Chiligati, kufuatia Sheria mpya ya Kazi namba 7/2004, kifungu namba 35 (1).

Akitangaza mishahara hiyo jijini Dar es Salaam jana, Waziri Chiligati, alisema viwango hivyo vipya vya kima cha chini vitahusu wafanyakazi wa sekta binafsi pekee.

Alisema mishahara hiyo mipya inagusa sekta zote ikiwemo ya kilimo, madini, afya, biashara na viwanda, ulinzi wa makapuni binafsi, huduma za usafiri na mawasiliano, maji, pamoja na wafanyakazi wa majumbani na mahotelini. Bonyeza hapa upate kusoma habari hii ya gazeti la Mwananchi kwa kina zaidi.

Saturday, October 06, 2007

Breaking Newss: FT Interview: Jakaya Kikwete

FT: Agriculture has been the laggard. What's holding it back?

JK: Why I'm saying that there is great opportunity is because agriculture is mostly subsistence agriculture, peasant agriculture…and therefore production is low and the incomes of the people definitely are very low. What we are trying to do now is embark on a green revolution…looking at increasing irrigated agriculture, increasing the use of high yield seeds…the use of fertilisers. The average use of fertiliser is abysmally low; it is eight kilos per acre. When you compare with the Netherlands where it's 577 kilos per acre, so you can see why…the level of (production) is very low.

FT: Do you need to reform the land ownership laws to allow…?

JK: It's not this. Land ownership has never been a problem. People have access to land. The peasants cannot complain about land ownership.

FT: But to access credit they need land titles as collateral for the banks?

JK: It's not a problem of land ownership because owning land is also allowed. It's only that they don't have the titles. But this to us is not a critical problem. The other important thing is that they use pesticides and insecticides. We are looking at extension workers to train farmers…and then we are looking at the marketing structure. We are also looking at infrastructure, rural roads so that crops can get to the market. This is a whole package; you are looking at a seven-year programme. We are also trying to look at the fiscal incentives to give to investors.

FT: There's some controversy about incentives that have been provided in the past, for example in the mining sector.

JK: In the mining sector, I don't know if we've got a controversy…What became a problem is there was a clause that allowed investors to cover losses. As long as you made losses one year, you could carry them over to the next and to the next. And because of that they would pay no taxes. So this fellow takes all the gold away and he says he makes losses and so he does not pay us anything. So he is the only one that is being protected. Those of us who are losing our resources are not protected. This is the thing that created the kind of debate that we had and we had to renegotiate. Click Here for more interview.

JK kuwasili Dar kesho



Rais Jakaya Kikwete leo anatarajiwa kurejea nyumbani kutoka ziara yake ya wiki tatu nchini Marekani, ambako pamoja na mambo mengine alihudhuria Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete atawasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates.

Taarifa hiyo ilisema wakati wa ziara yake, iliyoanza Septemba 15, amefanya mambo mengi yenye manufaa kwa nchi katika nyanja za siasa, uwekezaji, utalii, madini, michezo, biashara, elimu na utamaduni.

Miongoni mwa mafanikio hayo ni pamoja na kuzidisha kwa uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani ambako taifa hilo kubwa limeahidi kusaidia mafunzo katika maeneo ya kijeshi.

Katika eneo la uwekezaji, makampuni kadhaa yameonyesha nia ya kujenga viwanda vya mbolea nchini na miradi mingine. Miongoni mwa makampuni makubwa yaliyoihakikishia Tanzania fedha za kuwekeza katika uchumi ni JP Morgan, Merrill Lynch, Tegris na Gibraltar Properties,

Wakati wa ziara yake, rais alizindua matangazo ya vivutio vya utalii wa Tanzania katika televisheni ya kimataifa ya CNN.

Makampuni kadhaa ya Marekani pia yamekubali kuwekeza katika utalii wa Tanzania miongoni mwao ikiwemo kampuni maarufu ya mahoteli ya Global Hyatt Corporation, ambayo imekubali kuja Tanzania na kuangalia maeneo ya kujenga mahoteli.

Kelele zetu inabidi zifikie mwisho

INAONEKANA kama vile kuna mwamko fulani miongoni mwetu dhidi ya ufisadi, kwa kila mmoja kuonyesha utaalamu wake wa kuzungumza kadiri awezavyo.

Wengine wameingia mikataba ya kutopokea rushwa wakasaini kwa mbwembwe, na bashasha kubwa lengo likiwa ni hilo hilo.

Wahariri nao wakatia saini kule Ubungo Plaza wakapitisha maazimio, nao wanataka kupambana na ufisadi na wakaapa kabisa kwamba lazima waikomeshe rushwa. Sijui nini kimewatuma sasa badala ya kuanza kuchachamaa kabla.

Kabla ya hapo, nimemsikia mzee wangu Dk Willibrod Slaa akiwaanika hadharani wale aliodai kuwa ni mafisadi wakuu wa nchi hii na hajaishia hapo amebeba ile orodha ya mafisadi na akahama nayo kwenda huko Marekani. Bonyeza hapa upate kusoma uchambuzi huu zaidi.

Friday, October 05, 2007

Serikali yawapigia magoti wafadhili



HATIMAYE serikali imekubali kuchunguza tuhuma za ufisadi wa mabilioni ya fedha za umma zilizotolewa na Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Willibrod Slaa, dhidi ya vigogo 11 na kuonya kuwachukulia hatua za kisheria au kuwawajibisha watakaopatikana na hatia.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni siku chache baada ya mabalozi wa nchi mbalimbali, ikiwamo Uholanzi Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), Marekani, Ujerumani, Benki ya Dunia na viongozi wa dini kuitaka serikali kutoka tamko linaloeleweka na la wazi kuhusu tuhuma hizo.

Uamuzi huo ulitangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kwa niaba ya serikali, alipozungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, jijini Dar es Salaam jana na kauli hiyo pia aliirudia jana mchana alipokutana na mabalozi wa nchi za nje wanaowakilisha nchi zao Tanzania.

Waziri Membe alisema ana uhakika Rais Jakaya Kikwete na serikali yake ya awamu ya nne, atahakikisha baada ya uchunguzi wa tuhuma hizo kukamilika, wahusika wanachukuliwa hatua za kisheria au kuwajibishwa.

Jamani watoto wetu

Watoto wetu jamani, ajali ajali hebu cheki hapa wanavuka barabara bila usimamizi wowote hapa ilikuwa karibu kabisa na Ikulu, hawa ni watoto wa shule ya msingi Kigamboni walikutwa na Mdau Deus Mhagale.

Wednesday, October 03, 2007

Kundi zima la Sisi Tambala

Nadhani mtakumbuka kibwagizo maarufu katika TV ambacho kinaimbwa perupe pepero perupe pepero hawa ni vijana wa Sisi Tambala waliokuwapo katika ziara ndefu ya nchini China wamerejea. Wasanii hao tisa wa kikundi cha sanaa cha `Sisi Tambala` cha jijini Dar es Salaam waliwasili toka China kushiriki tamasha la dunia la sanaa na muziki.

Jijini Dar walipokewa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Profesa Herman Mwansoko.

Kibiriti wa Sisi Tambala akinyanyua juu kikombe cha ushindi.

Wakipokelewa na Profesa Mwansoko.



Picha zote hizi kutoka kwa mdau Kassim Mbarouk.

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...