Saturday, March 31, 2018

RC SHIGELLA MGENI RASMI TANGA CITY MARATHON JUMAMOSI WIKI HII MJINI TANGA


Mratibu wa Mashindano ya Riadha ya Tanga City Marathon, Juma Mwajasho kulia akitetea jambo na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya kuelekea mashindano hayo Jumamosi wiki hiikushoto ni Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao niwaandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein na Katibu wa Chama cha Riadha Mkoani Tanga (RT) Hassan Mwagomba
Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uwepo wawashiriki kutoka Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapat afursa ya kuonyesha umahiri wao kulia ni Meneja wa Mkwabi Super Marketya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein,
Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo, KawkabHussein akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano huu kuhusiana na zawadi zitakazotolewa msimu huu
Sehemu ya medali zitakazotolewa kwenye mashindano hayo



MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella ametarajiwa kushuhudia mashindano ya riadha ya Tanga City Marathon msimu wa piliyanayotazamiwa kufanyika Jumamosi wiki hii mjini hapa.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mratibu wa Mashindano hayo, Juma Mwajasho alisema maandalizi yamekamilika kwa asilimia kubwa huku baadhi ya washiriki wakithibitisha kushiriki.

Alisema katika mashindano hayo msimu huu watazamia washiriki zaidi ya600 ambapo washindi watakabidhiwa zawadi mbalimbali zikiwemo medali ambazo zimeandaliwa na wadhamini wa mashindano hayo.

Aidha alisema mashindano hayo yatashirikisha wakimbaji kwenye umbali wa kilomita 21,10 na 5 ambapo wataanzia mbio hizo kwenye eneo la Mkwabi Super Market kuzunguka maeneo mbalimbali Jijini Tanga na kuishia eneo hilo.

“Lakini kwa mara ya kwanza washiriki wote watakaoshiriki mashindano hayo watapewa medali na mgeni rasmi kwenye mashindano hayo.Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Riadhaa Mkoa wa Tanga (RT) Hassan Mwagomba alisema mashindano hayo pia yatashirikisha washiriki kutoka Visiwa vya Shelisheli, Unguja na Pemba ambao watapata fursa yakuonyesha umahiri wao.

Alisema njia zitakazopitia mashindano hayo zimeboreshwa zaidi kiusalama kwa wakimbiaji ili kuweza kuepukana na adhari zinazoweza kujitokeza wakati yakiendelea.Naye kwa upande wake,Meneja wa Mkwabi Super Market ya Jijini Tanga ambao ni waandaaji wakuu wa mbio hizo,Kawkab Hussein alisema msimu huo wameboresha mashindano hayo kwa kutoa zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa kumi.

Alizitaja zawadi zinazotolewa kuwa ni mshindi wa kwanza km 21 atapata700,000 wa pili 500,000, huku mshindi wa tatu akipata 300,000 huku wengine kuanzia wa nne hadi wa kumi watapata kifuta jasho cha 50,000.

Hata hivyo alisema katika kilomita 10 mshindi wa kwanza atapata 250,000, wa pili 150,000 na wa tatu 100,000 huku washindi wa kuanzia nafasi ya nne mpaka 10 watapewa 30,000 pia kutakuwa na vituo maalumu kwaajili ya kutoa huduma ya maji kwa wakimbiaji (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)

No comments: