Tuesday, April 03, 2018

SHIRIKA LA NYUMBA LIKO IMARA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YAKE

 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akikaribishwa kwenya Shirika la Nyumba la Taifa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Feix Manyama Maagi muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya Shirika na kufanya ziara kufuatilia utendaji wa Shirika hilo.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akizungumza na menejimenti ya NHC leo hii.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Operesheni za Mikoa, Suzane Kyaruzi wakati alipotembelea Shirika.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akizungumza na menejimenti ya NHC leo hii.


 Waziri Lukuvi akiangalia namna ya utunzaji wa nyaraka za serikali kwenye mojawapo ya ofisi ya Shirika 


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi amewahakikishia Watanzania kuwa Shirika la Nyumba la Taifa liko imara kwaajili ya kutekeleza malengo lililopangiwa na serikali
Waziri Lukuvi ameyasema hayo leo wakati alipotembelea Shirika la Nyumba la Taifa kujionea utendaji kazi na kuwatakia heri na kuhimiza utendaji kazi wenye tija kwa Shirika.
Aliwataka wafanyakazi wa Shirika kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa huku akiwahakikishia kwamba Serikali ipo nyuma yao na ina matarajio makubwa ya kuhakikisha Wafanyakazi hao wanatimiza malengo ya Serikali ya kujenga nyumba 50,000 kwaajili ya Watanzania.
“Shirika la Nyumba lipo, lilikuwapo, litaendelea kuwapo kwasababu Serikali ipo, nyinyi endeleeni kuchapa kazi kwa bidii, tunawategemeeni muendelee kuhakikisha Shirika linabaki salama. Mambo mengine yanayotuhusu Serikali tuachieni sisi, siyo ya kwenu,” amesema.
Alitaka kila mfanyakazi atekeleze majukumu yake kwa tija ili Serikali iendelee kuvuna faida na kupata matokeo chanya ambayo yatafaidisha Watanzania wengi zaidi.
Alisema Shirika la Nyumba linaaminika na lina uwezo wa kutekeleza majukumu yake kama kawaida na kutaka miradi yote iliyoanza kujengwa ikamilishwe kwa wakati ili kusudi shughuli ya kuianza miradi mingine mingi zaidi ifanyike.
Waziri Lukuvi amehimiza jitihada ziongezeke katika ubunifu wa nyumba za gharama nafuu, ili nyumba zinazojengwa ili ziwe za gharama nafuu kweli.” Nyinyi ndiyo Champion wa kusimamia ujenzi wa nyumba za gharama nafuu hatutarajii Watanzania wakalalamikia nyumba zenu kuwa za bei juu.”
“Ni kweli mmejenga nyumba nyingi sana pale Iyumbu, Rais Magufuli amewasifieni sana na amefurahi, lakini suala linabaki hapa hoja siyo kujenga nyumba nyingi bali ni kujenga nyumba nyingi za gharama nafuu ziwafikie na kumilikiwa na Watanzania wengi zaidi,”amesema.


No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...