Monday, March 26, 2018

UBER IMEZINDUA HUDUMA MPYA YA uberPOA JIJINI DAR ES SALAAM

 
.Leo kampuni ya Uber imetangaza ujio wa huduma mpya ya uberPOA huduma hii ni ya bei nafuu inayolenga bajaji ikiwa ni juhudi za kupiga jeki huduma ya uberX jijini Dar es Salaam. Huduma hii mpya, ambayo wateja wataanza kufurahi kuanzia leo, itatolewa na bajaji au tukutuku ambazo zinatumia mafuta kidogo. uberPOA itawapa wasafiri wa sasa na wapya fursa ya kutumia huduma ya bei nafuu wanapofanya safari zao jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia huduma hii, Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, Bw. Alfred Msemo amesema, ‘Leo tunafuraha kubwa tunapozindua huduma hii ya uberPOA ambayo ni ya bei nafuu itakayotolewa na bajaji. Tuna furaha kwa sababu uberPOA inawapa wasafiri uhuru wa kuchagua huduma ya usafiri ambayo ni ya bei nafuu zaidi. Ujio wa huduma hii ni mkakati endelevu wa juhudi makusudi za kutumia ubunifu utakaoimarisha huduma tunazotoa katika kuafikia dhamira yetu ya kutoa usafiri salama, wa uhakika, na kwa bei nafuu jijini Dar es Salaam.” 

uberPOA itatumia bajaji ambazo kwa ujumla hazina gharama kubwa ya matengenezo. Huduma ya UberPOA itatolewa sanjari na huduma ya sasa ya uberX inayotolewa na magari madogo ya aina ya sedan. “Tuna imani kwamba wasafiri jijini Dar es Salaam wana haki ya kuwa na uhuru wa usafiri ambao wangependa kutumia wanapofanya shughuli zao katika jiji letu, usafiri ambao ni wa bei nafuu na wenye kuleta ufanisi mkubwa katika maisha yao - uberPOA inatoa fursa hii.” Ameongeza Bw. Msemo.

Bei ya chini ya uberPOA itakuwa Tsh 1,500, Tsh 400 kwa kila KM, Tsh 80 kwa kila dakika, nei ya chini kabisa ambayo msafiri anaweza kulipa ni Tsh 2,000 na ada ya kughairi safari ni Tsh 2,000. “Kampuni ya Uber tunaamini ya kwamba wasafiri na washirika wetu wana kila sababu ya kujua nauli watakayolipa na namna wanavyotumia Uber katika shughuli zao za kila siku.” Amesema Bw. Msemo.

Wakati wa kuzindua huduma hii ya UberPOA, kampuni ya Uber imekariri kwamba imeweka mkakati utakaowahikikishia madereva kiasi fulani cha mapato katika kipindi hiki wanapozindua huduma hii hapa jijini. Ili wasafiri wapate huduma hii, wanatakiwa kufungua programu yao ya Uber ambapo watakuwa na nafasi ya kuita usafiri wa UberPOA au UberX. Kwa sasa huduma ya uberPOA inapatikana maeneo ya Mwenge, Sinza, Kijitonyama, Mikocheni A, Mwananyamala, Kinondoni, Namanga, Msasani, Oysterbay, Masaki & Kigamboni ingawa huduma hii inasambaa maeneo mengi katika siku za baadaye.

Uber imejijengea utaratibu wa kuzindua bidhaa mpya, hali ambayo inaleta upatikanaji wa huduma aina mbalimbali ambazo zitakuwa na tija kubwa kwa wasafiri na madereva washirika. Katika nchi jirani ya Kenya, tayari kampuni ya Uber imezindua huduma kadhaa kama vile uberCHAPCHAP, uberX na UberSELECT. Katika miji mbalimbali duniani kampuni ya Uber inatoa huduma kama vile uberMOTO, UberXL, UberBLACK, UberCHOPPER, UberASSIST, UberEXEC na UberPool.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...