Marehemu Jackline Kilawe (Pichani) enzi za uhai wake
Marehemu Jacline Kilawe enzi za uhai wake
Baadhi ya waombolezaji wakitoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Kimara Korogwe kulikofanyika ibada ya kumuaga Marehemu Jackline John Kilawe kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Felix Maagi akijadiliana jambo na Edna Choggo ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Omari Makalamangi, Meneja wa Rasilimaliwatu kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Kimara Korogwe kulikofanyika ibada ya kumuaga Marehemu Jackline John Kilawe kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi.
Waombolezaji wakijadiliana jambo kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Kimara Korogwe kulikofanyika ibada ya kumuaga Marehemu Jackline John Kilawe kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi.
Waombolezaji wakifuatilia michakato ya uagaji mwili wa Jackline kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Kimara Korogwe kulikofanyika ibada ya kumuaga Marehemu Jackline John Kilawe kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi.
Mwili ukipandishwa kwenye gari kwaajili ya kusafirishwa kwenda Moshi.
Baadhi ya Waombolezaji wakifuatilia sala iliyokuwa ikiendelea ndani ya gari kabla ya kuusafirisha mwili.
Historia fupi ya Marehemu
Marehemu Jackline John Kilawe alizaliwa tarehe 27/03/1984
mkoani Arusha.
Alipata elimu yake ya sekondari kidato cha kwanza mpaka cha
nne katika Shule ya Sekondari Marangu – mkoani Kilimanjaro, kuanzia mwaka 1999
mpaka 2002, na elimu ya kidato cha tano na sita mwaka 2003 mpaka 2005 katika
Shule ya Sekondari Mkwawa – mkoani Iringa. Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari
marehemu alijiunga na Stashahada ya Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa katika Chuo
cha Diplomasia na Uhusiano wa Kimataifa cha Dar es Salaam kilichopo kurasini
ambapo alihitimu mwaka 2010.
Baadaye alijiunga na Shahada ya kwanza ya Sanaa na Mawasiliano
kwa Umma mwaka 2011 hadi 2014 katika Chuo cha Tumaini.
Katika uhai wake marehemu alifanya kazi sehemu mbalimbali zikiwamo
Wiltoc Co. Ltd, JafezTech Co. Ltd na Astra Insurance Broker Ltd.
Marehemu aliajiriwa katika Shirika la Nyumba la Taifa katika
Kurugenzi ya Utawala na Uendeshaji mikoa makao makuu tarehe 22/09/2014 katika
nafasi ya mapokezi na baadaye kuhamishiwa katika kitengo cha huduma kwa Wateja.
Vilevile marehemu alikuwa Mwakilishi wa Wafanyakazi kama
Mjumbe wa Tamico.
Marehemu alikuwa akisumbuliwa na kifua, mpaka umauti unamkuta
alfajiri ya tarehe 11/03/2018 alikuwa amelazwa katika hospitali ya Mloganzila –
Kibamba.
Shirika linasikitika sana kumpoteza mfanyakazi mahiri katika
kitengo cha Huduma kwa Wateja.
Shirika limetoa rambirambi ya fedha taslim, sanda, sanduku na
usafiri hadi nyumbani kwao Moshi, Kilimanjaro.
Pole kwa ndugu, jamaa na nyote mlioguswa na msiba huu. Mungu ailaze roho ya Jackline mahali pema peponi.
AMEN
No comments:
Post a Comment