Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inatarajia kufanya upasuaji mkubwa kwa njia ya matundu madogo(Laparoscopy Surgery) wa watoto watano ambao haujawahi kufanyika hapa nchini. Upasuaji huu utafanywa na madakari bingwa wa Muhimbili waliobobea katika upasuaji wa watoto kwa kushirikiana na mtaalamu kutoka Hospitali ya King Faisal ya nchini Saudia Arabia.
Upasuaji huu unatarajia kuanza Februari 20 hadi 25, mwaka huu ambao utahusisha upasuaji wa aina tano kwa watoto wadogo ambao ni;
a) Ni upasuaji wa nyama iliyojitokeza katika sehemu ya haja kubwa kwa watoto
b) Hatua ya pili ya upasuaji wa kushusha kokwa katika korodani
c) Upasuaji wa kushusha utumbo mkubwa na kutengenezea njia ya haja kubwa kwa watoto ambao wamezaliwa bila kuwa na njia ya haja kubwa.
d) Upasuaji wa kuondoa mfuko wa ziada kwenye koo kwa watoto.
e) Upasuaji kwa watoto wadogo ambao hawana celimbalimbali na hivyo kushindwa kusukuma choo kwenye utumbo mkubwa.
Upasuaji huu mkubwa utakaofanyika Muhimbili hufanyika kwa nchi zilizoendelea hivyo Tanzania ni mara ya kwanza kufanyika na utarajiwa kuleta mageuzi makubwa kwani upasuaji wa njia ya matundu maodogo ni wa kisasa na umeonekana kuwa na manufaa makubwa kwa wagonjwa ikiwemo kupona haraka na kuruhusiwa kwenda nyumbani mapema.
Imetolewa na;
Aminiel Aligaesha,
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma,
MNH-Februri 14, 2017.
No comments:
Post a Comment