Wednesday, February 15, 2017

AIRTEL YAMWAGA ZAWADI KWA WATEJA WA TECNO SMARTPHONE SIKU YA VALENTINE

Meneja wa Tecno Mobile Tanzania, Marco Wang akisoma jina la mshindi wakati wa kuendesha bahati simu ya jishindie Tecno smartphone kupitia promosheni maalumu iliyoendeshwa na Airtel pamoja na Tecno wakati wa msimu wa sikukuu ambapo mwisho wake ni leo na washindi 7 wamepatikana. Akishuhudia (wakwanza kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando, akifatiwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Bakari Majid , na kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba.
Afisa huduma kwa wateja wa Airtel , Bwn Pascal Maziku Akiokota jina la mshindi wakati wa kuendesha bahati simu ya jishindie Tecno smartphone kupitia promosheni maalumu iliyoendeshwa na Airtel pamoja na Tecno wakati wa msimu wa sikukuu ambapo mwisho wake ni leo na washindi 7 wamepatikana. Akishuhudia (wakwanza kulia) ni Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando, akifatiwa na msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha bwana Bakari Majid, na kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwn Jackson Mmbando akitangaza majina ya washindi wa promosheni maalumu iliyozinduliwa wakati wa msimu wa sikukuu inayowawezesha wateja wa Airtel kujishindia zawadi mbalimbali pindi watakaponunua simu za smart phone za Airtel. Washindi 7 wamepatikana katika droo ya Bahati nasibu iliyochezeshwa leo katika makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es saalam , akishuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba
Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma kwa wateja , Bi Adriana Lyamba akionyesha simu aina ya Tecno iliyokabithiwa kwa washindi wakati wa droo ya bahati nasibu iliyochezeshwa katika ofisi za makao makuu ya Airtel jijini Dar es Saalam
Wafanyakazi wa Airtel na wafanyakazi wa Tecno wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kuchezesha droo ya bahati nasibu,
  • Wateja kujishindia vifaa mbalimbali vya majumbani kupitia droo ya Bahati nasibu
·         Airtel na Tecno wawazawadia wateja wake wa SmartphoneKampuni ya mkononi ya Airtel Kwa kushirikiana na Tecno mobile  leo imewazawadia wateja wake kupitia promosheni iliyozinduliwa maalumu kwa msimu wa sikukuu za crismass, mwaka mpaya na valentine kwa lengo la kuwahamasisha wateja kutumia simu za kisasa za smartphone na kujishindiaPromosheni hiyo ilihusisha wateja wa Airtel wanaonunua simu aina ya TECNO N6 and TECNO W3  kwa kipindi cha sikukuu za krismasi, mwaka mpya na valentine na kisha kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ili  kujishindia vifaa mbalimbali vya nyumbani vikiwemo , Televisheni, Mashine ya kutengenezea Juisi, Jiko la kuchoma nyama, Mashine ya kutengeneza Sandwich , Brenda mashine pamoja na simu za smartphone za TECNO W4 mbiliAkiendesha droo hiyo iliyofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema “Airtel tuefika mwisho wa promosheni yetu lakini bado smartphone zinapatikana katika maduka yetu zikiambatana na ofa kabambe.  Napenda kuwashukuru wote walijiunga na ulimwengu wa smartphone kupitia promosheni hii nakuwaomba wateja wetu wengine waendelee kutembelea maduka yetu ili kupata simu za kisasa kwa bei nafuu na kufurahia huduma zetu bora ikiwemo, Airtel Money Relax, huduma ya Inteneti na nyingine nyingi”Kampuni ya Airtel ilizindua promosheni ya shinda na Smartiphone mwishoni mwa mwaka jana ili kila mteja wake anaenunua simu aweze kupata nafasi ya kushinda.  






No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...