Tuesday, February 21, 2017

MADIWANI MUFINDI WAPITISHA ENEO JIPYA LA UJENZI WA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI

 Mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa eneo la ujenzi wa makao makuu.
Mwenyekiti wa kamati  iliyokuwa imeundwa kwa ajili ya kutafuta eneo la ujenzi Bw. Ubisimbali Jeswald akiwasilisha kazi yao kwa baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindiwakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa kamati wakati anawasilisha kazi walioifanya na kamati hiyo.

Hatimaye baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limepitisha na kulitambua rasmi eneo lililopo kata ya Igowole kuwa ndipo zitakapojengwa Ofisi za makao makuu ya halmshauri hiyo hivyo, kuruhusu kuanza kwa ujenzi wa mradi wa kwanza wa hospitali ya halmshauri ya Wilaya katika eneo teule.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Ofisa habari na mawasilino wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake  Mwakapiso, amesema baraza hilo limefanya uamuzi huo wa  kihistoria wakati wa kikao cha baraza maalum lililoitishwa kwa mujibu wa kanuni  kwa agenda maalum ya kuridhia mapendekezo ya kamati teule ya wataalamu iliyopendekeza maeneo katika   vijiji vya Ibatu na Nzivi vilivyopo kata ya Igowole.

Ofisa habari huyo, ametaja baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa wakati wa kulipitisha eneo hilo, kuwa ni pamoja na utayari wa wananchi na halmshauri za vijiji kulitoa eneo bure bila kudai fidia, Eneo kuwa ubali wa km 13 kutoka barabara kuu, eneo  kupendekezwa kwa asilimia 29 wakati wa mchakato wa kusaka maoni katika kata 27 za halmshauri, likifuatiwa na Nyololo kwa asilimia 25 sanjari na Ukubwa wa eneo lenyewe likiwa na ekali 127.

Uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni takribani mwaka mmoja baada ya kuzaliwa kwa halmshauri mpya ya Mji wa Mafinga ambao kwa sasa ndiyo wenye mamlaka kamili ya kuuendesha mji huo. Aidha, uongozi wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi umewashukuru wenyeviti wa kamati za kata na wanamufindi kwa ujumla wao kwa ushirikiano waliounesha wakati wa  kupendekeza eneo la ujenzi wa  makao makuu ya halmshauri.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...