Wednesday, February 22, 2017

MKUU WA MKOA WA ARUSHA ASHIRIKIANA NA WANANCHI KATIKA KAZI ZA MAENDELEO MONDULI


Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto)akipokea kutoka kwa Mhandisi Shin Pil Soo sehemu ya msaada mabati 300 na mifuko ya Sementi 500 iliyotolewa na Kampuni ya ujenzi ya Hanil Jiangsu Joint Venture Ltd inayojenga barabara ya Sakina hadi Tengeru yenye urefu wa kilometa 14.1 ,kulia ni Meneja wa Tanrods mkoa wa Arusha,Mhandisi John Kalupale,msaada huo umetolewa kwa Mkuu wa mkoa ili umwezeshe kusaidia shughuli za maendeleo zilizoanzishwa na wananchi na alikabidhi ili utumike kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Makuyuni wilayani Monduli. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishirikiana na askari wa JKT kambi ya Makuyuni na wananchi wa Kata ya makuyuni katika ujenzi wa Kituo cha Afya katika ziara yake wilayani Monduli. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(katikati) akilakiwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rifit Valley Kata ya Majengo wilaya ya Monduli,kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Idd Kimanta na kulia ni Mkuu wa Shule,Julius Maghembe. 
Mkuu wa Shule ya Sekondari Rift Valley ,Julius Maghembe akiinua Sh 500,000 zilizotolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho gambo kwaajili ya kununua viti vitano vya walimu. 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto) akiwa na viongozi wa wilaya ya Monduli ndani ya moja vya vyumba viwili madarasa vilivyozinduliwa baada ya ujenzi wake kukamilika katika Shule ya Sekondari Rifit Valley. 
Wananchi wakichangia nguvu zao katika ujenzi wa jengo la Upasuaji kwenye Kituo cha Afya Mto wa Mbu 
Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishiriki kazi za mikono pamoja na wananchi katika ujenzi wa jengo la Uapsuaji katika Kituo cha Afya Mto wa Mbu aliahidi kutoa mifuko 100 ya Sementi na Mabati 100. 

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...