AWAPA SIKU 14, WAFANYA BIASHARA NJE YA SOKO KUAMIA NDANI YA SOKO
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza na Wananchi mapema leo kwenye muendelezo wa ziara yake jijini Dar
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akisikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Wanachi wa Mzimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi.
Na Anthony John Glob Jamii.
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameendelea na ziara ya kutembelea Kata za wilaya ya kinondoni, ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkuu wa wilaya ametembelea kata Mzimuni, akiwa katika soko la Magomeni, ametoa siku 14 kwa uongozi wa soko hilo kuhakikisha wanaondoa baa na ghala vilivyopo katikati ya soko hilo.
Akiwa ndani ya soko hilo, Hapi alisema inasikitisha kuona hata wamiliki wa ghala hizo hawafahamiki.Alisema uwepo wa ghala na baa katikati ya soko hilo inasababisha kuwanyima fursa wafanyabiashara walio wengi hasa wale wadogo.
"Ninatoa siku 14 kwa viongozi wa soko na manispaa kuhakikisha wanaaondoa maghala haya kwani inaonyesha ni ya wafanyabiashara wakubwa hivyo waende kwa wenzao hapa hapawafai,"alisema Hapi.
Sambamba na hilo mkuu huyo ametoa siku 14 nyingine kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko hilo kurejea ndani ya.soko.Alisema sheria zipo wazi na hakuna aliyejuu ya sheria zaidi ya kuzingatia sheria hizo.
"Hakuna aliyeruhusu wafanyabiashara wengine kufanya biashara nje ya soko, hivyo naagiza ndani ya siku 14 wote mhamie ndani kwa sababu mnaleta usumbufu kwa wengine na kuleta malalamiko,"alisema Hapi.
Baadae mkuu wa wilaya alifanya mkutano wa adhara katika shule msingi Mikumi, katika mkutano huo wananchi waliuliz maswali mbali mbali lakini kero kubwa imeonekana kuwa viongozi wao sio waaminifu hukusanya pesa kwa wananchi lakini hafanyi yaliyokusudiwa, mkuu wa wilaya akijibu hoja hiyo ameagiza viongozi wote kutoa risit za EFD kwa kila malipo yanapofanyika
No comments:
Post a Comment