SOKO dogo lililopo eneo la Forest ya zamani, karibu na Chuo Kikuu cha Mzumbe na Chuo Kikuu Huria jijini Mbeya, limeteketea kwa moto jana usiku. Inadaiwa moto huo ulianza majira ya saa 3 za usiku na kudhibitiwa na zimamoto kabla ya kuleta madhara zaidi.
Tukio hili limetokea ikiwa ni siku moja kutoka soko lingine la Mwanjelwa eneo la SIDO kuteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa. Matukio haya yanayotokea jijini Mbeya yanaacha maswali mengi kwa wananchi kiasi cha kuhoji 'KUNANI MBEYA ?'
Picha kwa hisani ya Mbeya Yetu Blog
No comments:
Post a Comment