Monday, September 19, 2011

Rais Ali Mohammed Shein awapa pole Mtambwe


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na wananchi wa familia 70 wa Kisiwani Piki na Mzambaun Takao,waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni, akiwa katika ziara maalum ya kuwapa pole wananchi waliofili na jamaa zao katika kisiwa cha Pemba.

Waziri wa Ardhi,Makaazi,maji na Nishati Mhe Ali Juma Shamuhuna,akiwapa pole wananchi wa Mtambwe Daya waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja ikielekea Pemba,hivi karibuni

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwamamwema Shein,akiwapa pole wananchi wa Mtambwe Daya waliofiliwa na jamaa zao katika ajali ya Meli ya Mv Spice Islander,iliyozama katika mkondo wa Nungwi kaskazini Unguja ikielekea Pemba,hivi karibuni.

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...