Friday, April 02, 2010

Ujumbe wa Tanzania Kwenye Mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU)


Spika wa Bunge Samuel sitta akitoa shukrani zake kwa Balozi Cisco Mtiro kwa mapokezi mazuri (kulia) kwa niaba ya ujumbe wa Tanzania unaohudhuria mkutano wa 122 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wakati wa chakula cha usiku jana,katika Hotel ya Conrad mjini Bangkok. Balozi Cisco licha ya kuwa Ubalozi wake upo Kuala Lumpar Malaysia, pia anashughulikia nchi ya Thailand ambapo kwa kipindi hiki cha mkutano wa 122 wa IPU naye yupo Bangkok kuratibu ugeni wa Tanzania katika nchi hii.

Spika wa Bunge Samuel Sitta na Balozi Sisco Mtiro wakibadilishana vitabu vilivyo tiwa sahihi za wajumbe waliohudhuria Mkutano wa 122 wa IPU toka Tanzania na wageni waalikwa kama ishara ya kumbukumbu ya mkutano huo. Picha na Afisa Habari wa Bunge Owen Mwandumbya

No comments:

WIZARA YA ARDHI YAPONGEZWA KUTENGA FEDHA KUKAMILISHA MRADI WA MAKTABA

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeipongeza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kutenga fedha kiasi cha Shiling...